Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Januari 7, 2018

TAARIFA MPYA

Madhara ya Chai na Kahawa Kiafya

Picha
CAFFEINA/KAFEINA. Kafeina ni nini?: 1. Kafeina ni madawa ya kulevya kundi la ‘Stimulants drugs’. Utashangaa. Habari ndiyo hiyo. Hii ndiyo sababu kwa mtu aliyezoea kunywa chai hii kila siku au kahawa, siku asipokunywa kichwa humuuma, ni kwa sababu amekuwa mtegemezi au teja wa kafeina. Kafeina ni kiungo mhimu karibu katika soda zote zenye rangi nyeusi; Coca-cola, Pepsi, Sayona nyeusi, Azam cola na kadharika. Kafeina huongezwa pia katika Red bull, Malta na katika baadhi ya dawa za kupunguza maumivu mwilini. Kwahiyo Kafeina ambayo hupatikana katika chai na kahawa ni aina mojawapo ya madawa ya kulevya. 2. Kafeina ni kikojoshi (diuretics). Kafeina ni dawa ya kukufanya ukojowe. Ukinywa kikombe kimoja cha kinywaji chenye kafeina yaani chai au kahawa, basi muda si mrefu utaenda kukojoa vikombe viwili. Kwa sababu kafeina ni taka isiyotakiwa mwilini, mwili utafanya kila uwezalo ikibidi ujikamuwe wenyewe kupata maji ya ziada kuweza kuitoa kafeina hii uliyoinywa kwa kisingizio ch...

Guardiola aongeza rekodi nyingine EPL

Picha
Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola ameweka rekodi ya kuwa kocha wa kwanza kutwaa tuzo ya kocha bora wa mwezi mara nne mfululizo kwenye ligi kuu soka nchini England EPL. Kocha huyo raia wa Hispania ametwaa tuzo hiyo katika miezi ya Septemba , Oktoba , Novemba na Disemba hivyo kuweka rekodi hiyo ya pekee . Guardiola amefanikiwa kuweka rekodi hiyo akiwa ameiongoza City katika michezo 60 ya ligi kuu soka nchini England katika msimu mmoja na nusu tangu awe kocha wa timu hiyo . Katika mechi hizo ametwaa tuzo hiyo mara tano . Katika mwezi Disemba Man City imecheza mechi nane na kushinda mechi saba huku ikitoka sare mchezo mmoja dhidi ya Crystal Palace na kufunga mabao 19 katika mechi hizo . Guardiola sasa amemuacha mpinzani wake Jose Mourinho ambaye tangu aanze kufundisha timu za EPL amefundisha mechi 272 na kutwaa tuzo hiyo mara tatu pekee .

Takukuru kufatiria Matumizi , fedha za Umma

Picha
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ( Takukuru ), mkoani Kilimanjaro imesema mkakati wao mwaka huu ni kufuatilia matumizi ya fedha za umma zinazotolewa na serikali , ili zitumike kama zilivyokusudiwa . Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa Takukuru , Mkoa wa Kilimanjaro, Holle Makungu , alipokuwa akizungumza na wanahabari kuwa serikali inatoa fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo, lakini wapo baadhi ya watumishi wa umma ambao sio waadilifu na kuzifuja. Alisema, ili kuhakikisha lengo la serikali linakusudiwa, mkakati mkubwa watakaoutekeleza katika mwaka huu ni kufuatilia fedha hizo na utaanza zitakapotolewa na wizara kuhakikisha zinafika zote kwa mtumiaji, upatikanaji wa makandarasi, ulipwaji wa kandarasi na ukaguzi wa miradi. “Mpango huu utatoa uhakika kuwa fedha za umma zinatumika ipasavyo kwa ubora uliokusudiwa tofauti na ilivyokuwa awali, fedha nyingi zilichepushwa na kufanyiwa ubadhirifu, ndio maana tumekuwa tukiibua ub...

Ajibu Aipigia Magoti Yanga

Picha
Mshambuliaji wa Yanga , Ibrahim Ajibu . BAADA ya kipigo cha penalti 5-4 dhidi ya URA , juzi mshambuliaji wa Yanga , Ibrahim Ajibu Migomba ameom­ba radhi kwa mashabiki wa timu hiyo kuto­kana na ma­tokeo ma­baya . Yanga ilion­dolewa kwenye michuano ya Kombe la Map­induzi katika hatua ya nusu fainali na URA ya Uganda kutinga fainali dhidi ya Azam FC . Msham­buliaji huyo alisema hawakupenda kupata matokeo ya aina ile lakini ilitokea vile kwa sababu mpira una matokeo matatu. “Naomba mashabiki wetu wa Yanga wa­tusamehe kwa matokeo mabaya hakuna timu ambayo inapenda kupoteza zaidi mtupe sapoti ,”al­isema Ajibu. Hata hivyo katika mchezo huo wachezaji ambao wali­piga penalti ni Papy Tshishim­bi, Hassan Kessy, Gadiel Michael, Daud Raphael na Obrey Chirwa ambaye alikosa.

