TAARIFA MPYA

Madhara ya Chai na Kahawa Kiafya

Picha
CAFFEINA/KAFEINA. Kafeina ni nini?: 1. Kafeina ni madawa ya kulevya kundi la ‘Stimulants drugs’. Utashangaa. Habari ndiyo hiyo. Hii ndiyo sababu kwa mtu aliyezoea kunywa chai hii kila siku au kahawa, siku asipokunywa kichwa humuuma, ni kwa sababu amekuwa mtegemezi au teja wa kafeina. Kafeina ni kiungo mhimu karibu katika soda zote zenye rangi nyeusi; Coca-cola, Pepsi, Sayona nyeusi, Azam cola na kadharika. Kafeina huongezwa pia katika Red bull, Malta na katika baadhi ya dawa za kupunguza maumivu mwilini. Kwahiyo Kafeina ambayo hupatikana katika chai na kahawa ni aina mojawapo ya madawa ya kulevya. 2. Kafeina ni kikojoshi (diuretics). Kafeina ni dawa ya kukufanya ukojowe. Ukinywa kikombe kimoja cha kinywaji chenye kafeina yaani chai au kahawa, basi muda si mrefu utaenda kukojoa vikombe viwili. Kwa sababu kafeina ni taka isiyotakiwa mwilini, mwili utafanya kila uwezalo ikibidi ujikamuwe wenyewe kupata maji ya ziada kuweza kuitoa kafeina hii uliyoinywa kwa kisingizio ch...

Wanachama wa UN watupilia mbali Vitisho vya Trump

New York. Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zimekaidi vitisho vya Serikali ya Marekani na kupiga kura ya ndiyo kuidhinisha azimio linalotupilia mbali tangazo la Rais Donald Trump kuutambua mji wa Jerusalem kama makao makuu ya Israel.

Nchi wanachama 128 zilipiga kura ya ndiyo dhidi ya kura tisa zilizopinga, huku nchi 35 zikijiondoa kupiga kura.

Baada ya kura, Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Nikki Haley aliyashukuru mataifa 65 yaliyopinga azimio hilo, yaliyojizuia kupiga kura au hayakuwapo wakati wa kupiga kura.

Marekani, Togo, Honduras na Guatemala ni mataifa ambayo yalipiga kura kupinga azimio hilo.

Mataifa ya Canada, Mexico, Rwanda, Uganda, Poland, Jamhuri ya Czech na Romania hayakupiga kura.

Kabla ya kura, Marekani ilitishia kuzuia misaada kwa mataifa yatakayopiga kura kuunga mkono azimio hilo.

Haley amesema kura hiyo haitabadilisha kitu katika mipango ya Marekani kuhamishia ubalozi wake mjini Jerusalem kutoka Tel Aviv.

Maoni

ZILIZO SOMWA MARA NYINGI

ULAJI WA MARA KWA MARA WA MBEGU ZA MABOGA HUKUKINGA NA KUKUEPUSHA NA MAGONJWA 1O MWILINI MWAKO...

Dalili 6 zitakazokuonyesha kuwa mwenzi wako ana mtu mwingine katika mahusiano

FAIDA YA JUICE YA KAROTI KATIKA MWILI WA BINADAM

DAWA BORA YA NGUVU ZA KIUME NA MAUMBILE MADOGO

AINA ZA MBOLEA & MATUMIZI YAKE KITAALAM

Madhara ya Chai na Kahawa Kiafya

Fahamu Aina 7 Za Juisi Zenye Kuondoa Sumu Mwilini

Ugonjwa wa Chango La Uzazi

Madhara Ya Kuangalia Video za Porno {Ngono} na Namna ya Kujizuia

Athari za kiafya za vyakula vyenye Wanga