TAARIFA MPYA

Madhara ya Chai na Kahawa Kiafya

Picha
CAFFEINA/KAFEINA. Kafeina ni nini?: 1. Kafeina ni madawa ya kulevya kundi la ‘Stimulants drugs’. Utashangaa. Habari ndiyo hiyo. Hii ndiyo sababu kwa mtu aliyezoea kunywa chai hii kila siku au kahawa, siku asipokunywa kichwa humuuma, ni kwa sababu amekuwa mtegemezi au teja wa kafeina. Kafeina ni kiungo mhimu karibu katika soda zote zenye rangi nyeusi; Coca-cola, Pepsi, Sayona nyeusi, Azam cola na kadharika. Kafeina huongezwa pia katika Red bull, Malta na katika baadhi ya dawa za kupunguza maumivu mwilini. Kwahiyo Kafeina ambayo hupatikana katika chai na kahawa ni aina mojawapo ya madawa ya kulevya. 2. Kafeina ni kikojoshi (diuretics). Kafeina ni dawa ya kukufanya ukojowe. Ukinywa kikombe kimoja cha kinywaji chenye kafeina yaani chai au kahawa, basi muda si mrefu utaenda kukojoa vikombe viwili. Kwa sababu kafeina ni taka isiyotakiwa mwilini, mwili utafanya kila uwezalo ikibidi ujikamuwe wenyewe kupata maji ya ziada kuweza kuitoa kafeina hii uliyoinywa kwa kisingizio ch...

Siri ya Yanga kutolewa Mapinduzi cup


UMAKINI wa safu ya kiungo na ulinzi ya timu ya URA uliiwia vigumu mabingwa wa soka nchini Yanga kuweza kupata ushindi kwenye dakika 90 za mchezo wa nusu fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi.

Yanga inayodhaminiwa na kampuni ya Sportpesa jana ilitolewa kwenye michuano hiyo, baada kufungwa kwa penalti 5-4 na Waganda hao ambao sasa wametinga hatua ya fainali.

Pamoja na kumiliki mpira kwa asilimia 56, Yanga walikosa mbinu ya kuipita ngome ya ulinzi ya URA licha ya mashambulizi waliyoyafanya katika kipindi cha kwanza.

URA imeendelea kuwa mwiba kwa timu za Tanzania baada ya kuzifunga Azam FC na Simba kwenye hatua ya makundi kabla ya kuifunga Yanga jana.

Wafungaji wa penalti kwa upande wa Yanga ambayo jana Kocha wake Mkuu, George Lwandamina aliishuhudia timu yake akiwa jukwaaniwalikuwa ni Papy TshishimbiHassan Kessy,  Raphael Daudi na Gabriel Michael, huku Obrey Chirwa akikosa penalti ya mwisho.

Penalti za URA zilifungwa na Kalama DebossKibumba Enock, Kagimu ShafikKulaba Jimmy na Brian Majwega.

KIPINDI CHA KWANZA

Kipindi cha kwanza kilianza kwa URA kuwahi kufika langoni mwa Yanga katika dakika ya kwanza tu ya kipindi hicho, lakini shuti la mshambuliaji Bokota Labama lilitoka nje ya lango la Yanga.

Winga Kagamba Nicholas wa URA aliachia shoti dakika ya pili, lakini kipa wa Yanga, Youthe Rostand alilipangua na kuwa kona tasa.

Huku timu zote zikisoma, dakika  ya tisa  kiungo wa Yanga aliachia shuti kali langoni mwa URA akiwa nje ya 18, lakini liliwababatiza mabeki wa URA kabla ya kipa kudaka.

Kuanzia dakika ya 15, Yanga ilitawala mchezo, lakini kama ilivyokuwa dakika za mwanzo kwa URA, nayo haikuwa na mipango mizuri ya kutengeneza bao.

URA walirudi langoni mwa Yanga dakika ya 24 ila Rostand alikuwa makini na kulicheza shuti la Deboss.

Kama Yanga ingekuwa makini dakika ya 33 ubao wa matangazo kwenye uwanja wa Amaan mjini hapa ungeweza kubadilikalakini Ibrahimu Ajibu na Juma Mahadhi walijichanganya katika kuuwahi mpira mrefu uliopigwa na Hassan Kessy hivyo kumpa nafasi kipa Alionzi Nafian kudaka kirahisi.

Kipindi cha pili URA walianza tena kwa kasi na katika dakika ya kwanza ya kipindi hicho ilifanya shambulizi kali, lakini Rostam alikuwa makini kuokoa hatari.

Katika dakika ya 49 hadi ya 52 Yanga iliweka kambi langoni mwa URA na kupata kona tatu, lakini hazikifanikiwa kuzaa matunda.

 Licha ya Yanga kufanya mabadiliko katika dakika ya 53 kwa kumtoa Buswita na kumuingiza Obrey Chirwa bado hakukusaidia timu hiyo kupata bao.

URA sasa itacheza fainali na mshindi wa mchezo wa jana usiku kati ya Azam FC dhidi ya Singida United.

 Vikosi Yanga: Youthe Rostand, Hassan Hamisi, Mwinyi Haji,  Andrew Vicent, Kelvin Yondani,  Said Juma, Pius Buswita,  Papy Tshishimbi, Juma Mahadhi,  Ibrahim Ajibu,  Emmanuel Martin

URA: Alionzi Nafian,  Kibumba Enoch,  Majwega Brian,  Munaamba Allan,  Mbowa Patrick,  Mutyaba Julius,  Kagaba Nicholas,  Kalama Deboss, Bokota Labama,  Kagimu Shafik,  Ssempa Charles.

Maoni

ZILIZO SOMWA MARA NYINGI

ULAJI WA MARA KWA MARA WA MBEGU ZA MABOGA HUKUKINGA NA KUKUEPUSHA NA MAGONJWA 1O MWILINI MWAKO...

Dalili 6 zitakazokuonyesha kuwa mwenzi wako ana mtu mwingine katika mahusiano

FAIDA YA JUICE YA KAROTI KATIKA MWILI WA BINADAM

DAWA BORA YA NGUVU ZA KIUME NA MAUMBILE MADOGO

AINA ZA MBOLEA & MATUMIZI YAKE KITAALAM

Madhara ya Chai na Kahawa Kiafya

Fahamu Aina 7 Za Juisi Zenye Kuondoa Sumu Mwilini

Ugonjwa wa Chango La Uzazi

Madhara Ya Kuangalia Video za Porno {Ngono} na Namna ya Kujizuia

Athari za kiafya za vyakula vyenye Wanga