TAARIFA MPYA
BAS LAUWA SAFARINI
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Zawadi Seif Mlawa mwenye umri wa miaka 37 mkazi wa Morogoro, amefariki dunia baada ya kugongwa na kugandamizwa na gari aina ya TATA yenye namba za usajili T496 CST lililokuwa likitokea eneo la Rushungi kuelekea Lindi mjini baada ya kushindwa kufunga breki wakati likitaka kulipita roli lililokuwa limeegeshwa mbele yake kwa matengenezo.
Mama huyo ni kati ya wahusika wa roli lililoegeshwa kando ya barabara katika eneo la Mtubwaruma kata ya Mchinga wilayani Lindi, ambapo wakiwa katika eneo la tukio, walijikuta wakisombwa na basi hilo ambalo dereva wake alishindwa kulimudu likiwa katika mwendo na kupoteza uelekeo kabla ya kusababisha ajali hiyo, kama wanavyosimulia mashuhuda.
Polisi Mkoani Lindi wamethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo uchunguzi wa chanzo unafuatiliwa.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni
TAFADHARI !!
- Tumia Lugha Nzuri Kutoa Maoni
Usitumie kauli za Karaha AU Zenye Kukela :
C.E.O
Gneous OG