TAARIFA MPYA
Nini Tutarajie Tuzo Mchezaji Bora
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Mohamed Salah, Pierre Aubameyang na Sadio Mane wanatoana jasho kuwania tuzo ya mchezaji bora wa bara la Afrika ambapo tuzo hizo hutolewa kila mwaka na mwaka huu zinatolewa mjini Accra.
Salah aanapewa nafasi kubwa sana kutwaa tuzo ya mchezaji bora Afrika mwaka huu, hii iko wazi kutokana na kiwango kikubwa sana anachokionesha msimu huu na Liverpool ambapo ndio anaongoza kwa ufungaji EPL.
Salah anaonekana kuibeba Liverpool mabegani mwake sawa na alivyowabeba Wamisri na kuwapeleka fainali za kombe la dunia mwakani na ni wazi kwamba sio Mane wala Aubameyang anayekaribia mafanikio yake msimu huu.
Dua za raia wa Senegal zitakuwa mbaya kwa Salaah kwani wana kiu sana ya kutwaa tuzo hiyo ambayo tangu El Hadji Diouf atwae tuzo hiyo mwaka 2002 haijawahi kufika tena Senegal na Mane ndio anategemewa kuipeleka Senegal.
Tayari Piere Aubameyang ameshatwaa tuzo hiyo mwaka juzi lakini Mane na Salah hii inaweza kuwa mara yao ya kwanza kuchukua tuzo hii ambayo kwa sasa inashikiliwa na nyota wa Algeria Riyad Mahrez.
Tuzo nyingine ambayo inasubiriwa sana ni tuzo ya kocha bora Afrika ambapo kocha wa Nigeria Gernot Rohr, kocha wa Misri Hector Cuper na kocha L’Hussein Amouta wa Wydad Club watatoana jasho katika tuzo hii.
Pia kutakuwa na tuzo ya mwanasoka bora wa kike Afrika ambapo Mnigeria Asisat Oshoala atachuana na Chrestina Kgatiana wa Afrika Kusini pamoja na Gabrielle Obiudi anayekipiga timu ya taifa Cameroon na klabu ya CSKA Moscow.
Samahan kwakutokuwa na Picha
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni
TAFADHARI !!
- Tumia Lugha Nzuri Kutoa Maoni
Usitumie kauli za Karaha AU Zenye Kukela :
C.E.O
Gneous OG