Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Desemba 17, 2017

TAARIFA MPYA

Madhara ya Chai na Kahawa Kiafya

Picha
CAFFEINA/KAFEINA. Kafeina ni nini?: 1. Kafeina ni madawa ya kulevya kundi la ‘Stimulants drugs’. Utashangaa. Habari ndiyo hiyo. Hii ndiyo sababu kwa mtu aliyezoea kunywa chai hii kila siku au kahawa, siku asipokunywa kichwa humuuma, ni kwa sababu amekuwa mtegemezi au teja wa kafeina. Kafeina ni kiungo mhimu karibu katika soda zote zenye rangi nyeusi; Coca-cola, Pepsi, Sayona nyeusi, Azam cola na kadharika. Kafeina huongezwa pia katika Red bull, Malta na katika baadhi ya dawa za kupunguza maumivu mwilini. Kwahiyo Kafeina ambayo hupatikana katika chai na kahawa ni aina mojawapo ya madawa ya kulevya. 2. Kafeina ni kikojoshi (diuretics). Kafeina ni dawa ya kukufanya ukojowe. Ukinywa kikombe kimoja cha kinywaji chenye kafeina yaani chai au kahawa, basi muda si mrefu utaenda kukojoa vikombe viwili. Kwa sababu kafeina ni taka isiyotakiwa mwilini, mwili utafanya kila uwezalo ikibidi ujikamuwe wenyewe kupata maji ya ziada kuweza kuitoa kafeina hii uliyoinywa kwa kisingizio ch...

Faham Namna ya kuishi na Mpenzi anaekupendea Hela (Pesa)

Picha
HAPA   tunazungumza kuhusu mapenzi kama kawaida yetu . Leo nimekuja na mada ambayo naamini itawagusa wengi . Marafiki zangu , kusaidia katika mapenzi ni jambo zuri tena lenye mantiki sana. Suala la kusaidiana si la upande mmoja . Linaweza kuwa kwa wote , kwa mwanaume au mwanamke . Ni kati ya nguzo muhimu katika mapenzi , lakini kwa bahati mbaya kuna wale ambao   wamekuwa na tabia ya kupenda sana fedha! Unajua wenzi wanajuana kulingana na wanavyoishi, hivyo ni rahisi sana kumgundua mwenzako kama anapenda sana fedha au ni kweli ana tatizo linalohitaji msaada wako. Hii ni kasoro, lakini haimaanishi kwamba ndiyo sababu ya kuachana. Katika mada hii ipo dawa ya namna ya kudumu katika mapenzi motomoto na mwenzi wa aina hii. Imekuwa ni kawaida kumsikia msichana akitamba mbele ya wasichana wenzake kwa kusema: “Mimi nina kibuzi changu bwana kila ninachotaka kinanipa, kinajua kisiponipa nakitosa tu, yaani nakichuna kama sina akili nzuri....

AZAM YAZIDI KUSONGA MBELE

TIMU ya Azam FC , imeanza vema michuano ya Azam Sports Federation Cup ( ASFC ) baada kuipiga Area C United mabao 4-0, mchezo uliomalizika usiku huu kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi , Dar es Salaam. Azam FC ilionyesha kuwa imedhamiria kuibuka na ushindi katika mchezo huo baada ya kufanya shambulizi kali dakika ya pili tu kufuatia Enock Atta kuwazidi ujanja mabeki wa Area C na kupiga mpira mzuri wa faulo uliomkuta Paul Peter, aliyepiga kichwa kilichogonga mwamba wa pembeni kabla ya mabeki kuokoa hatari hiyo. Azam FC kwa ushindi huo mnono, ni kama imetoa zawadi ya Sikukuu ya Krismasi kwa mashabiki wake kutokana na mchezo huo kuwa wa mwisho kwa timu hiyo kabla ya maadhimisho ya sikukuu hiyo kufanyika keshokutwa Jumatatu na Jumanne. Alikuwa ni kiungo Salmin Hoza, aliyeanza kufungua mlango wa mabao kwa Azam FC dakika ya 17 baada ya kupiga shuti kali nje kidogo ya eneo la 18 akimalizia mpira wa faulo aliotengewa na winga Enock Atta Agyei, ambay...

Sahau kuhusu matokeo lakini haya unapaswa kuyajua baada ya El Clasico ya leo

Picha
Lioneil Mesai alifunga bao lililomfanya kufikisha mabao 25 katika El Clasico na hilo likiwa bao lake la 50 mwaka huu, Messi anakuwa amefunga mabao 50 kwa miaka 6 kuanzia 2010 akiwa ameacha 2013 tu. Mchezo huu uliisha kwa sare ya bila kufungana katika kipindi cha kwanza na hii ikiwa mara ya kwanza kwa Barca kushindwa kufunga bao la katika kipindi cha kwanza Santiago Bernabeu tangu April 2011 katika La Liga. Goli la kwanza la Barcelona lilifungwa na Luis Suarez likiwa ni bao lake la 5 katika El Clasico 7 alizocheza na huku Real Madrid wakishindwa kuweka clean sheet katika michezo ya El Clasico 7 iliyopita. Lioneil Messi alimpoteza Cristiano Ronaldo hii leo kwani ukiachana na bao alilofunga lakini alikamilisha pasi 50/57,akitengeneza chance 9 na mashuti 3 on target, huku CR7 akikamilisha pasi 22/27,akitengeneza chance 1 na shuti 1 on target. Bao la 3 la Barcelona lilifungwa na Alex Vidal dakika ya mwisho na kuifanya Barcelona kwa mara ya kwanza katika historia kushinda michezo 3 mful...

Waziri wa Ulinzi Awatembelea Wanajeshi DRC CONGO

Picha
Ikiwa zimepita siku 16 tangu kuuawa kwa askari 14 wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) waliokuwa kwenye  oparesheni ya ulinzi wa amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Waziri wa Ulinzi wa Tanzania Husssein Mwinyi  amewatembelea wanajeshi wa Tanzania waliopo nchini humo. Mwinyi alifika nchini humo December 22, 2017 ambapo  alipowatembelea Wanajeshi wa Tanzania wanaoshiriki katika kikosi cha kimataifa cha kulinda amani mashariki ya Congo, na kuwatembelea wanajeshi waliojeruhiwa wakati wa shambulizi la December  7, 2017. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Beni, Mwinyi ametoa wito wa kudumisha ushirikiano kati ya pande zote zinazoshiriki katika kuleta amani Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). Wanajeshi 14 wa Tanzania wa kikosi maalum cha nchi za Kusini mwa Afrika SADC waliuawa na wengine 44 kujeruhiwa wakati wa majibizano ya risasi na waasi wasiojulikana katika kambi yao huko Semulik, karibu na mji wa Beni.

