Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Desemba 31, 2017

TAARIFA MPYA

Madhara ya Chai na Kahawa Kiafya

Picha
CAFFEINA/KAFEINA. Kafeina ni nini?: 1. Kafeina ni madawa ya kulevya kundi la ‘Stimulants drugs’. Utashangaa. Habari ndiyo hiyo. Hii ndiyo sababu kwa mtu aliyezoea kunywa chai hii kila siku au kahawa, siku asipokunywa kichwa humuuma, ni kwa sababu amekuwa mtegemezi au teja wa kafeina. Kafeina ni kiungo mhimu karibu katika soda zote zenye rangi nyeusi; Coca-cola, Pepsi, Sayona nyeusi, Azam cola na kadharika. Kafeina huongezwa pia katika Red bull, Malta na katika baadhi ya dawa za kupunguza maumivu mwilini. Kwahiyo Kafeina ambayo hupatikana katika chai na kahawa ni aina mojawapo ya madawa ya kulevya. 2. Kafeina ni kikojoshi (diuretics). Kafeina ni dawa ya kukufanya ukojowe. Ukinywa kikombe kimoja cha kinywaji chenye kafeina yaani chai au kahawa, basi muda si mrefu utaenda kukojoa vikombe viwili. Kwa sababu kafeina ni taka isiyotakiwa mwilini, mwili utafanya kila uwezalo ikibidi ujikamuwe wenyewe kupata maji ya ziada kuweza kuitoa kafeina hii uliyoinywa kwa kisingizio ch...

CHELSEA YAKWAA KISIKI KOMBE LA FA, SARE 0-0 NA NORWICH

Picha
Kiungo Mbrazil wa Chelsea, Willian akimtoka beki wa Norwich City, Timm Klose katika mchezo wa Raundi ya Tatu Kombe la FA England jana Uwanja wa Carrow Road mjini Norwich, Norfolk timu hizo zikitoka sare ya 0-0 na sasa zitarudiana kutafuta timu ya kwenda Raundi ya Nne ya michuano hiyo PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

KOCHA MROMANIA WA AZAM AMEKUBALI KWA YULE MGHANA.

Picha
Bosi wa benchi la ufundi la Azam FC, Aristica Cioaba, raia wa Romania na wasaidizi wake, wanakoshwa na soka la mshambuliaji wao mpya, Bernard Arthur raia wa Ghana ambaye amekuwa msaada mkubwa katika ushambuliaji.  Arthur amejiunga na Azam akitokea Liberty Professional ya kwao Ghana, Jumatano wiki hii aliiongoza timu hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Jamhuri kwenye Kombe la Mapinduzi. Katika ushindi huo, Arthur alifunga bao moja kati ya matatu waliyopata na kuiwezesha Azam kufikisha pointi sita kabla ya mchezo wa jana dhidi ya URA na leo dhidi ya Simba.  Cioaba alisema Arthur amekuwa msaada katika safu yao ya ushambuliaji ambayo ilikuwa inafunga mabao machache. “Amekuja vizuri kwa kuingia ndani ya timu na kutupa matokeo yale ambayo tulikuwa tunayataka sisi, utaona kwamba ana muendelezo mzuri wa kufunga tangu alipoanza kutufungia dhidi ya Stand United katika ligi kuu. “Naamini kwa uwezo wake kuna kitu kikubwa ambacho atakifanya kwenye mechi zinazoku...

Serikali yamjibu Lissu

Picha
Saa chache tu baada ya Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu kufanya mkutano na waandishi wa habari katika Hospitali ya Nairobi Kenya ambapo alikuwa akipatiwa matibabu na katika mazungumzo yake kuihusisha serikali na tukio la yeye kushambuliwa Mjini Dodoma September 7, 2017, Msemaji Mkuu wa Serikali Dr Hassan Abbas amezungumza. Kupitia ukurasa wake wa Twitter Dr. Abbas ameandika ujumbe unaosema “Mhe Lissu bado ni mgonjwa na yuko wodini hivyo Serikali haioni busara kulumbana naye kwa sasa, Tunaendelea kumuombea apone haraka.”

Dodoma, Alliance, zaponza waamuzi daraja la kwanza

Kamati ya uendeshaji na usimamizi ya Bodi ya Ligi imewachukulia hatua waamuzi wote waliochezesha mchezo wa ligi daraja la kwanza kati ya Dodoma FC dhidi ya Alliance uliopigwa mjini Dodoma Jumamosi iliyopita ambapo mwamuzi wa kati alikuwa ni Andrew Shamba ambaye alionekana kuboronga zaidi katika mchezo huo na kuchezesha chini ya kiwango. Kitu ambacho kilistua wengi ni mwamuzi huyo kutoa kadi nne nyekundu kwa timu mmoja (Alliance) Afisa mtendaji mkuu wa Bodi ya Ligi Boniface Wambura amethibitisha: “Katika mechi hiyo, waamuzi wote wanne wamefungiwa miaka mitatu kila mmoja na sababu ya kuwafungia ni kwamba walichezesha mechi chini ya kiwango.” “Ripoti ya kamishna imeonesha hivyo na adhabu yao imezingatia kanuni ya ligi daraja la kwanza inayohusu udhibiti wa waamuzi na ikumbukwe kati ya waamuzi hao wawili ni waamuzi wa ligi kuu Tanzania bara kwa hiyo kamati imeona kwamba kama mwamuzi wa ligi kuu anakwenda kuchezesha mechi ya daraja la kwanza chini ya kiwango kamati ilia...