Neymar Aja na Style mpya ya Ushangiliaji

Picha
Nyota Mbrazil , Neymar Junior akiweka kiatu chake kichwani kushangilia bao la kwanza aliloifungia Paris Saint-Germain dakika ya 53 kwa penalti katika ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji , Amiens SC kwenye mchezo wa hatua ya 16 Bora Kombe la Ligi Ufaransa usiku wa jana Uwanja wa Licorne , Amiens. Bao la pili la PSG lilifungwa na Adrien Rabiot dakika ya 78

Siri ya Yanga kutolewa Mapinduzi cup

Picha
UMAKINI wa safu ya kiungo na ulinzi ya timu ya URA uliiwia vigumu mabingwa wa soka nchini Yanga kuweza kupata ushindi kwenye dakika 90 za mchezo wa nusu fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi . Yanga inayodhaminiwa na kampuni ya Sportpesa jana ilitolewa kwenye michuano hiyo , baada kufungwa kwa penalti 5-4 na Waganda hao ambao sasa wametinga hatua ya fainali . Pamoja na kumiliki mpira kwa asilimia 56, Yanga walikosa mbinu ya kuipita ngome ya ulinzi ya URA licha ya mashambulizi waliyoyafanya katika kipindi cha kwanza. URA imeendelea kuwa mwiba kwa timu za Tanzania baada ya kuzifunga Azam FC na Simba kwenye hatua ya makundi kabla ya kuifunga Yanga jana . Wafungaji wa penalti kwa upande wa Yanga ambayo jana Kocha wake Mkuu , George Lwandamina aliishuhudia timu yake akiwa jukwaani ,  walikuwa ni Papy Tshishimbi ,  Hassan Kessy ,  Raphael Daudi na Gabriel Michael, hu...

Rais Magufuli afanya uteuzi mwingine

Picha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Alphayo Kidata kuwa Balozi. Soma taarifa kamili:

Usajili wa Coutinho waiumiza United kwa Dyabala

Ni mwendo wa pesa tu barani Ulaya, na kwa sasa kila mchezaji maarufu ukimgusa lazima uwe na kuanzia £70m na ndio maana haikushangaza sana kwa Philippe Coutinho kwenda Barcelona kwa dau la £145m. Lakini usajili huu umeanza kuongeza thamani ya wachezaji wengine na vilabu vingine vimeamua kuongeza dau kwa wachezaji wao baada ya kuonekana kwamba lolote linawezekana katika biashara ya sasa ya soka. Moja kati ya vilabu ambavyo inatajwa kuongeza bei ya mchezaji wake ni klabu ya Juventus, ripoti kutoka nchini Italia zinasema kwa sasa Juventus wameamua kwamba kwa timu yoyote inayomtaka Paulo Dyabala lazima ije na £150m. Pamoja na taarifa kutoka kwa mkurugenzi wa Juventus Giussepe Marotta kwamba Juventus haiwezi kumuuza Dyabala kwa kiasi chochote kile cha pesa lakini jarida moja la michezo nchini Italia limefahamu kuhusu mauzo ya Dyabala. Manchester United wanaonekana mstari wa mbele kumnunua Dyabala ambapo hapo mwanzo alitajwa kuwa na thamani ya £80m lakini sasa itawalaz...