Acacia yaendelea kuitesa Serikali

Picha
Wakati Serikali ikipambana kuhakikisha Wananchi wake wanapata ajira, Kampuni ya Uchimbaji Madini ya ACACIA imetangaza kupunguza wafanyakazi wake zaidi ya 3,000. Hatua hiyo imesababishwa na gharama za uendeshaji kuwa kubwa kutokana na hali ya ukata kuikumba kampuni hiyo. Aidha hatua hiyo imepelekea kupungua kwa shughuli za uzalishaji katika migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi iliyopo wilayani Kahama, Mkoani Shinyanga. Tanzania na Barrick Gold Corporation inayomiliki migodi hiyo kwa ubia na ACACIA zilifikia makubaliano tarehe 19 Oktoba, 2017 na kutiliana saini mkataba wa kutekeleza mwelekeo mpya wa namna kampuni hiyo itakavyoendesha biashara ya madini ya dhahabu yanayochimbwa katika migodi yake hapa nchini.

Lwandamila Aendelea kubaki Zambia

Picha
Kocha mkuu wa mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania bara klabu yaYanga , Mzambia George Lwandamina amepata msiba baada ya kufiwa na mtoto wake wa kiume . Taarifa ya Yanga imeeleza kuwa mtoto huyo aitwaye Mofya Lwandamina amefariki jana jioni huko nyumbani kwao Zambia. “ Kwa wana Yanga na wadau wote wa soka , kocha wetu George Lwandamina amepata msiba , amefiwa na mtoto wake wa kiume jana huko Zambia”, imeeleza taarifa ya klabu . Kocha George Lwandamina ataendelea kuwa kwao Lusaka kwa muda mrefu , ikumbukwe aliondoka Dar es Salaam wiki iliyopita kwenda nyumbani kwa ajili ya kuhudhuria mahafali ya mwanawe wa kike , Nasanta Lwandamina aliyehitimu Stashahada ya Afya ya Jamii katika Chuo Kikuu cha NRDC . Yanga SC kesho watakuwa kwenye Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam kumenyana na   Reha FC katika hatua ya 64 Bora ya kombe la shirikisho ( ASFC ).

Huyu Ndie Mwanamke Tajiri Zaidi Duniani

Picha
Baada ya Mfaransa Liliane Bettencourt , 94, kufariki mwezi uliopita , ambaye alikuwa mmiliki wa maduka ya bidhaa za urembo L’Oreal , ambaye ndiye aliyekuwa mwanamke tajiri zaidi duniani akiwa na utajiri wa Dola za Marekani bilioni 39.5, sawa na takriban Tshs trilioni 94, mikoba yake imepata mrithi . Mikoba hiyo imechukuliwa na Alice Walton, ambaye ana mali ya jumla ya Dola za Marekani bilioni 33.8. Kwa jumla, alishikilia nambari 17 katika orodha ya mabilionea wa Forbes waliotangazwa mapema mwaka huu. Hadi kufikia mwezi November mwaka huu Alice Walton ametajwa kuwa na utajiri wa Dola bilioni 45.9 sawa na Tsh za Tanzania trilioni 108. Watson ambaye ni binti pekee wa mwanzilishi wa maduka ya Wal-Mart Sam Walton, ndiye mwanamke tajiri zaidi Marekani na utajiri wake unatokana na hisa zake katika Wal-Mart pamoja na malipo ya mgawo wa faida.

HUYU NDIE MAMA ALIEJIFUNGUA WATOTO WA NNE

Picha
MWANAMKE mmoja mkazi wa Mkoa wa Morogoro, Asha Mashaka amejifungua watoto mapacha wanne katika Wodi ya Wazazi ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo jana Ijumaa, Desemba 22, 2017. Bi. Asha amejifungua kwa Opareshini na sasa yeye pamoja na watoto wake hao wanaendela vizuri hospitalini hapo.

Kocha Mkuu Simba Atimuliwa ni baada ya mkataba wake Kuvunjwa

Picha
Klabu ya Simba na kocha wake mkuu Joseph Omog, kwa pamoja wameamua kuvunja mkataba baina yao kwa makubaliano maalum yanayozingatia maslahi ya pande zote mbili. Taarifa hii inakuja ikiwa ni chini ya saa 24 tangu klabu hiyo ambayo walikuwa mabingwa watetezi wa kombe la shirikisho kutupwa nje ya michuano hiyo na timu ya Warrios kwenye mchezo uliochezwa jana jioni na kufungwa mabao 4-3 kupitia mikwaju ya panalti. Simba kupitia taarifa yake imeeleza kuwa, inamshukuru kocha Omog na inamtakia kila la kheri kwenye maisha yake nje ya Simba. Pia klabu hiyo imesema kwasasa majukumu yote ya ufundi yatakuwa chini ya kocha msaidizi Masoud Djuma na timu itaendelea na mazoezi siku ya kesho kisha kupumzika siku ya Jumatatu kwaajili ya sikukuu ya Krismas na itaingia kambini Jumanne. Simba itasafiri kwenda Mtwara wiki ijayo ambapo itacheza na timu ya Ndanda kwenye mchezo wa ligi kuu raundi ya 12 siku ya jumamosi Disemba 30. Simba inaongoza ligi ikiwa na  alama 23 baada ya michezo 11.

