TAARIFA MPYA
KIJUE KILIMO BORA CHA AMDALASINI
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
AINA
Mchanganyiko; za kienyeji (ndogo) na za kigeni ( kubwa)
HALI YA HEWA NA UDONGO
Mvua nyingi za kutosha 2000mm -2500mm kwa mwaka
Udongo wenye rutuba
Joto kwa wingi
Hewa yenye unyevunyevu
KUSIA MBEGU KWENYE VITALU
Mbegu hupatikana kwenye miti iliyokomaa
Sia mbegu kwenye kitalu zikiwa nusu sentimeta chini ya udongo
Baada ya kuchipua, mbegu huchukua miezi 6 hadi mwaka mmoja kufikia umri wa kupandikiza shambani
Panda miche wakati wa masika
Panda kwa nafasi ya 2m x2m. Nafasi hizi huwezesha miti kutoa machipukizi mengi. Nafasi kubwa hufanya miti kuwa na matawi mengi pia mashina hayanenepi wala kurefuka
UTUNZAJI
Acha machipukizi kwenye shina
Toa matawi kwenye mashina ili kunenepesha mashina
Weka shamba katika hali ya safi
Zuia magonjwa kama.
Vinundu (galls)wanaosababishwa na utitiri na wadudu scales na mealbugs kwa kutumia dawa za sumu kama Selecron, Karate nk.
KUVUNA
Anza kuvuna miaka 3 baada ya kupanda
Mazao ya mdalasini ni maganda ya mashina ya miti
Kata shina la mti,na tenganisha maganda na mti kwa njia ya kumenya
Kuwa mwangalifu ili ganda litoke vizuri bila kupasukapasuka
Seli za nje ya ganda la mdalasini ni chungu hivyo ni vizuri ziondolewe kwa kukaruza kwa kisu
Kausha vizuri siyo kwenye jua kali Mavuno
0.25 kg – 10kg maganda yaliyokaushwa kwa mti mmoja. Kiasi cha mazao hutegemea ukubwa na umri wa mti
Ubora wa mdalasini hushuka kulingana na umri wa mti. Mti wa umri mkubwa hutoa mganda yenye ubora wa chini
MATUMIZI
Mdalasini baada ya kukaushwa ikiwa umesagwa au bila kusagwa hutumika kama:
Kiungo kwenye chakula na vitafunwa kama keki, mandazi,vitumbua
Vikolezo kwenye vinjwaji km. chai, kahawa
Dawa ya tumbo hasa wakati wa kuvimbiwa, kutoa hewa tumboni pia kuongeza hamu ya chakula
Dawa ya ngozi
JINSI YA KUTUMIA
kiungo kwenye chakula
Tumia maganda au saga magada yaliyokauka. Tumia ili kuongeza ladha kwenye vyakula kama pilau, ndizi, mchuzi nk
Kutengenezea kinywaji
Weka vipanda vichache 2-3 (30gm) vya maganda kwenye kikombe ongeza maji yanayochemka, funika kwa dakika 15, ongeza vipande vya limao. Kunywa kila baada ya kula
MANUFAA
Miti hudumu shambani zaidi ya miaka 20. Miti huchipua na kutoa machipukizi mengine kila baada ya kuvuna
Gharama ndogo ya uzalishaji
Mazao yaweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu
Magonjwa na wadudu ni kidogo
Rahisi kuchanganya na mazao mengine
Nguvu kidogo, kipato kikubwa.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni
TAFADHARI !!
- Tumia Lugha Nzuri Kutoa Maoni
Usitumie kauli za Karaha AU Zenye Kukela :
C.E.O
Gneous OG