TAARIFA MPYA
Ndugai Ampa Pongezi Magufuli
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai amempa pongezi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuweza kusikiliza maoni ya Bunge na wabunge kwa kutekeleza moja ya maombi yao kuigawa Wizara ya Nishati na Madini.
Ndugai ametoa pongezi hizo leo Januari 8, 2018 akiwa Ikulu jijini Dar es Salaam katika hafla ya kuapishwa kwa Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Doto Mashaka Biteko na kusema kwa miaka mingi walikuwa wakitaka Wizara hizo kugawanywa lakini ilikuwa inashindikana ila katika awamu ya tano Rais Magufuli ndiyo ameweza kufanya hivyo.
"Sisi Bunge tulikuwa tukishauri toka miaka ya nyuma kwa Serikali kwamba Wizara iliyokuwa inaitwa Wizara ya Nishati na Madini ilikuwa ni nzito mno, ilikuwa imejaza mambo mengi sana kwa wakati mmoja ushauri wetu ulikuwa ni vizuri kuzitenganisha na kuzisimika kila moja kivyake. Jambo hili Mhe. Rais umelitekeleza kabisaa kwenye awamu ya tano umeunda wizara mbili na hata tendo la leo linadhirisha kabisa jinsi ambavyo unazidi kuimarisha sekta ya Nishati na Madini kwa hili tunakushukuru sana kwani linaonesha dhamira yako ilivyo" alisema Ndugai
Mbali na hilo Ndugai amesema kuwa katika miaka ya nyuma katika sekta ya madini na nishati kama nchi tumeliwa sana hivyo anaamini kuwa katika Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli na wateule wake jambo hilo halitaweza kuendelea tena.
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linatarajiwa kuanza mnamo Januari 30, 2018 Makao Makuu ya nchi mjini Dodoma.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni
TAFADHARI !!
- Tumia Lugha Nzuri Kutoa Maoni
Usitumie kauli za Karaha AU Zenye Kukela :
C.E.O
Gneous OG