Haji Manara; kitendo cha Klabu yangu kufungwa kwa penanti ni aibu ya mwaka

Picha
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Klabu ya Simba SC, Haji Manara amefunguka na kusema kitendo cha klabu yake ya Simba jana kufungwa kwa njia ya penati na kuondolewa kwenye michuano ya Azam Sports Federation Cup ni aibu ya mwaka. Haji Manara alisema hayo jana baada ya waliokuwa mabingwa watetezi wa (Azam Sports Federation Cup) Simba kupigwa na Green Warriors na kuondolewa katika michuano hiyo kwa penati 4-3 "Shame!! Aibu!!!Fedheha!!! Haivumiliki!!!Tumewakera fans wetu zaidi ya twenty millions... nimeumia kuliko siku zote toka nimeanza kazi Simba..Aibu ya mwaka" aliandika Haji Manara

Kocha Mkuu Simba Atimuliwa ni baada ya mkataba wake Kuvunjwa

Picha
Klabu ya Simba na kocha wake mkuu Joseph Omog, kwa pamoja wameamua kuvunja mkataba baina yao kwa makubaliano maalum yanayozingatia maslahi ya pande zote mbili. Taarifa hii inakuja ikiwa ni chini ya saa 24 tangu klabu hiyo ambayo walikuwa mabingwa watetezi wa kombe la shirikisho kutupwa nje ya michuano hiyo na timu ya Warrios kwenye mchezo uliochezwa jana jioni na kufungwa mabao 4-3 kupitia mikwaju ya panalti. Simba kupitia taarifa yake imeeleza kuwa, inamshukuru kocha Omog na inamtakia kila la kheri kwenye maisha yake nje ya Simba. Pia klabu hiyo imesema kwasasa majukumu yote ya ufundi yatakuwa chini ya kocha msaidizi Masoud Djuma na timu itaendelea na mazoezi siku ya kesho kisha kupumzika siku ya Jumatatu kwaajili ya sikukuu ya Krismas na itaingia kambini Jumanne. Simba itasafiri kwenda Mtwara wiki ijayo ambapo itacheza na timu ya Ndanda kwenye mchezo wa ligi kuu raundi ya 12 siku ya jumamosi Disemba 30. Simba inaongoza ligi ikiwa na  alama 23 baada ya michezo 11.

Mwanajeshi Mwingine JWTZ afariki Dunia Nchini CONGO DRC

Picha
Picha : Na maktaba . ASKARI wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ ) aliyekuwa katika Kikosi cha Umoja wa Mataifa cha Kulinda Amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) amefariki dunia nchini Uganda wakati akipatiwa matibabu . Askari huyo ni miongoni mwa askari 44 wa Tanzania waliojeruhiwa katika shambulio lililofanywa Desemba 7 mwaka huu na waasi wa The Allied Democratic Forces ( ADF ) katika kambi ya walinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa ( MONUSCO ), na kusababisha vifo vya wanajeshi 14 wa Tanzania na watano wa DRC. Msemaji wa Katibu wa Umoja wa Mataifa , Stephane Dujarric , alitangaza taarifa hiyo ya kusikitisha katika Makao Makuu wa UN, Mjini New York jana Desemba 22, 2017 usiku . Katika taarifa iliyotolewa na MONUSCO leo , imeeleza kwamba mwanajeshi wa 15 wa Tanzania amefariki dunia akipatiwa matibabu mjini Kampala. Umoja wa Mataifa umetuma salamu za pole kwa wan...

TUMIA shubiri Mwitu kutibu Magonjwa ya Kuku

Picha
Kuku ni moja ya miradi inayofanywa kwa wingi na watu wa kada mbalimbali , wakiwamo wakulima na wafugaji , na wanaofanya shughuli nyinginezo . Moja ya changamoto ambazo zimekuwa zikiwakabili na kuzungumziwa mara kwa mara ni magonjwa yanayoshambulia kuku , bila wafugaji kufahamu ni nini cha kufanya . Kumekuwepo na njia mbalimbali za kutibu kuku , zikiwemo za asili na zisizokuwa za asili. Moja wapo ya tiba rahisi ya asili kwa kuku ni kwa kutumia shubiri mwitu maarufu kama Aloe Vera. Mmea ambao umekuwa ukisifika kwa kutibu magonjwa mbalimbali kwa binadamu, wanyama na ndege. Shubiri mwitu (Aloe) imekuwa ikitumika kwa kutibu magonjwa mbalimbali ya binadamu na mifugo. Mmea huu unatumika sasa kutengeneza sabuni, dawa za binadamu na wanyama na mambo mengine mengi. Kwa sababu ya madawa mengi ya kiwandani kushindwa kutibu baadhi ya magonjwa kwa sababu wadudu wametengeza ukinzani, ipo haja kubwa ya kuweka mkazo kwenye madawa ya asili yatokanayo na mimea....

Vigezo Ambavyo Hutumiwa na Wanawake Kupenda Hushangaza Mno !

Picha
Watu wengu hujisikia vizuri wanapowavutia wenzao wa jinsia nyingine. Je, unafikiri ni kitu gani kinachomfanya mwanamke aonekane wa kuvutia? Kuna vitu vingi vinavyojulikana vizuri zaidi kwa upande wa mwanamke kama vile; mwili mzuri, sauti yenye mvuto, nywele, mikono mizuri na mengineyo mengi. Lakini, kuna vingine ambavyo siyo vya kawaida vinavyohusu mwanaume kumvutia mwanamke. Je, ni vitu au mambo gani ya kipekee ambayo, humfanya mwanamke aguswe na mwanaume fulani na huku mwanamke mwingine akishangaa ni kwa nini mwanamke mwenzake ameguswa sana na huyo jamaa? Inawezekana yapo mengi ambayo, huyajui. Kwa mfano, mwanamke anaweza akavutiwa na jina la kwanza au la ukoo la mwananume fulani. Hapa mwanamke hufikiri kwamba, huyo mwenye hilo jina hawezi kuwa mtu wa kawaida, na kila kitu anachofanya ni lazima kiwe cha ajabu. Labda ni kutokana na jina hilo kuwa ni la kigeni au anatoka kwenye ukoo ambao ni bora au wa kipekee au anafikiri labda huyo mwanaume atamwezesha kile ambacho, mara nyingi a...