Arsene Wanger Afungiwa

Picha
Kocha Arsene Wenger atatumikia adhab ya kukosa mechi tatu England KOCHA wa  Arsenal,  Arsene Wenger  amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya Pauni 40,000 kwa kumtolea maneno makali refa kwenye chumba cha kubadilishia nguo baada ya mchezo dhidi ya West Bromwich  Jumapili iliyopita.Wenger alikasirika baada ya refa Mike Dean kuwazawadia The Baggies penalti ya dakika ya mwisho baada ya mpira uliopigwa na Kieran Gibbs kumfikia mkononi Calum Chambers. Alimfuata Dean baada ya mechi na kuanza kumtolea maneno ya kulaumu uamuzi wake baada ya Jay Rodriguez kufunga penalti hiyo kuipatia timu yake sare ya 1-1. Wenger alifunguliwa mashitaka na Chama cha Soka England mapema wiki hii na sasa atakosekana kwenye mechi ya Raundi ya Tatu Kombe la dhidi ya Nottingham Forest Jumapili na mechi ya kwanza ya Nusu Fainali ya Kombe la Ligi , maarufu kama Carabao  dhidi ya Chelsea.

Fahamu Aina 7 Za Juisi Zenye Kuondoa Sumu Mwilini

Picha
Sumu mwilini hutokana na vile vitu au vyakula ambavyo binadamu hutumia huenda kwa kujua au kutokujua. Sumu hizo pia huweza kuchangiwa na matumizi ya yasiyosahihi ya dawa mbalimbali. Miongoni mwa mbinu bora na nzuri ya kuondoasumu hizo ndani ya mwili ni pamoja na kutumia vyakula halisi mara kwa mara. Hapa nanayo orodha ya vinywaji ambavyo huweza kuondoa sumu ndani ya mwili:- 1. Juisi ya mchanaganyiko wa tango na spinachi. 2.Jusi ya mchanganyiko wa tangawizi na spinachi. 3. Juisi ya mchanganyiko wa chungwa na tango. 4. Juisi ya komamanga pamoja na mapera 5. Juisi ya changanyiko wa passion na tango 6. Juisi ya mchanganyiko wa apple na parachichi 7. Juisi ya mchanganyiko wa mbegu za maboga na strawberry

Cervical Cancer Saratani Ya Mlango Wa Kizazi

Picha
Saratani ya mlango wa kizazi  Hii ni njia ya kizazi kati ya uke na mji wa mamba.Ugonjwa huu ukijulikana mapema unweza kutibiwa, wakati wa kufanyiwa uchunguzi wa ubwabwa na fupa nyongo. Nani yumo hatarini Wanawake wengine wamo hatarini mwa kupata saratani ya mlango wa kizazi: Wanawake wasioenda kwa uchunguzi wa kila mwaka wa fupa nyongo na ubwabwa Wanawake walio na “human papillomavirus” HPV au genital warts Kuvuta sigara, kuwa na ukimwi,na kutokula vyakula bora huweza kusababisha saratani ya mlango wa kizazi. Dalili ya saratani ya mlango wa kizazi Hamna dalili zozote mpaka unaposambaa nje ya mlango wa kizazi. Hali hii ikitokea waweza kuwa: Kuvuja damu katikati ya siku za hedhi, unaposhiriki ngono au baada ya hedhi kukatika Kuvuja damu nyingi zaidi ya kawaida. Ukiona dalili hizi pata ushauri wa daktari. Saratani ya Utumbo Mpana na Sehemu za Siri za Nyuma  Saratani ya sehemu za siri za nyuma zipo. Huambukiza sehemu za mmeng’enyo (digestive system...

Wivu wa mapenzi wapelekea kuua familia yake

Picha
Mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina la Ammy Lucas Lukule ambaye ni Mhasibu wa Hospitali ya Rufaa Mbeya, amechukua uamuzi wa kuua familia yake kutokana na wivu wa mapenzi. Akizungumza na mwandishi wa www.eatv.tv Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Benedict Kitalika amethibitisha kutokea kwa tukio hilo la mauaji, na kusema kuwa muuaji alifanya tukio hilo usiku wa jana huko nyumbani kwao Kimara jijini Dar es salaam, na kisha kutokomea kusikojulikana. “Ni kweli mwanaume mmoja ambaye anafanya kazi ya uhasibu katika hospitali ya rufaa ya Mbeya, aliyejulikana kwa jina la Ammy Lucas Lukule, ameua mke, mtoto na shemeji yake, inasemekana kulikuwa na ugomvi ambapo mwanaume alikuwa akimtuhumu mkewe kuwa huyu mtoto mdogo sio wake na anajihusisha na mapenzi na wanaume wengine, hivyo aliamua kuwaua kwa jembe na kukimbia”, amesema Kamanda Kitalika. Kamanda Kitalika ameendelea kwa kueleza kuwa baada ya kufanya tukio hilo marehemu aliacha ujumbe kuwa polisi wasihangaike kwani yeye ndiy...

Mark Zuckerberg ameahidi kufanya marekebisho Facebook

Picha
Mark Zuckerberg ameahidi katika mwaka huu wa 2018 kufanya marekebisho kutokana na makosa mengi yaliyojitokeza katika kutekeleza sheria na kuzuia utumiaji mbaya wa mtandao wa Facebook. Mkurugenzi huyo wa Facebook amekuwa na mpangilio wa kujiwekea malengo binafsi kila mwaka tangu 2009. Zuckerberg amesema hayo kupitia ujumbe aliouandika katika akaunti yake ya mtandao huo. Mtandao wa Facebook umekuwa ukikosolewa vikali kwa kuruhusu matangazo yenye uhusiano na nchi ya Russia wakati wa kinyang’anyiro cha uchaguzi wa Urais Marekani mwaka 2016. Hii ni taarifa yake. Every year I take on a personal challenge to learn something new. I’ve visited every US state, run 365 miles, built an AI for my home, read 25 books, and learned Mandarin. I started doing these challenges in 2009. That first year the economy was in a deep recession and Facebook was not yet profitable. We needed to get serious about making sure Facebook had a sustainable business model. It was a serious year, and I w...

