TAARIFA MPYA

Madhara ya Chai na Kahawa Kiafya

Picha
CAFFEINA/KAFEINA. Kafeina ni nini?: 1. Kafeina ni madawa ya kulevya kundi la ‘Stimulants drugs’. Utashangaa. Habari ndiyo hiyo. Hii ndiyo sababu kwa mtu aliyezoea kunywa chai hii kila siku au kahawa, siku asipokunywa kichwa humuuma, ni kwa sababu amekuwa mtegemezi au teja wa kafeina. Kafeina ni kiungo mhimu karibu katika soda zote zenye rangi nyeusi; Coca-cola, Pepsi, Sayona nyeusi, Azam cola na kadharika. Kafeina huongezwa pia katika Red bull, Malta na katika baadhi ya dawa za kupunguza maumivu mwilini. Kwahiyo Kafeina ambayo hupatikana katika chai na kahawa ni aina mojawapo ya madawa ya kulevya. 2. Kafeina ni kikojoshi (diuretics). Kafeina ni dawa ya kukufanya ukojowe. Ukinywa kikombe kimoja cha kinywaji chenye kafeina yaani chai au kahawa, basi muda si mrefu utaenda kukojoa vikombe viwili. Kwa sababu kafeina ni taka isiyotakiwa mwilini, mwili utafanya kila uwezalo ikibidi ujikamuwe wenyewe kupata maji ya ziada kuweza kuitoa kafeina hii uliyoinywa kwa kisingizio ch...

Dalili 6 zitakazokuonyesha kuwa mwenzi wako ana mtu mwingine katika mahusiano


Mahusiano yoyote yale huhitaji mtu mwenye uvumilivu, imara, mkweli na muwazi lakini hivi vyote vikishindikana basi, mahusiano hayo huingia doa.

Watu kuwa na wapenzi wawili wawili huenda ikawa sijambo geni, lakini ni jambo geni pale mwezi wako akilifanya.

Matatizo haya yamekuwepo kwa miaka mingi, lakini sidhani kama yatakuja kuzoeleka, maana kila mmoja hapa anahitaji upendo wa dhati na wakwake tuu, usio na kugawana na mtu mwingine.

Vitabu vya dini vinasisitiza upendo ulio mmoja katika mahusiano yaliyohalalishwa na Mwenyezi Mungu mwenyewe, 'tuliheshimu hili'.

Katika makala hii inayolenga kukuonyesha dalili za mwenzi wako kutoka nje ya mahusiano, kwa kiasi kikubwa itakusaidia wewe kuwa sehemu sahihi.

Dalili 6 zitakazokuonyesha kuwa mpenzi wako anamahusiano nje ya ndoa au urafiki wenu.

1.  Mmekuwa wawazi kwa muda sasa, yani mwenzi wako amekuwa akishea na wewe mambo mbalimbali ya siku nzima, ghafla anaanza kuchelewa kurudi kutoka kazini, na akirudi hakuambii alikuwa wapi.

2.  Umekuwa ukikaribishwa kumtembelea kazini kwake, lakini siku hizi anatengeneza sababu nyingi za kukuweka mbali na maeneo ya kazini kwake kabisaa.

3.  Siku moja unapanda katika gari ya mkeo au mmeo alafu unataka kufungua kile kibox kilichopo pale mbele ambacho huwa kinatumika kuhifadhia vitu mbali mbali, mara unakuta kimefungwa kabisa na mwenzi wako anagoma kukifungua.

4.  Ghafla mkeo/mme anaanza kujifungia bafuni anapokwenda kuoga, na hakuwa anafanya hivyo, je huenda akawa anatumia muda huo kuwasiliana na mtu mwingine kwa njia ya maandishi?

5.  Mke/mme wako ana mikutano au mitoko na marafiki na kumbuka kukuhusu sehemu wanayokwenda inautata, mfano disco, bar usiku alafu hakuambii n.k.

6.  Mpenzi wako anageuka kuwa msiri katika mambo yake, yani anakuficha nywila/passwod ya simu au laptop yake, tofauti na mwanzoni alikuwa anakuweka wazi.

Hayo na mengine mengi yanaweza kukufanya ukaona kuwa ni sehemu kubwa ya kuwa mumeo/mkeo anamahusiano na mtu mwingine nje ya mahusiano yenu.

Angalizo:  Dalili zote hizo 6 huenda mpenzi wako akawanazo baadhi tu, kwa mfano kuchelewa kazini, usiri wa kazini n.k hii aimaanishi tu ni msaliti wa mapenzi, hapana wakati mwingine ziko sababu za msingi zinazo msababisha yeye kufanya hivyo na sio kuchepuka. 

Maoni

ZILIZO SOMWA MARA NYINGI

ULAJI WA MARA KWA MARA WA MBEGU ZA MABOGA HUKUKINGA NA KUKUEPUSHA NA MAGONJWA 1O MWILINI MWAKO...

FAIDA YA JUICE YA KAROTI KATIKA MWILI WA BINADAM

DAWA BORA YA NGUVU ZA KIUME NA MAUMBILE MADOGO

AINA ZA MBOLEA & MATUMIZI YAKE KITAALAM

Madhara ya Chai na Kahawa Kiafya

Fahamu Aina 7 Za Juisi Zenye Kuondoa Sumu Mwilini

Ugonjwa wa Chango La Uzazi

Madhara Ya Kuangalia Video za Porno {Ngono} na Namna ya Kujizuia

Athari za kiafya za vyakula vyenye Wanga