U.R.A YAITUPA NJE YANGA MAPINDUZI CUP

Picha
YANGA SC itapanda boti kurejea mjini Dar es Salaam kesho baada ya kutolewa kwenye michuano ya Kombe la Mapunduzi kwa penalti 5-4 na URA ya Uganda kufuatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 jioni ya leo Uwanja wa Amaan , Zanzibar. Yanga SC imeendeleza utamaduni wake wa kufanya vibaya kwenye hatua ya matuta baada ya mshambuliaji wake Mzambia , Obrey Chirwa kumdakisha mpira kipa wa URA, Alionzi Nafian. Chirwa alikosa penalti ya mwisho ya Yanga baada ya wenzake wote wanne, Mkongo Papy Kabamba Tshishimbi na wazalendo Hassan Ramadhani Kessy, Raphael Daudi Lothi na Gardiel Michael Mbaga kufunga. Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Issa Hajji, aliyesaidiwa na Shehe Suleiman na Mwanahija Makame, penalti za URA zilifungwa na Patrick Mbowa, Enock Kigumba, Shafiq Kagimu, Jimmy Kulaba na Brian Majwega. Katika dakika 90 za mchezo timu zote zilishambuliana kwa zamu, ingawa URA ndiyo walioonekana kulitia misukosuko zaidi lango la Yanga. Tofauti na ilivyot...

NI YANGA NA URA, AZAM FC NA SINGIDA UNITED NUSU FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI JUMATANO ZANZIBAR

Picha
YANGA SC itakutana na URA ya Uganda katika Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi Jumatano Uwanja wa Amaan, Zanzibar wakati Singida United itacheza na Azam FC. Hiyo ni baada ya Yanga kutoka sare ya 1-1 na Singida United katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi usiku huu Uwanja wa Amaan. Nusu Fainali ya kwanza itakuwa kati ya Yanga na URA Saa 10:30 jioni na saa 2:15 usiku Singida United na Azam zitachukua nafasi kwa mujibu wa ratiba kama hakutakuwa na mabadiliko. Upo uwezekano mkubwa, mchezo kati ya Azam FC na Singida ukatangulia jioni na Yanga na URA wakahamishiwa usiku. Katika mchezo usiku wa leo wa Kundi B, baada ya dakika 45 ngumu za kipindi cha kwanza, Singida United walitangulia kwa bao la mshambuliaji Daniel Lyanga dakika ya 72 aliyefunga kwa kichwa akimalizia mpira wa adhabu wa kiungo Kiggi Makassy kutoka nje kidogo ya boksi upande wa kushoto. Yanga wakasawazisha katika mazingira yale yale, mpira wa adhabu wa kiungo mshambuliaji Ibrahim Ajib kutoka upande wa kulia ulipounga...

Hali mbaya Sudan wananchi waandamana kisa mkate

Picha
Sudan imekumbwa na maandamano katika miji mbalimbali kutokana na ongezeko la bei ya mkate. Habari zinasema gharama zimeongezeka mara mbili na sababu kubwa ni hatua ya serikali kuondoa ruzuku ya vyakula uamuzi ambao umesababisha bei ya mkate kuwa mara dufu. Maandamano yaliyofanyika magharibi mwa Darfur yamesababisha mwanafunzi mmoja kuuawa na wengine sita kujeruhiwa baada ya kuzuka fujo. Vyombo vya habari vimeripoti kwamba polisi walitumia mabomu ya machozi kutawanya watu ambao walikuwa wamefunga barabara na kuchoma matairi katika barabara za mji mkuu wa Khartoum. Lakini naibu waziri wa mambo ya ndani alisema maandamano hayo hayakutokana na ongezeko la bei na akaahidi kuwashughulikia wote waliofanya maandamano yenye fujo. Pia, Serikali imezuia kuuzwa mitaani magazeti yote yaliyokosoa ongezeko la bei. Vyanzo vya uhakika vimezema uamuzi wa kuongeza bei ya mkate umefikiwa na serikali ikiwa ni utekelezaji wa matakwa ya kufufua uchumi yaliyotolewa na IMF.

Dalili 6 zitakazokuonyesha kuwa mwenzi wako ana mtu mwingine katika mahusiano

Picha
Mahusiano yoyote yale huhitaji mtu mwenye uvumilivu, imara, mkweli na muwazi lakini hivi vyote vikishindikana basi, mahusiano hayo huingia doa. Watu kuwa na wapenzi wawili wawili huenda ikawa sijambo geni, lakini ni jambo geni pale mwezi wako akilifanya. Matatizo haya yamekuwepo kwa miaka mingi, lakini sidhani kama yatakuja kuzoeleka, maana kila mmoja hapa anahitaji upendo wa dhati na wakwake tuu, usio na kugawana na mtu mwingine. Vitabu vya dini vinasisitiza upendo ulio mmoja katika mahusiano yaliyohalalishwa na Mwenyezi Mungu mwenyewe, 'tuliheshimu hili'. Katika makala hii inayolenga kukuonyesha dalili za mwenzi wako kutoka nje ya mahusiano, kwa kiasi kikubwa itakusaidia wewe kuwa sehemu sahihi. Dalili 6 zitakazokuonyesha kuwa mpenzi wako anamahusiano nje ya ndoa au urafiki wenu. 1.  Mmekuwa wawazi kwa muda sasa, yani mwenzi wako amekuwa akishea na wewe mambo mbalimbali ya siku nzima, ghafla anaanza kuchelewa kurudi kutoka kazini, na akirudi hakuambii alikuwa wapi. 2....