Mohamed Salah ashinda Tuzo ya Mchezaji bora wa Afrika

Picha
Mohamed Salah amempiku mchezaji mwenzake wa Liverpool, Sadio Mane na mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang kutwaa Tuzo ya Mchezaji wa Afrika wa Mwaka 2017. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Misri aliibuka mshindi katika kinyang’anyiro hicho dhidi ya wachezaji wenzake katika mkutano wa Tuzo za Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika mjini Accra. Salah, ambaye ataikosa mechi ya Kombe la FA raundi ya tatu dhidi ya Everton, Ijumaa usiku, amefurahia mwaka wa mafanikio kwa klabu na kwa taifa lake pia. Baada ya kufunga mara 10 akiwa Roma kati ya Januari na Mei, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 aijiunga na Liverpool kwa uhamisho wa rekodi kwa klabu hiyo na kwa haraka ameshafanikiwa kuweka kimiani magoli 24 katika michuano yote. Akiongea kuelekea hafla hiyo, Salah aliwaambia waandishi: “Nadhani tuna timu bora ya taifa na tumefanya vizuri kwenye Kombe la Afrika na kufuzu Kombe la Dunia.” Salah pia alizifumania nyavu mara mbili katika ushindi wa Misri wa...

Mvua yazua taharuki Dodoma

Picha
Watu saba wanahofiwa kufa maji kufuatia mvua kubwa zilizonyesha jana Alhamisi mkoani Dodoma. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge amesema watu hao wamekufa baada ya kuzama katika mashimo ya machimbo, makaro ya vyoo na wengine wawili hawajulikani waliko baada ya kusombwa na maji wakiwa kwenye gari eneo la Kikomho Manispaa ya Dodoma. "Taarifa zote kamanda wetu wa polisi atawaambia lakini ni kweli Kongwa kuna watu wawili wamekufa baada ya kutumbukia kwenye shimo la choo wakiwa msibani ambapo mvua zilinyesha na kulivunja shimo hilo wakatumbukia watu sita wawili walikufa," amesema Mahenge. Wengine ni Ramadhani Haruni mtu mzima aliyekufa ndani ya shimo la machimbo ya dhahabu Nzuguni na Daudi Luwinga (16) mkazi wa Nzuguni pia ambaye alitumbukia kwenye shimo la kujenga choo wakati akitoka kwenye mchezo wa mpira. Katika kijiji cha Kikombo gari Toyota Mitsubishi lilisombwa na maji usiku wa kuamkia leo Ijumaa ambapo lilikuwa na dereva na abiria mmoja na wote hawajapatikana. ...

Ronaldo De Lima awafungukia Cristiano na Messi

Picha
Nyota wa zamani wa Real Madrid, Barcelona na timu ya taifa ya Brazil Ronaldo Luís Nazário de Lima amesema Cristiano Ronaldo na Lionel Messi wamefanikiwa kutwaa tuzo za mchezaji bora mara nyingi kutokana na kukosa ushindani. Ronaldo ambaye ni mshindi mara tatu wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa FIFA, amesema anaheshimu mafanikio ya nyota hao wawili lakini ukweli ni kwamba wameyapata kwasababu hakuna watu wengine wa kushindana nao tofauti na zamani ambapo vipaji vilikuwa vingi. ''Cristiano na Messi wamefanya vizuri kwa muda mrefu lakini suala la kuwa wachezaji bora katika kizazi chao limekuwa rahisi aidi kutokana na kukosekana kwa watu wa kushindana nao tofuati na zamani ambapo vipaji vilikuwa vingi'', amesema Ronaldo de Lima. Ronaldo ameengeza kuwa wakati yeye anakuwa mchezaji bora kulikuwa na ushindani mkubwa kuliko sasa. ''Wakati mimi natwa tuzo ya mchezaji bora mara tatu kulikuwa na vipaji vikubwa kama Zinedine Zidane, Rivaldo, Lus Figo pamoja na Ronaldi...

Hali ya Kingunge Yaimalika

Picha
 Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imesema hali ya mwanasiasa mkongwe nchini Kingunge Ngombale Mwiru, inaendelea kuimarika baada ya kuanza kupata matibabu. Akizungumza na Mwananchi leo Ijumaa hospitalini hapo, Ofisa Uhusiano wa MNH, Neema Ngomuo amesema kwa sasa afya yake imeimarika. "Anaendelea vizuri na afya yake imetengamaa, bado yupo chini ya uangalizi wa karibu wa madaktari, baada ya upasuaji aliofanyiwa," amesema Ngomuo. Taarifa za awali zimeeleza kuwa Rais mstaafu, Jakaya Kikwete jana Alhamisi jioni alifika hospitalini hapo kwa ajili ya kumjulia hali mwanasiasa huyo. Kingunge aliyelazwa katika wodi ya Mwaisela, alifiwa na mke wake Pares Mwiru jana Alhamisi saa nane mchana katika wodi ya Sewahaji alikokuwa amelazwa. Neema amesema mke wa mwanasiasa huyo alifikishwa Muhimbili tangu Oktoba 3, mwaka jana. Wakati Peras akifariki,  mumewe Kingunge anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali hiyo. Awali mtoto wa Kingunge, Kinje Mwiru alisema kifo cha mama yake kimeto...

