TAARIFA MPYA

Madhara ya Chai na Kahawa Kiafya

Picha
CAFFEINA/KAFEINA. Kafeina ni nini?: 1. Kafeina ni madawa ya kulevya kundi la ‘Stimulants drugs’. Utashangaa. Habari ndiyo hiyo. Hii ndiyo sababu kwa mtu aliyezoea kunywa chai hii kila siku au kahawa, siku asipokunywa kichwa humuuma, ni kwa sababu amekuwa mtegemezi au teja wa kafeina. Kafeina ni kiungo mhimu karibu katika soda zote zenye rangi nyeusi; Coca-cola, Pepsi, Sayona nyeusi, Azam cola na kadharika. Kafeina huongezwa pia katika Red bull, Malta na katika baadhi ya dawa za kupunguza maumivu mwilini. Kwahiyo Kafeina ambayo hupatikana katika chai na kahawa ni aina mojawapo ya madawa ya kulevya. 2. Kafeina ni kikojoshi (diuretics). Kafeina ni dawa ya kukufanya ukojowe. Ukinywa kikombe kimoja cha kinywaji chenye kafeina yaani chai au kahawa, basi muda si mrefu utaenda kukojoa vikombe viwili. Kwa sababu kafeina ni taka isiyotakiwa mwilini, mwili utafanya kila uwezalo ikibidi ujikamuwe wenyewe kupata maji ya ziada kuweza kuitoa kafeina hii uliyoinywa kwa kisingizio ch...

Mjerumani auawa kwa kuchomwa kisu

RAIA wa Ujerumani Gerd Winkdl (60), amefariki dunia Zanzibar akidaiwa kuchomwa kisu na marafiki zake wa kike kutokana na wivu wa kimapenzi huku wanawake wanne wakishikiliwa na Jeshi la Polisi kuhusiana na kifo hicho.

Tukio hilo lilitokea usiku wa mkesha wa Mwaka Mpya Shangani Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja.

Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Hassan Nassir Ali, akizungumza na Nipashe kisiwani hapa jana, alisema tukio hilo lilitokea majira ya saa 9:30 usiku baada ya kusherehekea Mwaka Mpya wa 2018 akiwa na marafiki zake hao.

Alisema kabla ya kukutwa na umauti, Winkdl akiwa na marafiki zake wanne ambao wanadaiwa kuwa na uhusiano naye wa kimapenzi, waligombana na baadaye ugomvi huo kusababisha kuchomwa kisu katika sehemu mbalimbali za mwili wake.

Kamanda Ali alisema watuhumiwa hao wanne ambao wote ni wanawake, raia wa Tanzania na Jeshi la Polisi linaendelea kuwashikiliwa kwa ajili ya kuwahoji na kukamilisha taratibu za kiuchunguzi.

"Inasemekana wote walikuwa wameshalewa na inadaiwa kuwa chanzo cha ugomvi ni wivu wa kimapenzi, lakini tunaendelea na uchunguzi," Kamanda huyo alisema.

Aidha, Kamanda Ali alibainisha kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye Hospitali ya Mnazimmoja kisiwani hapa.

Aliongeza kuwa raia huyo wa kigeni alikuwa anaishi Zanzibar akiwa ni msimamizi wa mapishi katika hoteli moja ya kitalii kisiwani hapa.

Maoni

ZILIZO SOMWA MARA NYINGI

ULAJI WA MARA KWA MARA WA MBEGU ZA MABOGA HUKUKINGA NA KUKUEPUSHA NA MAGONJWA 1O MWILINI MWAKO...

Dalili 6 zitakazokuonyesha kuwa mwenzi wako ana mtu mwingine katika mahusiano

FAIDA YA JUICE YA KAROTI KATIKA MWILI WA BINADAM

DAWA BORA YA NGUVU ZA KIUME NA MAUMBILE MADOGO

AINA ZA MBOLEA & MATUMIZI YAKE KITAALAM

Madhara ya Chai na Kahawa Kiafya

Fahamu Aina 7 Za Juisi Zenye Kuondoa Sumu Mwilini

Ugonjwa wa Chango La Uzazi

Madhara Ya Kuangalia Video za Porno {Ngono} na Namna ya Kujizuia

Athari za kiafya za vyakula vyenye Wanga