TAARIFA MPYA

Madhara ya Chai na Kahawa Kiafya

Picha
CAFFEINA/KAFEINA. Kafeina ni nini?: 1. Kafeina ni madawa ya kulevya kundi la ‘Stimulants drugs’. Utashangaa. Habari ndiyo hiyo. Hii ndiyo sababu kwa mtu aliyezoea kunywa chai hii kila siku au kahawa, siku asipokunywa kichwa humuuma, ni kwa sababu amekuwa mtegemezi au teja wa kafeina. Kafeina ni kiungo mhimu karibu katika soda zote zenye rangi nyeusi; Coca-cola, Pepsi, Sayona nyeusi, Azam cola na kadharika. Kafeina huongezwa pia katika Red bull, Malta na katika baadhi ya dawa za kupunguza maumivu mwilini. Kwahiyo Kafeina ambayo hupatikana katika chai na kahawa ni aina mojawapo ya madawa ya kulevya. 2. Kafeina ni kikojoshi (diuretics). Kafeina ni dawa ya kukufanya ukojowe. Ukinywa kikombe kimoja cha kinywaji chenye kafeina yaani chai au kahawa, basi muda si mrefu utaenda kukojoa vikombe viwili. Kwa sababu kafeina ni taka isiyotakiwa mwilini, mwili utafanya kila uwezalo ikibidi ujikamuwe wenyewe kupata maji ya ziada kuweza kuitoa kafeina hii uliyoinywa kwa kisingizio ch...

Mkurugenzi kuchunguzwa baada ya utendaji Mbovu wa kazi

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Morogoro VijijiniSudi Mussa Mpiri atafanyiwa uchunguzi kutokana na utendaji wake kutoridhisha ikiwemo kushindwa kutekeleza miradi ya maendeleo.

Agizo hilo la kufanyiwa uchunguzi limetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo, ameagiza kufanyika uchunguzi wa haraka kwa mkurugenzi huyo baada ya kutoridhishwa na miradi ya maendeleo aliyoitembelea.

Mussa Mpiri anadaiwa kushindwa kutoa ufafanuzi wa fedha zilizopokelewa na Halmashauri hiyo kiasi cha sh.milioni 1.6 ya mapato ya ndani. Imeelezwa pia zaidi ya asilimia 90 ya matumizi ya pesa hizo hayafahamiki hivyo kutia shaka juu ya utendaji wake.

Kufuatia hatua hiyo Waziri Jafo, ameagiza kitengo cha uchunguzi na ufuatiliaji kilichopo Ofisi ya Rais TAMISEMI kufika haraka ndani ya Halmashauri hiyo kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini mwenendo wa Mkurugenzi huyo.

Jafo amewataka madiwani wa Halmashauri hiyo kufahamu kwamba wao wapo kwa niaba ya wananchi wanyonge hivyo wanapaswa kulinda na kusimamia  rasilimali za Halmashauri hiyo.

Maoni