Namna ya kuishi na HIV ' upungufu,wa Kinga Mwilini

Picha
Tarehe 1 desemba kila mwaka, ni siku ya ukimwi duniani.Ukimwi na magonjwa mengine makubwa yamepewa siku rasmi kila mwaka ili kuikumbusha jamii juu ya mapambano dhidi ya magonjwa hayo. Katika siku hizo pia hutolewa matokeo ya tafiti mbalimbali zinazohusu magonjwa husika. Juzi tumeambiwa kuwa kiwango cha maambukizi ya virusi vya ukimwi kimeshuka kutoka 5.7% hadi 5.1%. Ndio kusema katika kundi la watanzania ishirini, mmoja ameambukuzwa virusi vya ukimwi. Swali, je! Mtanzania huyo mmoja kati ya ishirini ameelimishwa vya kutosha juu ya njia za kuishi na maambukizi hayo? Namna ya kuishi na maabukizi ya ukimwi. Virusi vya ukimwi vina nguvu za kipekee sana, pamoja na mwili kuwa na kinga yake ya asili ya kupambana na virusi hivyo lakini mara nyingi kinga hiyo hushindwa na kumfanya mwathirika apate anguko la kiafya. Kuna mbinu kadhaa ambazo mwathirika  anaweza kuzitumia ili kuongezea kinga yake nguvu ya kupambana na virusi. Mwathirika afanye nini anapogundua hali yake ? Mara tu baada ya...

Kombe la Shirikisho la Azam Sport Federation Cup Kutimua Vumbi Leo

Picha
Msimu wa tatu wa Azam Sports Federation Cup unazinduliwa rasmi leo Ijumaa katika mchezo wa raundi ya pili kati ya bingwa mtetezi Simba SC dhidi ya Green Warriors. Tangu kuanza kwa mechi za msimu huu hapajawahi kufanyika uzinduzi rasmi kutokana na bingwa mtetezi kutokuanzia katika hatua za awali, na sasa kwa mujibu wa ratiba hafla ya uzinduzi itafanyika leo wakati wa mchezo huo utakaopigwa kwenye dimba la Chamazi Dar es Salaam na kurushwa mbashara kupitia Azam Sports 2.   Tayari mechi za msimu huu zilianza kuchezwa tangu hatua ya awali iliyohusisha mabingwa wa mikoa hadi kufikia hatua hii inayojumuisha timu 64 zikiwemo timu 16 za ligi kuu ya Tanzania bara. Mbali na mchezo huo, mechi nyingine saba za raundi ya pili zitapigwa leo katika viwanja ni kama ifuatavyo:- Stand United vs AFC ya Arusha, Polisi Dar vs Mgambo JKT, Kariakoo vs Transit Camp, Biashara United vs Mawenzi Market, Ruvu Shooting vs Madini FC, Mufindi United vs Pamba, Singida United vs Bodaboda FC. Katik...

Madhara Ya Kuangalia Video za Porno {Ngono} na Namna ya Kujizuia

Picha
Kuangalia video za ngono sio jambo jipya kwa jamii yetu , kimsingi ni watu wachache sana wanaweza kujizuia kujichua au kupiga punyeto baada ya kuangalia video za ngono . Bahati mbaya tabia ya kuangalia video hizi watu wengi huipata wakiwa wadogo sana na usipokua makini tabia hii itakufanya vibaya sana kisaikolojia . Tabia ya kujichua sasa iko wazi kwa jinsia zote yaani wanawake na wanaume japokua imekua ikiathiri zaidi wanaume sababu ya maumbile yao. Japo wengi hufanya kwa siri na kuficha ili wasijulikane na wengine. Vijana wengi wamekuwa wakiangalia video hizo wakiwa wamejificha wenyewe chumbani, na hasa nyakati za usiku. Kuangalia video za ngono kuna madhara mbalimbali ya kiafya na kisaikolojia. Haya hapa ni baadhi ya madhara unayoweza kuyapata kama utaangalia sana video za ngono. Kuishiwa hamu ya tendo la ndoa na nguvu za kiume Kuangalia sana video za ngono hukufanya ushindwe kusisimuliwa na mwanamke au mwanaume wa kawaida, video za ngono...

Boti ya zama ziwa Tanganyika ' Watu 22 Wahofiwa kufa

Picha
Watu 22 wanahofiwa kufa maji katika Ziwa Tanganyika katika ajali ya boti iliyotokea iliotokea leo alfajiri. Imeelezwa miili ya watu wanne imeopolewa na imetambuliwa na ndugu zao huku watu wengine 115 wameokolewa wakiwa hai baada ya boti kugonga mtumbwi. Ofisa wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra) Mkoa wa Kigoma, Amaniel Sekulu amesema ajali hiyo imetokea katika kitongoji cha Lubengela kijijini Msihezi, Kata ya Sunuka wilayani Uvinza. Amesema mtumbwi uitwao Mv Pasaka uligongwa ubavuni na boti ya Atakalo Mola na kupasuka, hivyo kuzama ziwani. Sekulu amesema mtumbwi ulikuwa umebeba abiria 137 waliokuwa wanakwenda kwenye mkutano wa injili katika Kijiji cha Sunuka. Amesema  boti ilikuwa ikitokea Kigoma kwenda Kalya ikiwa imebeba abiria 65. Sekulu amesema  boti na mitumbwi inayobeba abiria hairuhusu kufanya safari usiku. Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Sweetbert Njewike akizungumzia ajali hiyo amesema  wanaendelea kuwatafuta watu ambao h...

Majaliwa Atoa Agizo wizara ya chakula leo

Picha
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza mtambo wa kutengenezea mbegu za pamba ulioko mkoani Mbeya, kuondolewa mara moja na kupelekwa kwenye mikoa inayolima zao hilo huku akihoji sababu za msingi zilizochangia mtambo huo kuwekwa huko. Akizungumza na wadau wa zao hilo  Waziri Mkuu alitoa agizo hilo na kuitaka wizara inayohusika kuchukua hatua mara moja huku akivitaka viwanda vya ndani vyenye uwezo wa kuzalisha mbegu kujitokeza. Amesema haiwezekani mtambo unaotengeneza mbegu za pamba ukawekwa kwenye mkoa ambao haulimi zao hilo na kuhoji kulikuwa na sababu gani ya msingi ya kuwekwa mkoani Mbeya, ndipo aliamua kuagiza kuondolewa na kupelekwa kwenye mikoa inayolima pamba. Hata hivyo Majaliwa  alisema kiwanda cha Quiton ambacho kimewekeza nchini kwa ajili ya  kutengeneza mbegu za pamba aina ya Quiton lakini cha kusikitisha mpaka msimu wa kilimo unafika hakuna mbegu na hii kampuni inamilikiwa na Wazimbabwe na wao wanalima pamba nchini kwao katika hili tutafakari. ‘’T...

