TAARIFA MPYA
Mbona wanawake wengi hufa kutokana na mshtuko wa moyo kuliko wanaume?
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Ni wamawake wachache ambao hupatwa na matatizo ya mshtuko wa moyo wanaoweza kufa ikiwa watapata matibabu sawa na yale wanayopewa wanaume, uchunguzi umeonyesha.
Utafiti huo uliangazia matokeo ya wagonjwa 180,368 nchini Sweden ambao walikumbwa na mshtuko wa moyo katika kipindi cha miaka 10.
Waligundua kuwa wanawake wako mara tatu zaidi ya kufa kutokana na mshtuko wa moyo kuliko wanaume wanapopatwa na hali hiyo.
Wakfu wa British Heart Foundation, ulisema kuwa mshtuko wa moto mara nyingi huonekana kama tatizo la wanaume lakini wanawake zaidi hufa kutokana na magonjwa ya moyo hata kuliko saratani.
Watafiti katika chuo cha Leeds na taasisi ya Karolinska nchini Sweden walikusanya takwimu kutoka na sajili ya ugonjwa wa moyo ya mtandaoni ya sweden.
Waligundua kuwa wanawake walikuwa na uwezekano mdogo wa kupata matibabu yanayostahili baada ya kupatwa na mshtuko wa moyo.
Prof Chris Gale, wa chuo cha Leeds, ambaye aliandika utafiti huo alisema hii ni kutokana na sababu ya fikra za umma na hata kwa madaktari kuhusu ni vipi mtu aliyepatwa na mshutuko wa moyo anastahili kuwa.
"Kawaida tunapofikiria kuhusu mgonjw aaiyepatwa na na mshutuko wa moyo, tanamuona mwanamume wa makamo aliye na uzito mkubwa wa mwili na kisukari na anayevuta sigara.
"Hii sio ukweli kwa sababu mshtuko wa moyo huwapata watu wengi wakiwemo wanawake."
Takriban wanaume 124,000 na wanawake 70,000 hulazwa hospiytalini kutokana na mshtuko wa moyo nchini Uingereza kila mwaka
Prof Gale alisema kuanzia wakati wa mgonjwa anakutana kwa mara ya kwanza na madaktari, wanawake wako katika hali ya kutopata uchunguzi unaostahili ikilinganishwa na wanaume.
Utafiti huo ulingundua kuwa wanawake pia walikuwa na uwezekano wa kupatwa na magonjwa mengine kama kisukari na shinikizo la damu.
Huku utafiti huu ukiwa unatumia takwimu za Sweden, watafiti wanasema kuwa wanawake nchini Uingerea wako katika hali mbaya kwa kuwa wengi hufariki kutokana na mshutuko wa moyo.
Sweden ni nchi inayoongoza kwa huduma za matibabu ikiwa na vifo vichache zaidi vinavyotokana na mshutuko wa moyo, lakini pia kuna hata hivyo mwanya mkuwa wa matibabu uliopo kati ya wanaume na wanawake.
Prof Jeremy Pearson kutoka British Heart Foundation, anasema kuwa matokeo hayo ni ya kutia wasi wasi.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni
TAFADHARI !!
- Tumia Lugha Nzuri Kutoa Maoni
Usitumie kauli za Karaha AU Zenye Kukela :
C.E.O
Gneous OG