TAARIFA MPYA
Lwandamila Aendelea kubaki Zambia
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Kocha mkuu wa mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania bara klabu yaYanga, Mzambia George Lwandamina amepata msiba baada ya kufiwa na mtoto wake wa kiume.
Taarifa ya Yanga imeeleza kuwa mtoto huyo aitwaye Mofya Lwandamina amefariki jana jioni huko nyumbani kwao Zambia.
“Kwa wana Yanga na wadau wote wa soka, kocha wetu George Lwandamina amepata msiba, amefiwa na mtoto wake wa kiume jana huko Zambia”, imeeleza taarifa ya klabu.
Kocha George Lwandamina ataendelea kuwa kwao Lusaka kwa muda mrefu, ikumbukwe aliondoka Dar es Salaam wiki iliyopita kwenda nyumbani kwa ajili ya kuhudhuria mahafali ya mwanawe wa kike, Nasanta Lwandamina aliyehitimu Stashahada ya Afya ya Jamii katika Chuo Kikuu cha NRDC.
Yanga SC kesho watakuwa kwenye Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam kumenyana na Reha FC katika hatua ya 64 Bora ya kombe la shirikisho (ASFC).
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni
TAFADHARI !!
- Tumia Lugha Nzuri Kutoa Maoni
Usitumie kauli za Karaha AU Zenye Kukela :
C.E.O
Gneous OG