JENGO LA TANESCO KUBOMOLEWA KABLA YA JANUARY

Picha
Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani ametoa siku kumi kwa jengo la  Tanesco lililopo Ubungo libomolewe ili kupisha ujenzi wa barabara ya Morogoro. Waziri huyo pia  amewataka  watumishi wa Tanesco wanaosimamia jengo hilo na wakandarasi waliowekwa kubomoa jengo hilo wasisafiri wala kusherekea Sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya bali washughulikie jengo hilo kuvunjwa. “Nataka kuanzia leo Desemba 22 ndani ya siku sita jengo hili lote libomoke  na kwasababu ni majengo mawili ndani ya siku kumi majengo yote mawili yawe yamebomoka kama mnaona vigumu kubomoa jengo lenu waambieni TBL ”amesema Amesema  hadi kufikia mwisho wa mwezi huu jengo hilo lote liwe limeanguka chini na hakuna cha sikukuu wala Krisimasi  kwenye kubomoa jengo hili na ujenzi wa barabara kama Tanesco wanaaza waanze tusiwakwamishe”amesema. Amesema wananchi wameshabomoa majengo yao kwanini Tanesco bado wanasuasua na kudai  Januari mosi ataenda  tena kukagua kuona kama a...

Arsenal kuizuia Liver pool kuweka Rekodi Leo

Picha
Tangia mwezi May mwaka 1998 klabu ya Arsenal haijawahi kupoteza mara nne mfululizo mbele ya Liverpool lakini hadi leo hii tayari wameshapoteza mara 3 mfululizo na hii ina maana wakipigwa leo watakuwa wamepoteza ya nne . Liverpool wanawafuata Arsenal huku washika mitutu hao wakionekana kukaza sana katika uwanja wao wa nyumbani kwani katika michezo 14 waliyocheza Emirates wameshinda 13 huku wakipoteza mmoja tu mwezi uliopita zidi ya Manchester United. Chini ya kocha Jurgen Klopp Liverpool wamefanikiwa kuifunga Arsenal walau mabao 3 au zaidi katika mechi nne walizokutana na Liverpool sasa wanakuwa wamewafunga Arsenal jumla ya mabao 14. Uwezo wa Liverpool katika viwanja vya ugenini unaonekana kuwapa kiburi mashabiki wengi wa klabu hiyo kwani ndio klabu pekee katika historia kuweza kushinda michezo 4 mfululizo kwa wastani wa kuanzia mabao 3. Endapo hii leo Liverpool watafanikiwa kumaliza mchezo bila nyavu yao kuguswa baasi itakuwa mara ya kwanza ...

LIJUA KALI APATA DHAMANA MAHAKAMANI MOROGORO

Picha
Mbunge wa jimbo la Kilombero kupitia Peter Lijualikali ameachiwa kwa dhamana baada ya kukamatwa na maofisa wa polisi akiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro. Kabla ya kuachiwa kwa dhamana Lijualikali ambaye anakabiliwa na kesi iliyoko mahakamani ya ushawishi na kuchoma moto ofisi ya serikali ya kijiji cha Sofi Malinyi amehojiwa kwa saa kadhaa katika kituo cha polisi mkoani Morogoro. Akieleza leo Desemba 22  sababu za kukamatwa kwa mbunge huyo Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Ulrich Matei amesema anatuhumiwa kwa kosa la kimtandao ambalo ni kusambaza picha za mtu anayedai kuwa anataka kumuua jambo ambalo ni kosa kisheria. Kamanda Matei amesema kuwa baada ya kuhojiwa kwa kina wameamua kumuachia kwa dhamana hata hivyo uchunguzi zaidi unaendelea kuhusiana na tuhuma hizo na upo uwezekano wa kumfikisha mahakamani. Lijualikali, Suzan Kiwanga ambaye ni mbunge wa Kilombero na wenzao 55 jana (Desemba 21) walifika mahakamani hapo ambapo wanashtakiwa kwa makosa nane likiwem...

Uganda na Tanzania zatiliana Saini

Picha
Tanzania kupitia kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo anayeshughulikia sekta ya Mifugo, Dkt. Mary Mashingo na Uganda kupitia kwa Balozi wake nchini Richard Tumusiime  Kabonero leo zimesaini makubaliano ya kuboresha sekta ya mifugo. Makubaliano hayo yamesainiwa mjini Bukoba na baada ya kutia saini Dkt. Mary  Mashingo amesisitiza kwamba ushirikiano wa kitaalam katika kuratibu, kufuatilia hali ya mifugo na kufanya tathmini ya kila wakati utaleta mafanikio makubwa  baina ya nchi ya Tanzania na Uganda. “Magonjwa ya mlipuko kwa  wanyama  ni suala mtambuka duniani kote, hivyo ni muhimu kulishughulikia  kwa pamoja ili kuwa na tija, pia tumeamua kwa pamoja kuanzia sasa kudhibiti tatizo la utoroshaji wa mifugo kwenye mipaka ya nchi zetu na hatua kali  zitachukuliwa  ili kutoa fundisho kwa yeyote atakayefanya makosa”, amesema Dkt. Mashingo. Naye Balozi Kabonero amesema magonjwa ya mlipuko kwa wanyama hayana mipaka hivyo makubaliano yaliyofanyik...

