TAARIFA MPYA
Ronaldo De Lima awafungukia Cristiano na Messi
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Nyota wa zamani wa Real Madrid, Barcelona na timu ya taifa ya Brazil Ronaldo Luís Nazário de Lima amesema Cristiano Ronaldo na Lionel Messi wamefanikiwa kutwaa tuzo za mchezaji bora mara nyingi kutokana na kukosa ushindani.
Ronaldo ambaye ni mshindi mara tatu wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa FIFA, amesema anaheshimu mafanikio ya nyota hao wawili lakini ukweli ni kwamba wameyapata kwasababu hakuna watu wengine wa kushindana nao tofauti na zamani ambapo vipaji vilikuwa vingi.
''Cristiano na Messi wamefanya vizuri kwa muda mrefu lakini suala la kuwa wachezaji bora katika kizazi chao limekuwa rahisi aidi kutokana na kukosekana kwa watu wa kushindana nao tofuati na zamani ambapo vipaji vilikuwa vingi'', amesema Ronaldo de Lima.
Ronaldo ameengeza kuwa wakati yeye anakuwa mchezaji bora kulikuwa na ushindani mkubwa kuliko sasa. ''Wakati mimi natwa tuzo ya mchezaji bora mara tatu kulikuwa na vipaji vikubwa kama Zinedine Zidane, Rivaldo, Lus Figo pamoja na Ronaldinho'', ameongeza.
Ronaldo ambaye ametwaa Kombe la Dunia mara mbili amekiri kuwa yeye ni shabiki mkubwa wa nyota hao wawili lakini amesisitiza kuwa kungekuwa na vipaji vingi kama zamani isingekuwa rahisi kwao kufikia mafanikio hayo. Cristiano na Messi wote wameshinda Ballon d'Or mara tano.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni
TAFADHARI !!
- Tumia Lugha Nzuri Kutoa Maoni
Usitumie kauli za Karaha AU Zenye Kukela :
C.E.O
Gneous OG