TAARIFA MPYA

Madhara ya Chai na Kahawa Kiafya

Picha
CAFFEINA/KAFEINA. Kafeina ni nini?: 1. Kafeina ni madawa ya kulevya kundi la ‘Stimulants drugs’. Utashangaa. Habari ndiyo hiyo. Hii ndiyo sababu kwa mtu aliyezoea kunywa chai hii kila siku au kahawa, siku asipokunywa kichwa humuuma, ni kwa sababu amekuwa mtegemezi au teja wa kafeina. Kafeina ni kiungo mhimu karibu katika soda zote zenye rangi nyeusi; Coca-cola, Pepsi, Sayona nyeusi, Azam cola na kadharika. Kafeina huongezwa pia katika Red bull, Malta na katika baadhi ya dawa za kupunguza maumivu mwilini. Kwahiyo Kafeina ambayo hupatikana katika chai na kahawa ni aina mojawapo ya madawa ya kulevya. 2. Kafeina ni kikojoshi (diuretics). Kafeina ni dawa ya kukufanya ukojowe. Ukinywa kikombe kimoja cha kinywaji chenye kafeina yaani chai au kahawa, basi muda si mrefu utaenda kukojoa vikombe viwili. Kwa sababu kafeina ni taka isiyotakiwa mwilini, mwili utafanya kila uwezalo ikibidi ujikamuwe wenyewe kupata maji ya ziada kuweza kuitoa kafeina hii uliyoinywa kwa kisingizio ch...

Hali mbaya Sudan wananchi waandamana kisa mkate

Sudan imekumbwa na maandamano katika miji mbalimbali kutokana na ongezeko la bei ya mkate.

Habari zinasema gharama zimeongezeka mara mbili na sababu kubwa ni hatua ya serikali kuondoa ruzuku ya vyakula uamuzi ambao umesababisha bei ya mkate kuwa mara dufu.

Maandamano yaliyofanyika magharibi mwa Darfur yamesababisha mwanafunzi mmoja kuuawa na wengine sita kujeruhiwa baada ya kuzuka fujo.

Vyombo vya habari vimeripoti kwamba polisi walitumia mabomu ya machozi kutawanya watu ambao walikuwa wamefunga barabara na kuchoma matairi katika barabara za mji mkuu wa Khartoum.

Lakini naibu waziri wa mambo ya ndani alisema maandamano hayo hayakutokana na ongezeko la bei na akaahidi kuwashughulikia wote waliofanya maandamano yenye fujo. Pia, Serikali imezuia kuuzwa mitaani magazeti yote yaliyokosoa ongezeko la bei.

Vyanzo vya uhakika vimezema uamuzi wa kuongeza bei ya mkate umefikiwa na serikali ikiwa ni utekelezaji wa matakwa ya kufufua uchumi yaliyotolewa na IMF.

Maoni

ZILIZO SOMWA MARA NYINGI

ULAJI WA MARA KWA MARA WA MBEGU ZA MABOGA HUKUKINGA NA KUKUEPUSHA NA MAGONJWA 1O MWILINI MWAKO...

Dalili 6 zitakazokuonyesha kuwa mwenzi wako ana mtu mwingine katika mahusiano

FAIDA YA JUICE YA KAROTI KATIKA MWILI WA BINADAM

DAWA BORA YA NGUVU ZA KIUME NA MAUMBILE MADOGO

AINA ZA MBOLEA & MATUMIZI YAKE KITAALAM

Madhara ya Chai na Kahawa Kiafya

Fahamu Aina 7 Za Juisi Zenye Kuondoa Sumu Mwilini

Ugonjwa wa Chango La Uzazi

Madhara Ya Kuangalia Video za Porno {Ngono} na Namna ya Kujizuia

Athari za kiafya za vyakula vyenye Wanga