Moto wazuka jumba la Trump New York

Picha
Maafisa wa kuzima moto wameitwa katika jumba la Trump Tower katika kisiwa cha Manhattan jijini New York kuzima moto uliokuwa umezuka kwenye ghorofa ya juu ya jengo hilo. Idara ya kuzima moto ya New York imesema moto huo ulidhibitiwa na kwamba hakukuwa na majeruhi. Shirika la habari la CBS News limesema moto huo ulizuka mwendo wa saa moja asubuhi saa za huko (saa sita mchana GMT) karibu na paa la jumba hilo la ghorofa 68. Jumba hilo lilikuwa makazi rasmi ya Bw Trump kabla ya kuapishwa kwake karibu mwaka mmoja uliopita. CBS News wamepakia picha za wazima moto wakiwa kwenye paa la jumba hilo huku moshi ukifuka kutoka kwa sehemu moja ya jumba hilo.

Simba Yatolewa Mapinduzi Cup na U.R.A

Picha
Rasmi Simba wameng’olewa katika michuano ya Mapinduzi kwa kuchapwa bao 1-0 na URA ya  Uganda. Kipigo hicho leo kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar kimekuwa cha pili mfululizo kwa Simba . Mechi iliyopita , Simba ilikutana na kipigo kama hicho kutoka kwa Azam FC na matumaini yao kuendelea ilikuwa leo dhidi ya URA . Bao la URA lilipatikana dakika za nyongeza za kipindi cha kwanza na kipindi chote cha pili, Simba ilishindwa kupata angalau bao moja.

Mbona wanawake wengi hufa kutokana na mshtuko wa moyo kuliko wanaume?

Picha
Ni wamawake wachache ambao hupatwa na matatizo ya mshtuko wa moyo wanaoweza kufa ikiwa watapata matibabu sawa na yale wanayopewa wanaume, uchunguzi umeonyesha. Utafiti huo uliangazia matokeo ya wagonjwa 180,368 nchini Sweden ambao walikumbwa na mshtuko wa moyo katika kipindi cha miaka 10. Waligundua kuwa wanawake wako mara tatu zaidi ya kufa kutokana na mshtuko wa moyo kuliko wanaume wanapopatwa na hali hiyo. Wakfu wa British Heart Foundation, ulisema kuwa mshtuko wa moto mara nyingi huonekana kama tatizo la wanaume lakini wanawake zaidi hufa kutokana na magonjwa ya moyo hata kuliko saratani. Watafiti katika chuo cha Leeds na taasisi ya Karolinska nchini Sweden walikusanya takwimu kutoka na sajili ya ugonjwa wa moyo ya mtandaoni ya sweden. Waligundua kuwa wanawake walikuwa na uwezekano mdogo wa kupata matibabu yanayostahili baada ya kupatwa na mshtuko wa moyo. Prof Chris Gale, wa chuo cha Leeds, ambaye aliandika utafiti huo alisema hii ni kutokana na sababu ya fikra za umma na h...

Ndugai Ampa Pongezi Magufuli

Picha
Spika wa Bunge Mhe . Job Ndugai amempa pongezi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt . John Pombe Magufuli kwa kuweza kusikiliza maoni ya Bunge na wabunge kwa kutekeleza moja ya maombi yao kuigawa Wizara ya Nishati na Madini . Ndugai ametoa pongezi hizo leo Januari 8, 2018 akiwa Ikulu jijini Dar es Salaam katika hafla ya kuapishwa kwa Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Doto Mashaka Biteko na kusema kwa miaka mingi walikuwa wakitaka Wizara hizo kugawanywa lakini ilikuwa inashindikana ila katika awamu ya tano Rais Magufuli ndiyo ameweza kufanya hivyo. "Sisi Bunge tulikuwa tukishauri toka miaka ya nyuma kwa Serikali kwamba Wizara iliyokuwa inaitwa Wizara ya Nishati na Madini ilikuwa ni nzito mno, ilikuwa imejaza mambo mengi sana kwa wakati mmoja ushauri wetu ulikuwa ni vizuri kuzitenganisha na kuzisimika kila moja kivyake. Jambo hili Mhe. Rais umelitekeleza kabisaa kwenye awamu ya tano umeunda wizara mbili na hata tendo la leo linadhirish...

