TAARIFA MPYA
Rugemalila Anataka Kumtaja Mwizi wa Fedha za ESCROW
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Mfanyabiashara James Rugemalila anayekabiliwa na kesi ya utakatishaji fedha ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa anahitaji kuonana na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) ili ampe ushahidi wa nani anayepaswa kukamatwa katika kesi hiyo.
December 8, 2017 Rugemarila aliieleza mahakama hiyo kuwa unahitajika ushirikiano baina yake na upande wa mashtaka ili kumbaini mwizi wa Sh.Bil 309 za Serikali.
Mbali ya Rugemarila, Mshtakiwa mwingine ni mmiliki wa IPTL Harbinder Singh Sethi ambapo kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi, utakatisha fedha na kuisababishia Serikali hasara ya USD 22, 198,544.60 na Sh.Bil 309.
Rugemarila ameyaeleza hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Leornad Swai kudai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, hivyo anaomba ahirisho.
Baada ya kueleza hayo, Rugemarila alinyoosha mkono ambapo amesema kuwa anaushukuru upande wa mashtaka ulimchukua gerezani na kumpeleka Upanga kwa mahojiano na kumrudisha salama gerezani.
“Leo nimekuja na ushahidi, hivyo naomba nikutane na DPP ili niweze kumsaidia kumjua mwizi anayepaswa kukamatwa, kwani lengo letu ni kuonyesha kuwa tupo Innocent,” alieleza Rugemarila.
Kutokana na maelezo hayo, Hakimu Shaidi alimtaka Rugemarila kuwasiliana na mawakili wake ili waandike barua ya kuwasilisha kwa DPP kuhusu suala hilo la ushahidi wake, ambapo ameahirisha kesi hiyo hadi January 5, 2018
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni
TAFADHARI !!
- Tumia Lugha Nzuri Kutoa Maoni
Usitumie kauli za Karaha AU Zenye Kukela :
C.E.O
Gneous OG