TAARIFA MPYA
Dodoma, Alliance, zaponza waamuzi daraja la kwanza
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Kamati ya uendeshaji na usimamizi ya Bodi ya Ligi imewachukulia hatua waamuzi wote waliochezesha mchezo wa ligi daraja la kwanza kati ya Dodoma FC dhidi ya Alliance uliopigwa mjini Dodoma Jumamosi iliyopita ambapo mwamuzi wa kati alikuwa ni Andrew Shamba ambaye alionekana kuboronga zaidi katika mchezo huo na kuchezesha chini ya kiwango.
Kitu ambacho kilistua wengi ni mwamuzi huyo kutoa kadi nne nyekundu kwa timu mmoja (Alliance)
Afisa mtendaji mkuu wa Bodi ya Ligi Boniface Wambura amethibitisha: “Katika mechi hiyo, waamuzi wote wanne wamefungiwa miaka mitatu kila mmoja na sababu ya kuwafungia ni kwamba walichezesha mechi chini ya kiwango.”
“Ripoti ya kamishna imeonesha hivyo na adhabu yao imezingatia kanuni ya ligi daraja la kwanza inayohusu udhibiti wa waamuzi na ikumbukwe kati ya waamuzi hao wawili ni waamuzi wa ligi kuu Tanzania bara kwa hiyo kamati imeona kwamba kama mwamuzi wa ligi kuu anakwenda kuchezesha mechi ya daraja la kwanza chini ya kiwango kamati iliamini kamati ya waamuzi iliwapa mechi hiyo wakiamini wataiendesha vizuri.”
“Kamati ilitafakari sana hicho kiwango kilichooneshwa na waamuzi na haikuridhika hivyo imeona kwamba inawezekana kuna ushawishi mwingine uliwafanya waamuzi hao wachezeshe kwa kiwango hicho.”
“Kamati imewasiliana na TFF ikiomba suala hili liende kwenye vyombo vingine vya uchunguzi vinavyohusiana na makosa mengine ya rushwa kwa sababu TFF haina mamlaka au vyombo vinavyoweza kuchunguza masuala ya rushwa, tunashukuru TFF wameshapeleka barua TAKUKURU na sisis tumepewa nakala.”
Kamishna wa mchezo huo pia hakuna, amefungiwa miaka mitatu kwa kushindwa kutoa taarifa yenye usahihi kwa sababu kamati imeangalia taarifa na kugundua haikujitosheleza kuonesha nini hasa kilitokea wakati wa mechi.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni
TAFADHARI !!
- Tumia Lugha Nzuri Kutoa Maoni
Usitumie kauli za Karaha AU Zenye Kukela :
C.E.O
Gneous OG