BAS LAUWA SAFARINI

Picha
Mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Zawadi Seif Mlawa mwenye umri wa miaka 37 mkazi wa Morogoro, amefariki dunia baada ya kugongwa na kugandamizwa na gari aina ya TATA yenye namba za usajili T496 CST lililokuwa likitokea eneo la Rushungi kuelekea Lindi mjini baada ya kushindwa kufunga breki wakati likitaka kulipita roli lililokuwa limeegeshwa mbele yake kwa matengenezo. Mama huyo ni kati ya wahusika wa roli lililoegeshwa kando ya barabara katika eneo la Mtubwaruma kata ya Mchinga wilayani Lindi, ambapo wakiwa katika eneo la tukio, walijikuta wakisombwa na basi hilo ambalo dereva wake alishindwa kulimudu likiwa katika mwendo na kupoteza uelekeo kabla ya kusababisha ajali hiyo, kama wanavyosimulia mashuhuda. Polisi Mkoani Lindi wamethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo uchunguzi wa chanzo unafuatiliwa.

Mkurugenzi kuchunguzwa baada ya utendaji Mbovu wa kazi

Picha
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Morogoro Vijijini ,  Sudi Mussa Mpiri atafanyiwa uchunguzi kutokana na utendaji wake kutoridhisha ikiwemo kushindwa kutekeleza miradi ya maendeleo . Agizo hilo la kufanyiwa uchunguzi limetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo , ameagiza kufanyika uchunguzi wa haraka kwa mkurugenzi huyo baada ya kutoridhishwa na miradi ya maendeleo aliyoitembelea. Mussa Mpiri anadaiwa kushindwa kutoa ufafanuzi wa fedha zilizopokelewa na Halmashauri hiyo kiasi cha sh.milioni 1.6 ya mapato ya ndani. Imeelezwa pia zaidi ya asilimia 90 ya matumizi ya pesa hizo hayafahamiki hivyo kutia shaka juu ya utendaji wake. Kufuatia hatua hiyo Waziri Jafo, ameagiza kitengo cha uchunguzi na ufuatiliaji kilichopo Ofisi ya Rais TAMISEMI kufika haraka ndani ya Halmashauri hiyo kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini mwenendo wa Mkurugenzi huyo. Jafo amewataka madiwani wa Halmashauri hiyo kufahamu kwamba wao wapo kwa...

Mkurugenzi kuchunguzwa baada ya utendaji Mbovu wa kazi

Picha
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Morogoro Vijijini ,  Sudi Mussa Mpiri atafanyiwa uchunguzi kutokana na utendaji wake kutoridhisha ikiwemo kushindwa kutekeleza miradi ya maendeleo . Agizo hilo la kufanyiwa uchunguzi limetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo , ameagiza kufanyika uchunguzi wa haraka kwa mkurugenzi huyo baada ya kutoridhishwa na miradi ya maendeleo aliyoitembelea. Mussa Mpiri anadaiwa kushindwa kutoa ufafanuzi wa fedha zilizopokelewa na Halmashauri hiyo kiasi cha sh.milioni 1.6 ya mapato ya ndani. Imeelezwa pia zaidi ya asilimia 90 ya matumizi ya pesa hizo hayafahamiki hivyo kutia shaka juu ya utendaji wake. Kufuatia hatua hiyo Waziri Jafo, ameagiza kitengo cha uchunguzi na ufuatiliaji kilichopo Ofisi ya Rais TAMISEMI kufika haraka ndani ya Halmashauri hiyo kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini mwenendo wa Mkurugenzi huyo. Jafo amewataka madiwani wa Halmashauri hiyo kufahamu kwamba wao wapo kwa...

Mwanamke anaswa na mzigo wa Bangi

Picha
Tofauti na ilivyoanza kuzoweleka hivi sasa kukamatwa wasafirishaji wa bangi wanaotoka Tarime mkoani Mara kwenda Mwanza , safari hii mwanamke anashikiliwa na polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kukutwa na bangi . Hata hivyo kinachoshangaza ni namna mwanamke huyo alivyokamatwa akiwa na bangi hiyo inayokadiriwa kuwa na uzito wa kati ya kilo 30 na 50 wilayani Ukerewe. Mara nyingi polisi imekuwa ikiwakamata watu wanaojihusisha na biashara hiyo kwenye magari yanayofanya safari zake kati ya Sirari wilayani Tarime na Mwanza. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema mwanamke huyo alikamatwa Desemba 19 katika Kisiwa cha Lyegoba kilichopo Kata ya Irugwa, saa moja jioni. Msangi alisema bangi hiyo ilikuwa kwenye gunia moja, maboksi matatu na misokoto 371 kwa pamoja ikikadiriwa kuwa na kilo kati ya 30 hadi 50. Alisema polisi wanaendelea na upelelezi ikiwamo kumhoji mtuhumiwa na endapo uchunguzi utakamilika watamfikisha mahakamani kujibu tuhu...

Zitto Azungumzia sakata la Airtel

Picha
Dar es Salaam. Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe ameshauri kutazamwa mchakato mzima wa ubinafsishaji kwa kufanya ukaguzi maalumu wa sera ili kutoa mapendekezo ya kurekebisha makosa yaliyofanyika. Amesema katika kufanya hivyo, suala la Airtel linaweza kushughulikiwa na kupata matunda mazuri zaidi. Zitto katika taarifa kwenye mitandao ya kijamii leo Ijumaa Desemba 22,2017 amesema Serikali inaweza kuunda tume kutazama namna ubinafsishaji ulivyofanyika na kuchukua hatua za kisayansi baada ya matokeo ya kazi hiyo. Amesema akiwa kiongozi wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) walifanyia kazi sera ya ubinafsishaji. “Katika kila taarifa yetu ya mwaka tulikuwa na sehemu maalumu iliyoeleza ufuatiliaji wetu wa utekelezaji wa sera ya ubinafsishaji,” amesema. Zitto amesema ubinafsishaji wa iliyokuwa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) ni suala walilolitolea taarifa mara kadhaa bungeni na ya mwisho ilikuwa Januari 2015. “Ni ukweli usio na shaka kuwa kampuni ya Cel...

Wolper azungumzia kurudiana na Hamonize

Picha
Msanii wa Filamu Bongo, Jacqueline Wolper amefunguka taarifa za kurudiana na Harmonize. Kauli hiyo inakuja mara baada ya Wolper kumjibu shabiki mmoja katika mtandao kuwa anaweza kumpata Harmonize kwa wakati wowote. “Kwanini nimejiaminisha?, sasa yule si njiwa wangu kabisa au hamjui Harmonize njiwa wangu,” amesema. Hata hivyo amesema kuwa kauli hiyo aliitoa kutokana mtu huyo alimkera hivyo akaamua kutoa neno la kumuumiza pia.

