TAARIFA MPYA
Kombe la Shirikisho la Azam Sport Federation Cup Kutimua Vumbi Leo
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Msimu wa tatu wa Azam Sports Federation Cup unazinduliwa rasmi leo Ijumaa katika mchezo wa raundi ya pili kati ya bingwa mtetezi Simba SC dhidi ya Green Warriors.
Tangu kuanza kwa mechi za msimu huu hapajawahi kufanyika uzinduzi rasmi kutokana na bingwa mtetezi kutokuanzia katika hatua za awali, na sasa kwa mujibu wa ratiba hafla ya uzinduzi itafanyika leo wakati wa mchezo huo utakaopigwa kwenye dimba la Chamazi Dar es Salaam na kurushwa mbashara kupitia Azam Sports 2.
Tayari mechi za msimu huu zilianza kuchezwa tangu hatua ya awali iliyohusisha mabingwa wa mikoa hadi kufikia hatua hii inayojumuisha timu 64 zikiwemo timu 16 za ligi kuu ya Tanzania bara.
Mbali na mchezo huo, mechi nyingine saba za raundi ya pili zitapigwa leo katika viwanja ni kama ifuatavyo:-
Stand United vs AFC ya Arusha,
Polisi Dar vs Mgambo JKT,
Kariakoo vs Transit Camp,
Biashara United vs Mawenzi Market,
Ruvu Shooting vs Madini FC,
Mufindi United vs Pamba,
Singida United vs Bodaboda FC.
Katika mechi saba zilizopigwa jana, Kagera Sugar iliiangushia kipigo cha mabao 7-0 timu ya Makambako Heroes katika dimba la Kaitaba Bukoba, Rhino Rangers ikaichapa Alliance bao 1-0, Njombe Mji ikaibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mji Mkuu na Polisi Tanzania ikaipiga Mshikamano mabao 2-1.
Katika viwanja vingine, JKT Oljoro ikaiangusha Ambassador ya Kahama kwa penati 4-3 baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya bao 1-1 katika mchezo uliopigwa dimba la Taifa Kahama, Majimaji Rangers ikaibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mbeya Kwanza na katika mchezo wa mwisho kwa siku ya jana uliopigwa kwenye dimba la Chamazi, Friends Rangers ikaibamiza Ashanti United mabao 2-0 yaliyofungwa na Hijja Shabani pamoja na Haruna Moshi ‘Boban’.
Hadi sasa timu 11 zimefuzu kuingia raundi ya tatu ya michuano hiyo. Timu hizo ni Ndanda FC, Toto African, KMC, Buseresere, Kagera Sugar, Rhino Rangers, Njombe Mji, Polisi Tanzania, JKT OljoroMajimaji Rangers na Friends Ranger
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni
TAFADHARI !!
- Tumia Lugha Nzuri Kutoa Maoni
Usitumie kauli za Karaha AU Zenye Kukela :
C.E.O
Gneous OG