TAARIFA MPYA
Takukuru kufatiria Matumizi , fedha za Umma
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), mkoani Kilimanjaro imesema mkakati wao mwaka huu ni kufuatilia matumizi ya fedha za umma zinazotolewa na serikali, ili zitumike kama zilivyokusudiwa.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa Takukuru, Mkoa wa Kilimanjaro, Holle Makungu, alipokuwa akizungumza na wanahabari kuwa serikali inatoa fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo, lakini wapo baadhi ya watumishi wa umma ambao sio waadilifu na kuzifuja.
Alisema, ili kuhakikisha lengo la serikali linakusudiwa, mkakati mkubwa watakaoutekeleza katika mwaka huu ni kufuatilia fedha hizo na utaanza zitakapotolewa na wizara kuhakikisha zinafika zote kwa mtumiaji, upatikanaji wa makandarasi, ulipwaji wa kandarasi na ukaguzi wa miradi.
“Mpango huu utatoa uhakika kuwa fedha za umma zinatumika ipasavyo kwa ubora uliokusudiwa tofauti na ilivyokuwa awali, fedha nyingi zilichepushwa na kufanyiwa ubadhirifu, ndio maana tumekuwa tukiibua ubadhirifu mwingi uliofanyika huko nyuma,” alisema Makungu.
Aliwataka watumishi wa umma kutimiza majukumu yao kwa kiapo na kanuni za maadili na kwamba yeyote atakayebainika kuomba au kupokea rushwa na kutumia fedha za serikali kinyume na malengo yaliyokusudiwa, atachukuliwa hatua za kisheria ikiwamo kufikishwa mahakamani.
Aidha Makungu alisema, taasisi hiyo itaendelea kutoa elimu kwa wananchi kupitia kampeni mbalimbali na kurugenzi ya uelimishaji umma ambayo ina watumishi kila wilaya, ili kuwawezesha kutoa taarifa mbalimbali zikiwamo kero.
“Tumekuwa tukitoa mkakati wa kitaifa wa kupambana na rushwa na mpango wa utekelezaji awamu ya tatu (NACSAP 111), unaowashirikisha wadau na sehemu mbalimbali nchini kupambana dhidi ya rushwa, tumekuwa tukiwahimiza wadau kuchukua hatua badala ya wao kubaki watazamaji,” alisema Makungu.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni
TAFADHARI !!
- Tumia Lugha Nzuri Kutoa Maoni
Usitumie kauli za Karaha AU Zenye Kukela :
C.E.O
Gneous OG