Dr SHEIN Ataka Muungano Ufanyike Z'nzibar pia

Picha
Zanzibar. Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein ametaka jambo linalohusu Muungano linalofanyika Tanzania Bara , lifanyike pia na visiwani humo bila ubaguzi wowote . Dk Shein ametoa kauli hiyo jana katika ufunguzi wa jengo jipya la Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ( SMZ ) liliopo Mazizini nje kidogo ya mji wa Zanzibar. Huku akitolea mfano jengo hilo alisema , “ Kukamilika kwa jengo hili ambalo linafanana na lile la Dodoma ni ishara mojawapo ya kuwa ipo haja kwa kila jambo la muungano linalofanyika Tanzania Bara na Zanzibar linapaswa kufanyika pia ili kutoufanya upande mmoja kujiona kama umetengwa . Si busara kwa mambo ya muungano kufanywa upande mmoja tu au upande mmoja kuonekana unajivutia wenyewe kila kitu , hali hiyo inaweza kuleta madhara makubwa katika utendaji wa masuala ya muungano .” Alisema watendaji wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,...

Wezi Wa Pesa Za Escrow Watajwa na Rugemarila

Picha
Leo January 5, 2017 Mfanyabiashara James Rugemarila anayekabiliwa na kesi ya utakatishaji fedha amewataja wezi wa fedha za Escrow katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kama alivyodai awali kuwa atawataja . Wezi hao amewataja mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu , Thomas Simba baada ya Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Leornad Swai kueleza upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, hivyo anaomba iahirishwe hadi tarehe nyingine. “Mwizi ni Standard Chartered Tanzania Ltd na Standard Chartered Hong Kong ambao wameisababishia serikali hasara ya Trilioni 37, pia nimewapelekea TAKUKURU washiriki wengine wa fedha hizo, hivyo ninaomba niendelee kuwa hai ili nije kuwa shahidi mzuri wa upande wa mashtaka kuhusu wezi hao.” – James Rugemarila Pia Rugemarila amedai kuwa wezi hao ndio wamemuibia hata kwenye kampuni anayoisimamia ya VIP ambayo inawadai Trillion 16. Wakili Swai alidai kuwa ni kweli Rugemarila aliwasilisha taarifa ofisini kwao na wanazifanyia kaz...

Madiwani Wengine Waikimbia Chadema

Picha
Madiwani wawili kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zakayo Chacha Wangwe wa kata ya Turwa wilaya Tarime, na mwenzake wa Kata ya Mwangata Manispaa ya Iringa Mjini, Angelusi Mbogo wametangaza kujivua uanachama wa Chama hicho kwa kile kilichoelezwa kuwa kimepoteza imani yao kwa wananchi huku pia kikiendeshwa kibabe hivyo wameamua kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) ili kuunga mkono juhudi za Rais John Magufuli katika kuleta maendeleo na vita dhidi ya ufisadi.

Hofu ya Kenya ' Sport Pesa , Yawapa Hofu SIMBA ' YANGA YATOA AHADI

Picha
Hofu ya Simba na Yanga kwamba wanaweza kumkosa mdhamini sasa imetoewa . Maan Kampuni ya kubashiri michezo ya kubahatisha ya SportPesa Tanzania imezitoa hofu klabu za Simba , Yanga na Singida United ya kuendelea kuzidhamini kama kawaida . Hiyo , ikiwa ni moja tangu kampuni hiyo kusitisha udhamini wake kutokana na uamuzi wa serikali ya Kenya kuongeza ushuru . Klabu ambazo SportPesa inazidhamini za kutoka Kenya ni Gor Mahia , AFC Leopards na Nakuru All Stars pamoja na Ligi ya Super 8. Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa , Abbas Tarimba alisema kilichokea Kenya cha kusitisha mkataba wa kuendelea kuzidhamini klabu , hausiki kwa Simba , Yanga na Singida United. Tarimba alisema, wao SportPesa wamepanga kuendelea na udhamini wa klabu hizo za hapa nchini tena kwa kuzidi kuziboresha zaidi siku za baadaye ili kuhakikisha klabu hizo zinapata mafanikio. Aliongeza kuwa, tofauti na udhamini wa klabu hizo, pia wamepan...

Arsenal Wakata Tamaa

Picha
Usiku wa jana kwa mara nyingine tena mzimu wa penati unaendelea kumtesa golikipa wa Arsenal Petre Cech , wengi walitarajia Hazard angefunga tuta lile labda kama angepiga nje ya lango la Arsenal. Ni penati ya 15 kwa Cech tangu ajiunge na klabu ya Arsenal akitokea Chelsea, lakini huwezi amini kwamba pamoja na ubora wake wote alionao mlinda lango huyo lakimi hajawahi kuokoa penati hata moja akiwa na Arsenal. Mbaya zaidi ni kwamba kati ya mikwaju ya penati 15 iliyopigwa kuelekea lango lake, mikwaju 3 tu ndio aliweza kuifuata huku mikwaju 12 ya penati aliruka upande ambao mpira haukwenda. Tayari hoja kuhusu uwezo wa golikipa huyo kwenye suala la penati imekuwa kubwa kiasi cha kumfanya mlinda lango wa zamani wa Arsenal David Seaman kuwaomba mashabiki wa Gunnerz kuwa watulivu. Seaman ametoa ushauri kwa Cech kwamba kama anataka ushauri kutoka kwake baasi anaweza kumpigia simu wakati wowote na anaweza kumpa ushauri kuhusu mbinu za kuokoa penati....

