TAARIFA MPYA
Alie Katwa Maskio kwa kumlawiti Mtoto Atiwa nguvuni na Jeshi La Polisi
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga Simon Haule amethibitisha kuwa Jeshi la Polisi Mkoani kwake linamshikilia kijana Msigala Salum (24) kwa tuhuma za kumlawiti mtoto mwenye umri wa miaka mitatu.
Kamanda Haule amesema Kijana huyo aliyejulikana kwa jina la Msigala Salum (24) amekatwa masikio yote mawili na wananchi wenye hasira kali baada ya kumlawiti mtoto huyo mwenye umri wa miaka mitatu katika eneo la Majengo Mapya Kata ya Lubaga Manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga.
"Tukio hilo limetokea Disemba 20, 2017 majira ya saa tatu asubuhi ambapo kijana huyo anayejishughulisha na shughuli ya kuosha magari mkazi wa Ndala, alimdanganya mtoto huyo wakati akicheza na wenzake nyumbani kwao, kutokana na tukio hilo mtuhumiwa alishambuliwa na wananchi kabla ya Jeshi la polisi kufika eneo la tukio na kumuokoa", amesema Kamanda Haule.
Aidha kamanda Haule ameongeza kwa kusema kuwa mara baada ya tukio hilo baba mzazi wa mtoto huyo alimkamata mtuhumiwa na kumkata masikio yote mawili kwa kutumia kisu na kukimbia, na jeshi la Polisi bado linaendelea kumtafuta.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni
TAFADHARI !!
- Tumia Lugha Nzuri Kutoa Maoni
Usitumie kauli za Karaha AU Zenye Kukela :
C.E.O
Gneous OG