Wanachama wa UN watupilia mbali Vitisho vya Trump

Picha
New York. Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zimekaidi vitisho vya Serikali ya Marekani na kupiga kura ya ndiyo kuidhinisha azimio linalotupilia mbali tangazo la Rais Donald Trump kuutambua mji wa Jerusalem kama makao makuu ya Israel. Nchi wanachama 128 zilipiga kura ya ndiyo dhidi ya kura tisa zilizopinga , huku nchi 35 zikijiondoa kupiga kura. Baada ya kura, Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Nikki Haley aliyashukuru mataifa 65 yaliyopinga azimio hilo, yaliyojizuia kupiga kura au hayakuwapo wakati wa kupiga kura. Marekani, Togo, Honduras na Guatemala ni mataifa ambayo yalipiga kura kupinga azimio hilo. Mataifa ya Canada, Mexico, Rwanda, Uganda, Poland, Jamhuri ya Czech na Romania hayakupiga kura. Kabla ya kura, Marekani ilitishia kuzuia misaada kwa mataifa yatakayopiga kura kuunga mkono azimio hilo. Haley amesema kura hiyo haitabadilisha kitu katika mipango ya Marekani kuhamishia ubalozi wake mjini Jerusalem kutoka Tel Aviv.

CUF ya Maalim Seif Yaendelea Kung'ara

Picha
Mahakama ya Rufaa Tanzania imekubali maombi ya Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Wananchi (CUF) inayomuunga mkono Katibu Mkuu wa chama hicho,Maalim Seif Sharif Hamad katika shauri Namba 43/01/2017 kuhusu kumkataa Jaji Kihiyo kusikiliza shauri la msingi. Taarifa hiyo ya maamuzi ya mahakama ya Rufaa, imetolewa mapema leo Disemba 22, 2017 kwa vyombo vya habari na Naibu Mkurugenzi wa Habari CUF, Mbarala Maharagande. “Mahakama ya Rufaa imeipa ushindi Maombi ya Bodi ya Wadhamini ya CUF chini ya Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad katika shauri Namba 43/01/2017 (From Civil Application No.23/2017) kuhusu kumkataa Jaji Kihiyo kusikiliza shauri la msingi tajwa hapo juu. “Shauri hili ndilo linalohoji uhalali na mamlaka ya Msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji Francis Mutungi kumrejesha Lipumba katika nafasi ya Uongozi ndani ya CUF baada ya kujiuzulu na kukubaliwa kujiuzulu kwake na Mkutano Mkuu wa Taifa wa CUF uliofanyika katika ukumbi wa Blue Pearl, Ubungo Plaza Tarehe 21 August, 2...

Kauli ya ACT-Wazalendo baada ya Zitto Kabwe Kukutana na Viongozi wa Upinzani

Picha
Baada ya kuenea kwa picha za Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe kuwa na baadhi ya viongozi wengine wa vyama vya upinzani hatimae chama hicho kimeeleza kuwa kiliazimia kuanza kufanya mazungumzo na viongozi wengine wa vyama vya upinzani ili kuunganisha nguvu kwenye mapambano ya demokrasia. Akiongea na Bongo5 leo, Katibu Itikadi na Uenezi wa Chama hicho, Ndugu.Ado Shaibu amesema kuwa ingawa kila Chama kina Itikadi, sera na programu zake, yapo mambo ambayo Chama cha upinzani hakiwezi kufanya peke yake. “Kamati Kuu ya Chama chetu iliazimia kuwa Uongozi wa juu wa Chama uanze mazungumzo na viongozi wengine wa Vyama vya upinzani ili kuunganisha nguvu kwenye mapambano ya demokrasia. Ingawa kila Chama kina Itikadi, sera na programu zake, yapo mambo ambayo Chama cha upinzani hakiwezi kufanya peke yake. Moja ya mambo hayo ni mapambano ya kidemokrasia kwa hiyo, Zitto amekwishafanya mazungumzo na Mbowe na Rungwe na atafanya mazungumzo na viongozi wa Vyama vingine,” amesema Ado. ...

Rugemalila Anataka Kumtaja Mwizi wa Fedha za ESCROW

Picha
Mfanyabiashara James Rugemalila anayekabiliwa na kesi ya utakatishaji fedha ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa anahitaji kuonana na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) ili ampe ushahidi wa nani anayepaswa kukamatwa katika kesi hiyo. December 8, 2017 Rugemarila aliieleza mahakama hiyo kuwa unahitajika ushirikiano baina yake na upande wa mashtaka ili kumbaini mwizi wa Sh.Bil 309 za Serikali. Mbali ya Rugemarila, Mshtakiwa mwingine ni mmiliki wa IPTL Harbinder Singh Sethi ambapo kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi, utakatisha fedha na kuisababishia Serikali hasara ya USD 22, 198,544.60 na Sh.Bil 309. Rugemarila ameyaeleza hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Leornad Swai kudai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, hivyo anaomba ahirisho. Baada ya kueleza hayo, Rugemarila alinyoosha mkono ambapo amesema kuwa anaushukuru upande wa mashtaka ulimchukua gerezani na kumpeleka Upanga kwa mahojiano na kumrudi...

Alie Katwa Maskio kwa kumlawiti Mtoto Atiwa nguvuni na Jeshi La Polisi

Picha
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga  Simon Haule amethibitisha kuwa Jeshi la Polisi Mkoani kwake linamshikilia kijana Msigala Salum (24) kwa tuhuma za kumlawiti mtoto  mwenye umri wa miaka mitatu. Kamanda Haule  amesema Kijana  huyo aliyejulikana kwa jina la Msigala Salum (24) amekatwa masikio yote mawili na wananchi wenye hasira kali baada ya kumlawiti mtoto huyo mwenye umri wa miaka mitatu katika eneo la Majengo Mapya Kata ya Lubaga Manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga. "Tukio hilo limetokea Disemba 20, 2017 majira ya saa tatu asubuhi ambapo kijana huyo anayejishughulisha na shughuli ya kuosha magari mkazi wa Ndala, alimdanganya mtoto huyo wakati akicheza na wenzake nyumbani kwao, kutokana na tukio hilo mtuhumiwa alishambuliwa na wananchi kabla ya Jeshi la polisi kufika eneo la tukio na kumuokoa", amesema Kamanda Haule. Aidha kamanda Haule ameongeza kwa kusema kuwa mara baada ya tukio hilo baba mzazi wa mtoto huyo alimkamata mtuhumiwa na kumkata masikio yote m...