Nini Tutarajie Tuzo Mchezaji Bora

Mohamed Salah , Pierre Aubameyang na Sadio Mane wanatoana jasho kuwania tuzo ya mchezaji bora wa bara la Afrika ambapo tuzo hizo hutolewa kila mwaka na mwaka huu zinatolewa mjini Accra. Salah aanapewa nafasi kubwa sana kutwaa tuzo ya mchezaji bora Afrika mwaka huu , hii iko wazi kutokana na kiwango kikubwa sana anachokionesha msimu huu na Liverpool ambapo ndio anaongoza kwa ufungaji EPL. Salah anaonekana kuibeba Liverpool mabegani mwake sawa na alivyowabeba Wamisri na kuwapeleka fainali za kombe la dunia mwakani na ni wazi kwamba sio Mane wala Aubameyang anayekaribia mafanikio yake msimu huu . Dua za raia wa Senegal zitakuwa mbaya kwa Salaah kwani wana kiu sana ya kutwaa tuzo hiyo ambayo tangu  El Hadji Diouf atwae tuzo hiyo mwaka 2002 haijawahi kufika tena Senegal na Mane ndio anategemewa kuipeleka Senegal. Tayari Piere Aubameyang ameshatwaa tuzo hiyo mwaka juzi lakin...

YANGA yazidi Endeleza Ubabe Mapinduzi Cup

Picha
BAO la dakika ya 90 la beki Hassan Ramadhani Kessy limeipa ushindi wa 1-0 Yanga SC dhidi ya JKU katika mchezo wa Kundi B Kombe la Mapinduzi jioni ya leo Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Sifa zimuendee mwenyewe Kessy kwa bao hilo, kwani aliingia na mpira ndani kwa kasi kutokea pembeni akampasia Pius Buswita aliyemsogezea mbele beki huyo kwa pasi ya kisigino akaikuta na kufunga. Kwa ushindi huo mwembamba, Yanga SC inafikisha pointi sita baada ya mechi mbili, ikiwemo ya kwanza waliyoshinda 2-1 dhidi ya Mlandege juzi.   Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Nassor Salum aliyesaidiwa na Iddi Khamis na Mussa Hemed ndani ya dakika 45 za kipindi cha kwanza timu zote zilifanya mabadiliko. JKU walianza kumtoa Ali Omar na kumuingiza Said Zege dakika ya 38, kabla ya Yanga kumpumzisha mshambuliaji Matheo Anthony na kumuingiza Yohanna Oscar Nkomola. Katika kipindi hicho ilishuhudiwa JKU wakitawala mchezo na kupeleka mashambulizi mengi langoni mwa Yanga, lakini hayakuwa na madhara. Kwa Yan...

Trump Afunguka Kuhusu Marekani

Picha
Rais wa Marekani, Donald Trump leo ameuthibitishia ulimwengu kuwa hata Marekani inamiliki silaha za Nyuklia ingawaje imekuwa mstari wa mbele kupiga vita utengenezwaji wa silaha hizo kwa mataifa mengine duniani. Haya yamethibishwa na Rais Donald Trump baada ya kumjibu Rais wa Korea Kaskazini, Kim Jung Un kwa kauli yake aliyoitoa wiki iliyopita akioonya Marekani kuwa kitufe cha kuwashia makombora yake kipo kwenye kitanda chake akimaanisha kuwa muda wowote anaweza kuilipua Marekani. Trump naye kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema kuwa hata yeye ana kitufe cha kuwashia makombora ya silaha za nyuklia na kumuonya kwa kumwambia kuwa silaha zake ni kubwa kuliko za Korea Kaskazini. Rais huyo ambaye haishiwi vituko ameongeza kwa kusema kuwa Rais Kim amekuwa mbwatukaji wa kutoa vitisho kila siku lakini hakuna chochote na kumuonya kwamba yeye kitufe chake kinafanya kazi. “Kiongozi wa Korea Kaskazini ameanza kuongea tena “nina kitufe cha nyuklia kwenye meza yangu” kama siku ...

Moshi kubomolewa majengo ya Biashara

Picha
Maofisa mipango miji na askari wa Manispaa ya Moshi wameanza kusimamia ubomoaji wa majengo ya biashara yaliyojengwa na kukarabatiwa kinyume cha sheria. Ujenzi huo uliofanywa chapuchapu kati ya Desemba 23 na Desemba 26,2017 katika kata za Kiusa, Bondeni na Mawenzi, ulifichuliwa na gazeti la Mwananchi na kusababisha madiwani kupaza sauti wakitaka majengo hayo yavunjwe. Kwa mujibu wa sheria za mipango miji na mpango kabambe wa mji wa Moshi, inakatazwa kukarabati majengo ya zamani au kujenga mapya ambayo si ya ghorofa katika kata hizo. Leo Jumatano Januari 3,2018 kuanzia saa tatu asubuhi, maofisa mipango miji na askari wa mji walifika katika moja ya nyumba hizo iliyojengwa upya bila vibali vya halmashauri wakiwataka wabomoe au manispaa ibomoe. Baada ya mazungumzo, wamiliki wa jengo hilo lililopo barabara ya Sokoni karibu na hosteli ya Umoja waliokataa kuzungumza na wanahabari walikubali kubomoa wakianzia kuondoa mabati. Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango Miji ya Halmashauri ya Manispaa y...

