TAARIFA MPYA
RAIS wa KOREA KASKAZINI APIGA MARUFUKU KUNYWA ' KULEWA SIKU YA KLISMASI
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Kim Jong Un.
RAIS Kim Jong Un wa Korea ya Kaskazini amepiga marufuku kuimba, kunywa vileo na kufanya mikusanyiko ya aina yote nchini humo wakati wa Krismasi mwaka huu.
Kwa mujibu wa shirika la ujasusi la Korea ya Kusini (NIS), hatua hiyo inakazia amri ya kupiga marufuku sherehe za Krismasi ya mwaka jana (2016) ikilenga kuzuia nguvu za upinzani nchini humo hususan sasa ambapo vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya nchi hiyo vinaonyesha kuiumiza nchi hiyo.
“Korea ya Kaskazini imeanzisha mfumo wa jumuia za chama tawala kuripoti matatizo ya kiuchumi ya watu wanayokumbana nayo kila siku, na imepiga marufuku mikusanyiko inayohusiana na unywaji wa vileo, uimbaji na burudani nyingine, na imeimarisha udhibiti wa habari kutoka nje,” lilisema NIS.
Fursa za kuitumia sikukuu hiyo kueneza uelewano na furaha zinazidi kufifia katika taifa hilo linalodaiwa kutawaliwa kidikteta na ambalo limepiga marufuku dini zote isipokuwa maadhimisho ya familia iliyoasisi taifa hilo la kikomunisti. Mwaka jana, Kim aliwazuia Wakristo nchini humo kuadhimisha Krismasi na badala yake akawataka kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa bibi yake, Kim Jong-suk, aliyezaliwa siku ya mkesha wa Krismasi mwaka 1919.
Akiwa Mkomunisti aiyebobea, mke wa kwanza wa mwasisi wa taifa hilo la kikomunisti, Kim Il Sung, anafahamika kwa wananchi wa Korea ya Kaskazini kama “Mama Mtukufu wa Mapinduzi”. Miti yenye mapambo ya kuadhimisha Krismasi huonekana katika maduka makubwa ya bidhaa jijini Pyongyang, lakini hakuna alama zozote za kidini.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni
TAFADHARI !!
- Tumia Lugha Nzuri Kutoa Maoni
Usitumie kauli za Karaha AU Zenye Kukela :
C.E.O
Gneous OG