TAARIFA MPYA
Arsenal Wakata Tamaa
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Usiku wa jana kwa mara nyingine tena mzimu wa penati unaendelea kumtesa golikipa wa Arsenal Petre Cech, wengi walitarajia Hazard angefunga tuta lile labda kama angepiga nje ya lango la Arsenal.
Ni penati ya 15 kwa Cech tangu ajiunge na klabu ya Arsenal akitokea Chelsea, lakini huwezi amini kwamba pamoja na ubora wake wote alionao mlinda lango huyo lakimi hajawahi kuokoa penati hata moja akiwa na Arsenal.
Mbaya zaidi ni kwamba kati ya mikwaju ya penati 15 iliyopigwa kuelekea lango lake, mikwaju 3 tu ndio aliweza kuifuata huku mikwaju 12 ya penati aliruka upande ambao mpira haukwenda.
Tayari hoja kuhusu uwezo wa golikipa huyo kwenye suala la penati imekuwa kubwa kiasi cha kumfanya mlinda lango wa zamani wa Arsenal David Seaman kuwaomba mashabiki wa Gunnerz kuwa watulivu.
Seaman ametoa ushauri kwa Cech kwamba kama anataka ushauri kutoka kwake baasi anaweza kumpigia simu wakati wowote na anaweza kumpa ushauri kuhusu mbinu za kuokoa penati.
Matokeo ya suluhu ya jana yanawafanya Arsenal kubaki katika nafasi ya 6 ya msimamo wa ligi ya EPL wakiwa na alama 39 nafasi ambayo inawaweka njoa panda kushiriki michuano ijayo ya Champions League.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni
TAFADHARI !!
- Tumia Lugha Nzuri Kutoa Maoni
Usitumie kauli za Karaha AU Zenye Kukela :
C.E.O
Gneous OG