Waliovalia Sare za Magereza Wavamia Baa na kujeruhi wateja

Picha
Mkuu wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Dar es Salaam, Agustine Mboje   Watu zaidi ya 10 wakiwemo waliovaa sare za askari Magereza walivamia baa moja iliyopo Keko jijini hapa jana , kujeruhi watu huku wakipora mali mbalimbali zikiwamo simu za mkononi na fedha za wateja . Watu hao walivamia baa hiyo iitwayo Omax saa tano usiku na kuanza kuwapiga na kuwapora mali hizo wateja kisha kutokomea gizani. Awali, kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Emmanuel Lukula alisema alipopigiwa simu na mwandishi wa habari hizi, alisema yuko Kibiti kikazi. Hata hivyo alikiri kupigiwa simu usiku wa siku ya tukio na watu wakitaka kupatiwa fomu za PF3 kwa ajili ya matibabu. “Nilipigiwa simu na watu wengi wakitaka kupatiwa PF3 wameumia, nikawaambia niko mbali waende tu Kituo cha Polisi Chang’ombe watasaidiwa, sasa sijui walienda ama vipi na sasa hivi siwezi kutoa ufafanuzi kwa sababu niko Kibiti kikazi,” alisema. Mkuu wa Jeshi la Magereza Mkoa wa D...

Walim Watimuliwa Sababu Utoro

Picha
Walimu tisa wa shule za msingi wilayani Bahi wamefukuzwa kazi kutokana na utoro huku wanafunzi sita wakishindwa kumaliza elimu ya msingi kutokana na mimba. Ofisa elimu na taaluma wilayani humo, Issa Nchila ametoa taarifa hiyo leo Jumatano kwenye kikao cha wadau wa elimu waliokutana kujadili changamoto zinazosababisha wilaya hiyo kuendelea kushuka kielimu. Nchila amesema walimu hao walikuwa miongoni mwa walimu 11 waliokuwa wameshtakiwa kwa makosa mbalimbali ya utoro na nidhamu kazini. Amesema walimu wawili kati ya hao, walishushwa vyeo ikiwemo kupunguziwa mishahara yao. Ofisa huyo amekiri hali mbaya kwa matokeo ya elimu huku wilaya ikiwa imeshika nafasi ya tano katika halmashauri 8 za Mkoa wa Dodoma. "Bado tutaendelea kuwachukulia hatua kali kwa kushirikiana na TSD ili kukomesha vitendo hivyo kwani ni moja ya mambo yanayotukwamisha na kufanya watoto wetu wafanye vibaya," amesema Nchila. Amesema bado wilaya inakabiliwa na mdondoko mkubwa wa elimu kwani wanafunzi walioandi...

SERIKALI yasema Haina Mpango wa Kuchoma Moto wala kuuza,

Dar es Salaam. Wakati China ikipiga marufuku biashara ya meno ya tembo , Serikali imesema haina mpango wa kuuza wala kuteketeza meno iliyonayo . Kabla ya kuukaribisha mwaka mpya , Desemba 31, 2017, Waziri wa Misitu wa China, Zhang Jianlong alitangaza marufuku ya kuingiza nchini humo meno hayo kwa wafanyabiashara wote . Kutokana na msimamo huo uliosubiriwa kwa muda mrefu, katibu mkuu wa Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi alisema uamuzi huo utasaidia kupambana na ujangili nchini na Afrika kwa ujumla. Kwa kutambua uwepo wa zaidi ya tani 118 za meno hayo nchini ambayo wakati fulani wadau waliishauri Serikali ama kuyauza au kuyateketeza, katibu mkuu huyo alisema yataendelea kutunzwa. “Mpango wa kuyauza meno hayo kwa sasa haupo. Na hatutayateketeza, tutaendelea kuyatunza,” alisema meja jenerali huyo. Kwa mujibu wa makubaliano yaliyoridhiwa mwaka 1975 na mataifa mbalimbali duniani chini ya mkataba unaopiga marufuku biashara y...

TFF Yapewa Maagizo Mazito

Picha
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ameitaka TFF kuyafanyia kazi malalamiko yote yanayohusu michezo ya ligi daraja la kwanza, kati ya Dodoma FC vs Alliance na Pamba vs Biashara. Sakata la maamuzi yasiyo ya haki katika michezo ya Dodoma FC dhidi Alliance ya Mwanza na Pamba ya Mwanza dhidi Biashara ya Musoma ndio limefanya Waziri mwenye dhamana ya michezo kutoa agizo hilo kwa shirikisho ili kuhakikisha utata huo unamalizika. Katika taarifa yake  Waziri Mwakyembe ameeleza kusikitishwa na malalamiko ya vitendo vya uonevu na upendeleo katika maamuzi ya mechi hizo huku TFF ikiwa kimya bila kutoa ufafanuzi wa maamuzi hayo. Mechi hizo zilipigwa Disemba 30 maamuzi yake kugubikwa na utata mkubwa hivyo Waziri amemtaka Rais wa TFF Wallace Karia na viongozi wengine wahusika kuchukua hatua za kuchunguza maamuzi hayo na kuchukua hatua

MKUTANO WA FIFA KUFANYIKA TANZANIA, RAIS WA CAF KUTUA DAR

Picha
Tanzania inataraji kuwa wenyeji wa mkutano mkubwa wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani FIFA (Fifa Summit) utakaofanyika February 22, 2018 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere. Mkutano huo mkubwa wa pili unaofanyika kwa mara ya kwanza Tanzania unashirikisha nchi 19 Wanachama wa Fifa. Mkutano huo utakaoongozwa na Rais wa FIFA Gian Infantino pia utahudhuriwa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Africa (CAF) Ahmad Ahmad, Makamu wa Rais wa Fifa,Katibu mkuu wa Fifa na viongozi mbalimbali wa FIFA na CAF ikiwemo wajumbe wa kamati ya utendaji. Wageni kutoka nchi mbalimbali duniani watakaohudhuria mkutano huo wataanza kuwasili Tanzania Februari 20, 2018 Ajenda za mkutano huo mkubwa wa Fifa ni miradi mbalimbali ya Fifa zamani ikifahamika kama Goal Project na sasa ikifahamika Fifa Forward Programme,ajenda ya soka la vijana,Wanawake na klabu wakati ajenda nyingine ya mkutano huo ni kujadili kalenda ya kimataifa ya Fifa,kuboresha masuala ya uhamisho na vipaumbele vyak...

