TAARIFA MPYA

Madhara ya Chai na Kahawa Kiafya

Picha
CAFFEINA/KAFEINA. Kafeina ni nini?: 1. Kafeina ni madawa ya kulevya kundi la ‘Stimulants drugs’. Utashangaa. Habari ndiyo hiyo. Hii ndiyo sababu kwa mtu aliyezoea kunywa chai hii kila siku au kahawa, siku asipokunywa kichwa humuuma, ni kwa sababu amekuwa mtegemezi au teja wa kafeina. Kafeina ni kiungo mhimu karibu katika soda zote zenye rangi nyeusi; Coca-cola, Pepsi, Sayona nyeusi, Azam cola na kadharika. Kafeina huongezwa pia katika Red bull, Malta na katika baadhi ya dawa za kupunguza maumivu mwilini. Kwahiyo Kafeina ambayo hupatikana katika chai na kahawa ni aina mojawapo ya madawa ya kulevya. 2. Kafeina ni kikojoshi (diuretics). Kafeina ni dawa ya kukufanya ukojowe. Ukinywa kikombe kimoja cha kinywaji chenye kafeina yaani chai au kahawa, basi muda si mrefu utaenda kukojoa vikombe viwili. Kwa sababu kafeina ni taka isiyotakiwa mwilini, mwili utafanya kila uwezalo ikibidi ujikamuwe wenyewe kupata maji ya ziada kuweza kuitoa kafeina hii uliyoinywa kwa kisingizio ch...

Waliovalia Sare za Magereza Wavamia Baa na kujeruhi wateja

Mkuu wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Dar es Salaam, Agustine Mboje 

Watu zaidi ya 10 wakiwemo waliovaa sare za askari Magereza walivamia baa moja iliyopo Keko jijini hapa jana, kujeruhi watu huku wakipora mali mbalimbali zikiwamo simu za mkononi na fedha za wateja.

Watu hao walivamia baa hiyo iitwayo Omax saa tano usiku na kuanza kuwapiga na kuwapora mali hizo wateja kisha kutokomea gizani.

Awali, kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Emmanuel Lukula alisema alipopigiwa simu na mwandishi wa habari hizi, alisema yuko Kibiti kikazi. Hata hivyo alikiri kupigiwa simu usiku wa siku ya tukio na watu wakitaka kupatiwa fomu za PF3 kwa ajili ya matibabu. “Nilipigiwa simu na watu wengi wakitaka kupatiwa PF3 wameumia, nikawaambia niko mbali waende tu Kituo cha Polisi Chang’ombe watasaidiwa, sasa sijui walienda ama vipi na sasa hivi siwezi kutoa ufafanuzi kwa sababu niko Kibiti kikazi,” alisema.

Mkuu wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Dar es Salaam, Agustine Mboje alisema taarifa ya kuvamiwa kwa baa na watu kupigwa hana, lakini anachofahamu kuna askari wao alivamiwa na vibaka na kupigwa wakati akienda kazini, kisha wakatoa taarifa Kituo cha Polisi Chang’ombe.

Mboje alisema baada kutoa taarifa, polisi wakishirikiana na askari Magereza walifanya msako kuwatafuta na kuwakamata baadhi ya vibaka ambao waliwafikisha katika kituo hicho.

Mhudumu wa baa iliyovamiwa aliyejitambulisha kwa jina moja la Mary alisema walifika watu zaidi ya 10 wakiwa wameshika mikanda wakaanza kuwapiga watu, lakini alipoona hivyo alikimbilia chooni akiwa na mteja ambako walifuatwa na kuanza kupigwa.

Alieli Nelson aliyekuwa mteja ambaye alijeruhiwa kichwani, alisema walikuwa kwenye baa hiyo wakisubiri chakula na ghafla walivamiwa na kundi la watu wakiwa wamevalia sare za askari Magereza na wengine wakiwa wamevaa kiraia.

“Hapa nilipo nimepigwa vibaya, nimepasuliwa kichwa, nimeibiwa simu yangu pamoja na pesa Sh500,000 huku wakitutisha kwamba atakayeshtaki atafunguliwa kesi,” alisema Alieli.

George Cosmas alisema alivamiwa na kupigwa, lakini alishuhudia mmoja wa wateja wenzake akiumizwa mkono na kuporwa.

“Wamewapiga watu sana na kuwaibia vitu mbalimbali vikiwamo pesa na simu, pia kuna watu ambao ni raia wa Kongo wamepigwa na mmoja kuvunjwa mkono” alisema.

Akizungumzia tukio hilo, mmiliki wa baa hiyo, Gerald Temba alisema wakati wa tukio hakuwepo lakini alipigiwa simu akielezwa walikuwepo watu wavamizi wakiwemo waliovalia sare za Magereza waliokuwa wanapiga watu na kupora vitu.

Alisema baada ya kupewa taarifa alimpigia simu Kamanda Lukula kumfahamisha juu ya tukio hilo na kujibiwa kuwa taarifa zimeshamfikia. “Nilimpigia RPC wa Temeke kumfahamisha kwa nini tunavamiwa na kupigwa wakati leo ni sikukuu na muda wa kufunga ni saa sita, lakini alinijibu anayo hiyo taarifa,” alisema Temba.

Aliongeza kuwa katika tukio hilo alipata hasara ikiwemo viti, meza na chupa kuvunjika pamoja na wateja waliokuwemo kuondoka bila kulipa bili za vinywaji na chakula zinazofikia Sh300,000.

Maoni

ZILIZO SOMWA MARA NYINGI

ULAJI WA MARA KWA MARA WA MBEGU ZA MABOGA HUKUKINGA NA KUKUEPUSHA NA MAGONJWA 1O MWILINI MWAKO...

Dalili 6 zitakazokuonyesha kuwa mwenzi wako ana mtu mwingine katika mahusiano

FAIDA YA JUICE YA KAROTI KATIKA MWILI WA BINADAM

DAWA BORA YA NGUVU ZA KIUME NA MAUMBILE MADOGO

AINA ZA MBOLEA & MATUMIZI YAKE KITAALAM

Madhara ya Chai na Kahawa Kiafya

Fahamu Aina 7 Za Juisi Zenye Kuondoa Sumu Mwilini

Ugonjwa wa Chango La Uzazi

Madhara Ya Kuangalia Video za Porno {Ngono} na Namna ya Kujizuia

Athari za kiafya za vyakula vyenye Wanga