TAARIFA MPYA

Madhara ya Chai na Kahawa Kiafya

Picha
CAFFEINA/KAFEINA. Kafeina ni nini?: 1. Kafeina ni madawa ya kulevya kundi la ‘Stimulants drugs’. Utashangaa. Habari ndiyo hiyo. Hii ndiyo sababu kwa mtu aliyezoea kunywa chai hii kila siku au kahawa, siku asipokunywa kichwa humuuma, ni kwa sababu amekuwa mtegemezi au teja wa kafeina. Kafeina ni kiungo mhimu karibu katika soda zote zenye rangi nyeusi; Coca-cola, Pepsi, Sayona nyeusi, Azam cola na kadharika. Kafeina huongezwa pia katika Red bull, Malta na katika baadhi ya dawa za kupunguza maumivu mwilini. Kwahiyo Kafeina ambayo hupatikana katika chai na kahawa ni aina mojawapo ya madawa ya kulevya. 2. Kafeina ni kikojoshi (diuretics). Kafeina ni dawa ya kukufanya ukojowe. Ukinywa kikombe kimoja cha kinywaji chenye kafeina yaani chai au kahawa, basi muda si mrefu utaenda kukojoa vikombe viwili. Kwa sababu kafeina ni taka isiyotakiwa mwilini, mwili utafanya kila uwezalo ikibidi ujikamuwe wenyewe kupata maji ya ziada kuweza kuitoa kafeina hii uliyoinywa kwa kisingizio ch...

Majaliwa Atoa Agizo wizara ya chakula leo

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza mtambo wa kutengenezea mbegu za pamba ulioko mkoani Mbeya, kuondolewa mara moja na kupelekwa kwenye mikoa inayolima zao hilo huku akihoji sababu za msingi zilizochangia mtambo huo kuwekwa huko.

Akizungumza na wadau wa zao hilo  Waziri Mkuu alitoa agizo hilo na kuitaka wizara inayohusika kuchukua hatua mara moja huku akivitaka viwanda vya ndani vyenye uwezo wa kuzalisha mbegu kujitokeza.

Amesema haiwezekani mtambo unaotengeneza mbegu za pamba ukawekwa kwenye mkoa ambao haulimi zao hilo na kuhoji kulikuwa na sababu gani ya msingi ya kuwekwa mkoani Mbeya, ndipo aliamua kuagiza kuondolewa na kupelekwa kwenye mikoa inayolima pamba.

Hata hivyo Majaliwa  alisema kiwanda cha Quiton ambacho kimewekeza nchini kwa ajili ya  kutengeneza mbegu za pamba aina ya Quiton lakini cha kusikitisha mpaka msimu wa kilimo unafika hakuna mbegu na hii kampuni inamilikiwa na Wazimbabwe na wao wanalima pamba nchini kwao katika hili tutafakari.

‘’Tunataka zao la pamba liwe na mafanikio makubwa na haya yote yanapaswa kusimamiwa na watumishi wa serikali ili kuweza kumkomboa mkulima wa pamba, kulima kilimo chenye tija ambacho kitawaletea mabadiliko ya kiuchumi kwani asilimia 80 ya watanzania wanategemea kilimo” amesema waziri mkuu.

Kwa upande wake Waziri wa Chakula na Ushirika Dk Charles Tizeba amesema katika msimu uliopita jumla ya kilo 133 milioni za pamba zimezalishwa , ambapo kwenye msimu wa mwaka huu wanatarajia kuzalisha kilo 600 milioni za pamba huku uzalishaji wa tija utaongezeka kwa ekari kutoka kilo 200 hadi 500.

Amesema  ekari 1,100,000 zimepandwa mbegu zisizo na manyoya ambapo lengo ni kufikia ekari 3,000,000 milioni na kuongeza kuwa umetumika utaalamu katika upandaji ,huku akibainisha kuwa tayari kuna chupa 4,764,000 za dawa za kuuwa wadudu zimepatikana ambazo zitasambazwa kwa wakulima kwa awamu nne.

Awali akizungumza kwenye mkutano huo mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack amesema  jumla ya ekari 128,668 za pamba zimelimwa mpaka sasa mkoani Shinyanga, kutoka kwa wakulima 24,175 ambapo wanaendelea kutoa elimu kwa wakulima.

     

Maoni

ZILIZO SOMWA MARA NYINGI

ULAJI WA MARA KWA MARA WA MBEGU ZA MABOGA HUKUKINGA NA KUKUEPUSHA NA MAGONJWA 1O MWILINI MWAKO...

Dalili 6 zitakazokuonyesha kuwa mwenzi wako ana mtu mwingine katika mahusiano

FAIDA YA JUICE YA KAROTI KATIKA MWILI WA BINADAM

DAWA BORA YA NGUVU ZA KIUME NA MAUMBILE MADOGO

AINA ZA MBOLEA & MATUMIZI YAKE KITAALAM

Madhara ya Chai na Kahawa Kiafya

Fahamu Aina 7 Za Juisi Zenye Kuondoa Sumu Mwilini

Ugonjwa wa Chango La Uzazi

Madhara Ya Kuangalia Video za Porno {Ngono} na Namna ya Kujizuia

Athari za kiafya za vyakula vyenye Wanga