Kuwa Tajiri kwa Mtaji wa Laki 3 tu, Kupitia Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji

Picha
LEO TUANGALIE MCHANGANUO WA TSHS 300,000/= (LAKI TATU) KWA KUANZISHA MRADI WA UFUGAJI KUKU WA KIENYEJI. Hapa tuta hitaji kuku 11 tu wakubwa wanao taga yani majike 10 na Jogoo 1 tu. Kwa kutumia kuku hao 11 baada ya miezi mitatu unaweza ukawa na kuku mia Tatu 300 au na zaidi kama unataka. Nunua kuku wako katika chanzo cha kuaminika kuepuka magonjwa usinunue kuku sehemu za masokoni au kwenye mabanda ya njiani au kuku wanao safirishwa kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine. Unapo nunua kuku wakubwa kwanza unapo wafikisha wape chanjo ya mdondo (Newcastle vaccine) ili kuweka rekodi yako ya chanjo maana chanjo hii hurudiwa kila baada ya miezi 3. Ukumbuke tarehe uliyo wachanja na tarehe utakayo wachanja tena baadae. Usinunue kuku kabla hujaandaa banda na Chakula. Katika sh. 300000 toa sh.69500 ambayo utanunua Chakula cha kuku, kuku hawa hawana formula ya Chakula hivyo unaweza kununua material ukachanganya Chakula mwenyewe ampapo utaokoa pesa nyingi pia. Mchanganuo Wa 69500 ni:- Pumba gunia ...

Simba kupata nguvu mpya kwenye eneo la ulinzi

Picha
Klabu ya Simba SC ambao ni vinara wa ligi kuu soka Tanzania Bara leo inatarajia kupata nguvu mpya kwenye eneo lake la ulinzi kwa kuanza kuwatumia mabeki wake Shomari Kapombe na Asante Kwasi. Simba SC huenda ikaanza kuwatumia nyota hao leo kwenye mchezo wake wa kwanza wa michuano ya Kombe la Mapinduzi Visiwani Zanzibar itakapocheza na timu ya Mwenge. Kapombe na Kwasi jana wamefanya mazoezi ya mwisho hivyo kocha wa timu hiyto Juma Masoud, anaweza kuamua kuwaanzisha. Kapombe alikuwa majeruhi kwa muda mrefu tangu asajiliwe kutoka Azam FC hajaitumikia Simba kwenye michezo ya ligi. Simba SC kupitia ukurasa wake wa Instagram imethibitisha kuwa wachezaji hao wapo tayari kwaajili ya michuano hiyo. Asante Kwasi ambaye ni raia wa Ghana amesajiliwa katika dirisha dogo lililomalizika hivi karibuni. Klabu hiyo ya Msimbazi  itaanza rasmi michuano ya Mapinduzi Cup leo  dhidi ya Mwenge. Mchezo huo utapigwa saa 10:30 jioni kwenye uwanja wa Amaan.

Rais wa Iran: Trump ni adui wa Iran

Picha
Rais Rouhan wa Iran Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema rais wa Marekani ni adui mkuu wa taifa hilo kuanzia utosini hadi kwenye unyayo. Ameyasema hayo akijibu ujumbe wa rais Trump alioutoa kupitia ukurasa wake wa twitter. Katika ujumbe wake rais Trump amesema kuwa waandamanaji wa Iran wanadai haki yao ambayo wamekuwa wakipigania kwa miaka mingi kuhusiana na njaa na kukosekana kwa uhuru wao. Picha za video zimeonyesha waandamanaji wakikabiliana na Polisi katika maandmano yaliyoanza tangu siku ya alhamis na ambayo yanaendelea katika kusambaa katika miji mingine nchini humo. Polisi mmoja ameuawa na waandamanaji hao ambao baadhi yao wanajihami kwa bunduki aina ya rifle na hivyo kufanya idadi ya watu 13 kuuawa hadi sasa.

Mjerumani auawa kwa kuchomwa kisu

Picha
RAIA wa Ujerumani Gerd Winkdl (60), amefariki dunia Zanzibar akidaiwa kuchomwa kisu na marafiki zake wa kike kutokana na wivu wa kimapenzi huku wanawake wanne wakishikiliwa na Jeshi la Polisi kuhusiana na kifo hicho. Tukio hilo lilitokea usiku wa mkesha wa Mwaka Mpya Shangani Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja. Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Hassan Nassir Ali, akizungumza na Nipashe kisiwani hapa jana, alisema tukio hilo lilitokea majira ya saa 9:30 usiku baada ya kusherehekea Mwaka Mpya wa 2018 akiwa na marafiki zake hao. Alisema kabla ya kukutwa na umauti, Winkdl akiwa na marafiki zake wanne ambao wanadaiwa kuwa na uhusiano naye wa kimapenzi, waligombana na baadaye ugomvi huo kusababisha kuchomwa kisu katika sehemu mbalimbali za mwili wake. Kamanda Ali alisema watuhumiwa hao wanne ambao wote ni wanawake, raia wa Tanzania na Jeshi la Polisi linaendelea kuwashikiliwa kwa ajili ya kuwahoji na kukamilisha taratibu za kiuchunguzi. "Inasemekana wote walikuwa wameshalewa na inadaiwa...

