TAARIFA MPYA
HOMA YA MAPAFU YA MBUZI & JINSI UNAVYOSABABISHWA
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Homa ya mapafu ya mbuzi (HMM) ni ugonjwa hatari wa mbuzi unaosababishwa na Mycoplasma capricolum subspecies capripneumoniae (Mccp). Ugonjwa huu unajidhihirisha kwa dalili zifuatazo; kupumua kwa shida, homa kali (nyuzi 41 - 43 za sentigredi), kukohoa, kutiririsha mafua, usambaaji wa haraka na vifo vingi kwa mbuzi wa umri wowote na jinsia zote pamoja na kutupa mimba kwa mbuzi wenye mimba.
HMM ilitambuliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1873 huko Algeria na Bwana Thomas aliyejulikana kwa jina la kienyeji huko Algeria kama "bou frida" kwa sababu kati ya mbuzi wengi walipata ugonjwa ni pafu moja tu lililo athirika. Hata hivyo usambaaji wake kwa njia ya mgusano haukuweza kugunduliwa kwa sababu ugonjwa ulikuwa umesambaa maeneo mengi na kwa wanyama wengi.
Ilikuwa ni mwaka 1881 ulipotambuliwa kuwa ugonjwa wa homa ya mapafu ya mbuzi ni wa kuambukizana toka mbuzi moja kwenda mwingine pale mlipuko mkubwa ulipotokea Afrika Kusini na kusadikiwa kuwa uliletwa na mbuzi waliotoka Uturuki.
Kisababishi cha ugonjwa huu (Mccp) kiligunduliwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 1976 na MacOwan na Minette. Homa ya mapafu ya mbuzi imekwisha ripotiwa takribani katika nchi 40 za Ulaya Mashariki, Afrika, Asia na Mashariki ya Kati. Ugonjwa huu ulitghibitishwa kuwepo Tanzania mnamo mwaka 1998 na tangu hapo ulionekana kusambaa maeneo mbalimbali ya nchi huku jitihada kiduchu ziwekwa kuhusiana na kupambana na ugonjwa huu. Kwa Tanzania ugonjwa huu umeripotiwa.
katika maeneo ya Arusha, Morogoro, Kilimanjaro, Dar es Salaam, Pwani, Tanga,
Mtwara lakini pia kuna maeneo mengine mengi ambayo dalili kwa mbuzi zimehisiwa
kuwa ni za huu ugonjwa. Tatizo ni ugumu wa kuthibitisha ugonjwa huu hasa kwa njia
ya kuotesha wadudu lakini uwepo wa technolojia mpya kama PCR utawezesha
kuutambua ugonjwa huu kwa haraka zaidi.
Wanyama wanaopata HMM
Mbuzi ndio wanyama wa kwanza kupata ugonjwa huu na kondoo wanaweza
kuupata pia hasa wakiwa wanaishi na mbuzi.
Usambaaji wa HMM
Ugonjwa huu huenea haraka sana toka mnyama mmoja kwenda kwa mwingine kwa
njia ya kugusana. Wadudu wa ugonjwa huwa kwenye maji maji ya mfumo wa
upumuaji/hewa.
Dalili za HMM
Ugonjwa huanza kuonyesha dalili kuanzia siku ya 2 hadi ya 28 tangu maambukizi
yatokee na wastani ni siku 10. Afya ya mbuzi huanza kudhoofu na mwisho
kupelekea kifo ndani ya siku saba tangu kuanza kwa ugonjwa. Dalili za ugonjwa huu
ni kama ifuatavyo;
Mbuzi walioathirika na HMM wanaweza kufa ndani ya siku 1 hadi 3 bila kuonyesha dalili au wakiwa na dalili chache sana zisizoweza utambulisha ugonjwa.
Dalili za mwanzo ni homa kali (nyuzi joto 41-43), kuchoka/kudhoofika, mwenyeusingizi, na kukosa hamu ya kula, ikifuatiwa na kukohoa (mara kwa mara kwa nguvu kikohozi kizito) na kupumua kwa shida ndani ya siku 2 hadi 3.
Katika hatua za mwisho mbuzi hushindwa kutembea au husimama huku miguu yake ya mbele akiwa ameipanua na shingo yake imenyooka na kukakamaa.
