TAARIFA MPYA
KOCHA MROMANIA WA AZAM AMEKUBALI KWA YULE MGHANA.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Bosi wa benchi la ufundi la Azam FC, Aristica Cioaba, raia wa Romania na wasaidizi wake, wanakoshwa na soka la mshambuliaji wao mpya, Bernard Arthur raia wa Ghana ambaye amekuwa msaada mkubwa katika ushambuliaji.
Arthur amejiunga na Azam akitokea Liberty Professional ya kwao Ghana, Jumatano wiki hii aliiongoza timu hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Jamhuri kwenye Kombe la Mapinduzi.
Katika ushindi huo, Arthur alifunga bao moja kati ya matatu waliyopata na kuiwezesha Azam kufikisha pointi sita kabla ya mchezo wa jana dhidi ya URA na leo dhidi ya Simba.
Cioaba alisema Arthur amekuwa msaada katika safu yao ya ushambuliaji ambayo ilikuwa inafunga mabao machache.
“Amekuja vizuri kwa kuingia ndani ya timu na kutupa matokeo yale ambayo tulikuwa tunayataka sisi, utaona kwamba ana muendelezo mzuri wa kufunga tangu alipoanza kutufungia dhidi ya Stand United katika ligi kuu.
“Naamini kwa uwezo wake kuna kitu kikubwa ambacho atakifanya kwenye mechi zinazokuja, kwa sasa naamini mshambuliaji huyu ni mtu sahihi kabisa katika kikosi chetu ukizingatia mwenzake, Mbaraka Yusuph yuko nje kutokana na majeraha,” alisema kocha huyo.
SOURCE: CHAMPIONI
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni
TAFADHARI !!
- Tumia Lugha Nzuri Kutoa Maoni
Usitumie kauli za Karaha AU Zenye Kukela :
C.E.O
Gneous OG