California yahalalisha matumizi ya Bangi

Picha
California limekuwa jimbo kubwa zaidi nchini Marekani kuhalalisha matumizi ya bangi kwa burudani. Kuanzia sasa Januari mosi mwaka 2018 watu walio na umri wa kuanzia miaka 21, wanaweza kumiliki hadi gramu 28 za bangi na kupanda hadi miti 6 ya bangi nyumbani. Wanaopinga wanasema kuwa sheria hiyo itasababisha watu kuendesha magari wakiwa tayari wamevuta bangi kuchangia vijana kuvuta bangi. Lakini biashara zinatabiri kile kinaonekana kuwa sekta ya mabilioni ya dola miaka michache inayokuja. Wakaazi wa Califonria walipigaa kura kuunga mkono kipengee cha kuhalalisha bangi miaka 14 iliyopita katika kura ambayo ilifanyika sambamba na uchaguzi wa rais nchini humo. Tangu wakati huo sheria ngumu zinazohusu kodi zimeandikwa kudhibiti mauzo ya bangi. Biashara zinatabiri kile kinaonekana kuwa sekta ya mabilioni ya dola miaka michache inayokuja. Mkurugenzi mkuu wa kampuni ambayo inafuatilia soko la bangi duniani alitabiri kuwa kutakuwa na kushuka kwa bei kwa mwaka wa kwanza au miaka miwili. ...

VIGOGO WAPONZWA NA CHAPA

Picha
o VIGOGO kadhaa wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi wameponzwa na zoezi la upigaji chapa mifugo nchi nzima, baada ya kuvuliwa nyadhifa zao. Uamuzi wa kuwawajibisha vigogo hao umefanywa na waziri wa wizara hiyo, Luhaga Mpina, huku akiongeza muda wa mwezi mmoja zoezi la upigaji chapa mifugo kitaifa. Waliovuliwa nyadhifa ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Ugani wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dk. Erastus Mosha na Kaimu Mkurugenzi wa Ugani na Usajili, Bezia Rwengozibwa kwa kushindwa kusimamia kikamilifu zoezi hilo kwa mujibu wa Sheria ya Utambuzi, Usajili na Ufuatiliaji wa Mifugo na 12 ya mwaka 2010 na Kanuni zake za Mwaka 2011 GN 362. Mbali na wakurugenzi hao, pia maofisa wawili wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Luzangi Deogratius na Felista Kimario ambao wamepewa onyo kali kwa kushindwa kusimamia zoezi hilo huku waliovuliwa madaraka akiagiza wachukuliwe hatua kali za kinidhamu. Akizungumza jana katika zoezi la kuhitimisha upigaji chapa kitaifa katika Kata ya Migato Wilaya ya Itil...

HAJI APATA MKATABA KENYA

Picha
Beki wa kushoto wa Yanga, Mwinyi Haji. IMEBAINIKA kwamba uongozi wa timu ya AFC Leopards ya Kenya umemalizana na beki wa kushoto wa Yanga, Mwinyi Haji na umempa mkataba wa miaka miwili huku kinachosubiriwa kwa sasa ni beki huyo kupewa ruhusa na timu yake kabla ya kujiunga na timu hiyo ambayo inashiriki ligi ya Kenya. AFC Leopards inayonolewa na Mtanzania, Dennis Kitambi, imefikia uamuzi huo wa kumpa mkataba beki huyo baada ya kukoshwa na uwezo wake aliouonyesha wakati akiwa na timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes wakati ilipokuwa inashiriki michuano ya Chalenji iliyofikia tamati hivi karibuni. Chanzo cha karibu na beki huyo kimeliambia Championi Jumatatu kuwa Wakenya hao walishamalizana na Mwinyi ambapo kwa sasa kinachosubiriwa ni Yanga kumpa ruhusa beki huyo baada ya hivi karibuni kuandika barua ya kutaka kuondoka kutokana na kukosa namba ndani ya kikosi cha kwanza. “AFC Leopards wamefanya kweli baada ya kuonesha nia ya dhati tangu walipovutiwa na Mwinyi wakati akiwa ...

KOCHA WA YANGA Akubali Mbao FC iliwazidi Uwezo

Picha
go Kocha msaidizi wa Yanga Shadrack Nsajigwa amekubali kuwa timu yake ilizidiwa na Mbao na kujikuta ikiruhusu magoli mawili ndani ya kipindi cha pili , mlinzi huyo wa zamani wa kulia wa Yanga na Taifa Stars amesema kipindi cha pili Mbao walibadilika na kutumia nafasi walizozitengeneza kupata magoli . Nsajigwa amekubali kuwa Mbao walistahili kushinda mchezo huo baada ya kufanya kazi yao vizuri uwanjani . “ Hali ya mchezo kwa ujumla ilikuwa nzuri kiasi chake , kipindi cha kwanza mechi ilikuwa nusu kwa nusu lakini kipindi cha pili kilibadilika , Mbao walibadilika wakaja juu badae wakapata nafasi wakazitumia . Mpira ni mchezo wa matokeo , usipobadili nafasi ulizopata kuwa magoli basi huezi kufunga ”- Shadrack Nsanjgwa . “ Tumepoteza mchezo tunawapa hongera Mbao wamefanya kazi yao vizuri wamepata ushindi .” Nsajigwa akishirikiana na benchi la ufundi la Yanga ...