Mate yanaweza kuwa yanatoka mfululizo mdomoni na mbuzi anaweza kuwa anakoroma au kulia kwa maumivu makali.
Mwishoni mapovu puani na mate mdomoni yanaweza kuonekana
Mbuzi wenye mimba inaweza kutoka
Wanyama wenye ugonjwa hufikia aslimia 100 (wote huwa wagonjwa)
Vifo hufikia kati ya asilimia 60 hadi 100
Mbuzi walio athirika sana wanaweza kufa ndani ya siku 7 hadi 10 tangu waonyeshe dalili
Kuna baadhi ya mbuzi wanaoweza luendelea kukohoa kwa mudaq mrefu huku
wakitirisha makamasi na kuendelea kusambaza ugonjwa kwa muda mrefu.
Mbuzi amekonda na kuwa mpole mwenye shingo ya kukakamaa
Akichinjwa: Mapafu pekee huwa yame athirika, na ni upande mmoja tu huwa ume
athirika. Maji yanayozunguka mapafu huwa na rangi ya majani makavu. Viuvimbe
vidogo vya rangi ya njano huonekana kwenye mapafu na matezi yaliyo karibu ya
mapafu huwa yamevimba. Kwa mbuzi wanaokaa kwa muda mrefu, mapafu yao
huwa yameshikamana na kuta za mbavu pamoja na uvimbe kwenye mapafu
(majipu) wenye kapsuli imara.
Mbuzi amechinjwa na mapafu yake yakiwa na utando wa rangi ya njano au kijani
kikavu huku mapafu yakiwa yameshikamana na mbavu
Mapafu magumu yenye viuvimbe yaliyojaa damu.
Mbuzi aliyekaa sana na ugonjwa mapafu yake hubadilika rangi na kuwa ya kijivu na
yakiwa yamegandamana na mbavu
Magonjwa yanayofanana na HMM
Sotoka ya Mbuzi (Peste des petits ruminants, PPR)- Huu kondoo pia hupata sawa na mbuzi kwa usawa.
Pasteurellosis- Huu hushambulia mapafu yote wakati HMM ni upnde mmoja tu
MAKEPS (Mastitis, arthritis, keratitis, pneumonia na septicaemia syndrome) - Viungo vingine nje ya mapafu huathirika.
Utambuzi wa HMM
Kwa mfugaji dalili zilizotajwa hapo juu zitautambulisha ugongwa pamoja na matokea baada ya kumchinja na jinsi ugonjwa unavyosambaa kwa mbuzi wengi.
Maabara kuotesha wadudu na kutambua kwa njia za kikemikali, ELISA na PCR
Kukinga na Kupambana na HMM
Kuepuka kuingiza mbuzi wenye ugonjwa au toka nchi zenye ugonjwa.
Chanjo pia ikitumika kwa utaratibu mzuri kuchanja mbuzi wote itasaidia kuondoa ugonjwa, baadhi ya nchi zimefanikiwa
Kama kuna mlipuko, mbuzi wazuiwe kutembea ovyo au kuchangamana na wale wenye ugonjwa, kuchinja mbuzi wote walo athirika na kumwagia dawa (Sodium hypochlorite) sehemu waliyokuwa wanalala
Unapo dalili za ugonjwa huu muarifu mtaalamu wa mifugo mapema iwezekanvyo ili tatizo lipewe ufumbuzi
Chupa yenye dawa ya kunyuzia banda la mbuzi kuuwa wadudu wa ugonjwa
-Matibabu kwa kutumia dawa za antibiotics aina ya tylosin (kwa kuchoma 10 mg/kgkwa siku tatu mfululizo) imekuwa ikitumika na inaonekana kufaa katika hatua zamwanzo wa ugonjwa. Ukichelewa mbuzi huonekana kama wamepona lakinihuendelea kusambaza ugonjwa kwa mbuzi wengine. Lakini pia Oxytetracycline(OTC) katika dose ya 15 mg kwa kila kg ya uzito wa mbuzi (15mg/kg), Erythromycinna streptomycin zinaweza kutumika mapema ugunduliwapo ugonjwa.
Kwa huduma Tupigie
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni
TAFADHARI !!
- Tumia Lugha Nzuri Kutoa Maoni
Usitumie kauli za Karaha AU Zenye Kukela :
C.E.O
Gneous OG