ARSENAL WATEMESHWA UBINGWA WA FA NA 'TIMU YA MCHANGANI'

Picha
Wachezaji wa Arsenal wakierejea katikati kinyonge kuanzisha mpira baada ya kufungwa bao la tatu katika kipigo cha 4-2 mbele ya wenyeji, Nottingham Forest katika mchezo wa Raundi ya Tatu ya Kombe la FA leo Uwanja wa The City Ground mjini Nottingham, Nottinghamshire. Arsenal waliokuwa mabingwa watetezi wanavuliwa ubingwa na kutolewa na timu hiyo ya Daraja la Kwanza, Championship. Mabao ya Nottingham yamefungwa na Eric Lichaj mawili dakika ya 20 na 44, Ben Brereton kwa penalti dakika ya 64 na Kieran Dowell kwa penalti pia dakika ya 85, wakati ya Arsenal yamefungwa na Per Mertesacker dakika ya 23 na Danny Welbeck dakika ya 79 

MESSI, SUAREZ WOTE WAFUNGA BARCA YAUA 3-0 LA LIGA

Nyota wa Barcelona, Luis Suarez, Lionel Messi na Paulinho baada ya wote kufunga katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Levante kwenye mchezo wa La Liga leo Uwanja wa Camo Nou. Messi alifunga dakika ya 12, Suarez dakika ya 38 na Paulinho dakika ya 90 na ushei 

AJIBU nenda Ulaya, usiridhike na Chipsi Mayai

Picha
Priva ABIUD Nmeona umri wa Ibrahim kwenye mitandao. Inasemekana ana Miaka 21. Sawa haina tatizo. Ni umri sahihi kwa mwanasoka mwenye ndoto za kucheza ligi kubwa ulaya. Sijui chochote kuhusu Ajib. Nimemuona mara kadhaa akicheza. Sio kwamba anajua sana. Ila ni mtu ambaye nina iman akipata nafasi hafanyi makosa. Ana mguu wenye ladha ya soka. Mguu wake una maelewano mazuri na mpira. Kimsingi niseme kibongo bongo basi nae anajua jua ila mimi naona bado sana. Siwezi kumfananisha na mshambuliaji yoyote ulaya. Maana hafanani nao kabisa. Bado naona soka lake ni la kitanzania. Lakini umri wake na uwezo wake unafaa kwenda ulaya. Unamruhusu kujifunza lugha ya mpira  wa ulaya nae akawa kama wa ulaya. Nataka nimwambie Ajibu kucheza Yanga na Simba si kitu. Utaishia kututishia kula chipsi mayai na kuendesha Passo lakini kisoka tunakuona mwenzetu tu. Ajib nataka nimwambie sisi tumewazidi Indonesia Viwango vya FIFA. Indonesia wapo nafasi ya 162 huko sisi tupo ya 147. Tena wao walishawahi kushuka ...

Ugonjwa wa Chango La Uzazi

Picha
Tunapozungumzia mgonjwa wa chango tuna maana kuwa ni matatizo yaliyopo katika viungo vya uzazi kwa mke au mume . Huu ni ugonjwa ambao humpata mtu katika umri mdogo utotoni . Kwa mfano :- mume , hupata maumivu ya tumbo mara kueneza anapokuwa mdogo . Kwa upande wa mwanamke hupata maumivu ya tumbo anapoanza kuvunja ungo . Maumivu hayo hupelekea mtu ( mume / mwanamke ) kupata madhara katika viungo vyake vya uzazi. DALILI ZAKE Kwa mwanaume atakuwa akishiriki tendo la ndoa, anawahi sana kufika kileleni na kurudia mara nyingine ni vigumu sana. Pia mwanaume hatakuwa na uwezo wa kusimamisha. Ni vigumu kumpa mimba mwanamke. Mwanamke mwenye chango la uzazi ana dalili zifuatazo:- Kupata maumivu makali wakati anapokaribia kuingia katika siku zake za hedhi Kuhisi maumivu makali wakati wa kushiriki tendo la ndoa Siku zake za hedhi hazitakuwa na ratiba, zitakuwa zinabadilika badilika Hujisikia homa kali anapokaribia siku zake za dhedhi Kupatwa has...