RAIS wa KOREA KASKAZINI APIGA MARUFUKU KUNYWA ' KULEWA SIKU YA KLISMASI

Picha
Kim Jong Un. RAIS Kim Jong Un wa Korea ya Kaskazini amepiga marufuku kuimba, kunywa vileo na kufanya mikusanyiko ya aina yote nchini humo wakati wa Krismasi mwaka huu. Kwa mujibu wa shirika la ujasusi la Korea ya Kusini (NIS), hatua hiyo inakazia amri ya kupiga marufuku sherehe za Krismasi ya mwaka jana (2016) ikilenga kuzuia nguvu za upinzani nchini humo hususan sasa ambapo vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya nchi hiyo vinaonyesha kuiumiza nchi hiyo. “Korea ya Kaskazini imeanzisha mfumo wa jumuia za chama tawala kuripoti matatizo ya kiuchumi ya watu wanayokumbana nayo kila siku, na imepiga marufuku mikusanyiko inayohusiana na unywaji wa vileo, uimbaji na burudani nyingine, na imeimarisha udhibiti wa habari kutoka nje,” lilisema NIS. Fursa za kuitumia sikukuu hiyo kueneza uelewano na furaha zinazidi kufifia katika taifa hilo linalodaiwa kutawaliwa kidikteta na ambalo limepiga marufuku dini zote isipokuwa maadhimisho ya familia iliyoasisi taifa hilo la kikomunisti. Mwak...

DISKO LAPIGWA MARUFUKU DAR

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limepiga marufuku disko toto na ulipuaji wa baruti katika kipindi hiki cha Sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya huku ikitoa onyo kwa watu ambao watakaidi agizo hilo. Kamanda wa Kanda Maalum, Lazaro Mambosasa ametoa onyo hilo katika mkutano wake na wandishi wa habari ambapo pia alielezea mikakati ya Jeshi hilo katika kulinda amani kwenye msimu huu wa sikukuu

WABUNGE WAWILI WACHAGULIWA BILA LIDHAA YAO EALA

Picha
Arusha. Katika hali inayozidi kuleta mkanganyiko kuhusu ushiriki wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki (Eala), wabunge wawili wamechaguliwa wajumbe wa Tume ya bunge bila ya ridhaa yao. Wabunge hao ni Fancy Nkuhi na Mariam Ussi Yahya ambao Jumatano Desemba 20,2017 walichaguliwa wajumbe wa tume licha ya umoja wa wabunge wa Tanzania katika Eala kutaka majina yao yaondolewe. Kila mmoja alipata kura 35 katika uchaguzi uliosusiwa na wabunge wote kutoka Burundi. Habari kutoka ndani ya Bunge zilizothibitishwa na msemaji wa Eala, Bobi Odiko zimesema wabunge wa Tanzania sasa ni wajumbe halali wa Tume licha ya Taifa hili kususia vikao tangu Jumatatu wiki hii. Taarifa kutoka Eala zinasema wabunge hao walichaguliwa kwa kishindo kuwa wajumbe katika kikao kilichofanyika Jumatano ambacho kilihudhuriwa na wabunge watatu tu kutoka Tanzania. Odiko alisema ni kweli umoja wa wabunge wa Tanzania ulishamwandikia barua Katibu wa Bunge la Eala mapema wiki hii kuwa majina ya Nkuhi na Yahya yaondolew...

NA HII NDO SAFU MPYA YA YANGA

Picha
  Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania bara klabu ya Yanga SC imeteua wanachama 28 kwaajili ya kuunda kamati mpya ya mashindano . Taarifa ya klabu hiyo imeeleza kuwa kamati hiyo itakuwa chini ya Mwenyekiti Hussein Nyika , Makamu wake Mustapha Ulungo na Katibu Mkuu Samuel Lukumay . Uteuzi huo umefanyika jana katika kikao cha Kamati ya Utendaji kilichofanyika makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam huku. Yanga inakamata nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 21 baada ya mechi 11, ikizidiwa pointi mbili na vinara Simba na Azam FC. Yanga itasafiri Desemba 31 hadi jijini Mwanza ambapo itakwaana na Mbao FC kwenye uwanja wa CCM Kirumba, ikiwa ni mwendelezo wa mechi za ligi kuu msimu wa 2017/18. Wajumbe wa Kamati hiyo ni kama inavyoonekana hapo chini.

MO AANZA KUIHUDUMIA SIMBA

Picha
Mohammed Dewji ‘Mo’ MFANYABIASHARA maarufu nchini Tanzania, Mohammed Dewji ‘Mo’ ameanza rasmi kazi ya kuihudumia Klabu ya Simba. Mo ameanza kuihudumia klabu hiyo baada ya kupita kwenye mchakato wa kumtafuta muwekezaji wa Klabu ya Simba kwa ofa yake ya shilingi bilioni 20 na kupata hisa kwa asil­imia 50 huku 50 zikibaki kwa wanachama. Hata hivyo, bado kuna majadiliano na serikali ambayo inataka mwekezaji wa klabu asizidi asilimia 49. Awali, mfanyabiashara huyo alikuwa anaihudumia timu hiyo kama mwanachama kabla ya kukabidhiwa na wanachama klabu hiyo na kuwa mwekezaji. Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Ijumaa, kutoka ndani ya timu hiyo, mfanyabiashara huyo ameanza kutoa huduma mbalimbali ikiwemo mshahara, posho na mahitaji mengine. Mtoa taarifa huyo alisema, kambi ya maan­dalizi ya mechi ya hatua ya pili ya Kombe la FA dhidi ya Green Warriors aliwezesha yeye kwa kuiweka timu ya Escape Two Hotel, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam. ...