TAARIFA MPYA
WENGER AVUNJA RECORD YA FERGUSON
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
KOCHA Mfaransa wa Arsenal, Arsene Wenger jana amevunja rekodi ya Mscotland, Alex Ferguson katika Ligi Kuu ya England.
Hiyo ni baada ya Arsene Wenger jana kuiongoza Arsenal katika mechi ya 811 ya Ligi Kuu ikilazimishwa sare ya 1-1 na wenyeji, West Bromwich Albion Uwanja wa The Hawthorns. Katika mchezo huo, Arsenal ilitangulia kupata bao dakika ya 83 baada ya shuti la mpira wa adhabu la Alexis Sanchez lilipombabatiza James McClean akajifunga.
Lakini West Bromwich Albion wakasawazisha bao hilo kupitia kwa Jay Rodriguez aliyefunga kwa penalti dakika ya 89 baada ya Calum Chambers kuunawa mpira.
Wenger alijiunga na Arsenal Septemba 22, mwaka 1996, akichukua nafasi ya Bruce Rioch aliyefukuzwa mwezi Agosti mwaka 1996.
Arsene Wenger jana amevunja rekodi ya Mscotland, Alex Ferguson katika Ligi Kuu ya England
Katika kipindi chote hicho, Wenger ameshinda mataji 17 Arsenal, matatu ya Ligi Kuu ya England misimu ya 1997–1998, 2001–2002 na 2003–2004, Kombe la FA saba misimu ya 1997–1998, 2001–2002, 2002–2003, 2004–2005, 2013–2014, 2014–2015 na 2016–2017.
Mataji mengine Wenger ameshinda Arsenal ni Ngao ya Jamii mara saba pia, miaka ya 1998, 1999, 2002, 2004, 2014, 2015 na 2017, wakati Ferguson katika mechi 810 kati ya 1986 na 2013 ameshinda mataji 34.
Hayo ni pamoja na ya Ligi Kuu 13 misimu ya 1992–1993, 1993–1994, 1995–1996, 1996–1997, 1998–1999, 1999–2000, 2000–2001, 2002–2003, 2006–2007, 2007–2008, 2008–2009, 2010–2011 na 2012–2013.
Matano ya Kombe la FA misimu ya 1989–1990, 1993–1994, 1995–1996, 1998–1999 na 2003–2004, Kombe la Ligi manne misimu ya 1991–1992, 2005–2006, 2008–2009, 2009–2010 na Ngao ya Jamii 10 miaka ya 1990, 1993, 1994, 1996, 1997, 2003, 2007, 2008, 2010 na 2011.
Mengine ni ya Ligi ya Mabingwa mawili 1998–1999 na 2007–2008, Kombe la Washindi Ulaya msimu wa 1990–1991, Super Cup ya UEFA 1991, Kombe la Mabara la klabu 1999 na Klabu Bingwa ya Dunia mwaka 2008.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni
TAFADHARI !!
- Tumia Lugha Nzuri Kutoa Maoni
Usitumie kauli za Karaha AU Zenye Kukela :
C.E.O
Gneous OG