TAARIFA MPYA
Kocha Mkuu Simba Atimuliwa ni baada ya mkataba wake Kuvunjwa
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Klabu ya Simba na kocha wake mkuu Joseph Omog, kwa pamoja wameamua kuvunja mkataba baina yao kwa makubaliano maalum yanayozingatia maslahi ya pande zote mbili.
Taarifa hii inakuja ikiwa ni chini ya saa 24 tangu klabu hiyo ambayo walikuwa mabingwa watetezi wa kombe la shirikisho kutupwa nje ya michuano hiyo na timu ya Warrios kwenye mchezo uliochezwa jana jioni na kufungwa mabao 4-3 kupitia mikwaju ya panalti.
Simba kupitia taarifa yake imeeleza kuwa, inamshukuru kocha Omog na inamtakia kila la kheri kwenye maisha yake nje ya Simba.
Pia klabu hiyo imesema kwasasa majukumu yote ya ufundi yatakuwa chini ya kocha msaidizi Masoud Djuma na timu itaendelea na mazoezi siku ya kesho kisha kupumzika siku ya Jumatatu kwaajili ya sikukuu ya Krismas na itaingia kambini Jumanne.
Simba itasafiri kwenda Mtwara wiki ijayo ambapo itacheza na timu ya Ndanda kwenye mchezo wa ligi kuu raundi ya 12 siku ya jumamosi Disemba 30. Simba inaongoza ligi ikiwa na alama 23 baada ya michezo 11.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni
TAFADHARI !!
- Tumia Lugha Nzuri Kutoa Maoni
Usitumie kauli za Karaha AU Zenye Kukela :
C.E.O
Gneous OG