TAARIFA MPYA
Arsenal kuizuia Liver pool kuweka Rekodi Leo
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Tangia mwezi May mwaka 1998 klabu ya Arsenal haijawahi kupoteza mara nne mfululizo mbele ya Liverpool lakini hadi leo hii tayari wameshapoteza mara 3 mfululizo na hii ina maana wakipigwa leo watakuwa wamepoteza ya nne.
Liverpool wanawafuata Arsenal huku washika mitutu hao wakionekana kukaza sana katika uwanja wao wa nyumbani kwani katika michezo 14 waliyocheza Emirates wameshinda 13 huku wakipoteza mmoja tu mwezi uliopita zidi ya Manchester United.
Chini ya kocha Jurgen Klopp Liverpool wamefanikiwa kuifunga Arsenal walau mabao 3 au zaidi katika mechi nne walizokutana na Liverpool sasa wanakuwa wamewafunga Arsenal jumla ya mabao 14.
Uwezo wa Liverpool katika viwanja vya ugenini unaonekana kuwapa kiburi mashabiki wengi wa klabu hiyo kwani ndio klabu pekee katika historia kuweza kushinda michezo 4 mfululizo kwa wastani wa kuanzia mabao 3.
Endapo hii leo Liverpool watafanikiwa kumaliza mchezo bila nyavu yao kuguswa baasi itakuwa mara ya kwanza kwao msimu huu kucheza michezo 3 bila kuruhusu wavu wao kuguswa.
Tangu Arsenal watoke sare ya bila kufungana na Middlesbrough October mwaka 2016, klabu hiyo haijawahi kucheza mchezo katika uwanja wao wa Emirates katika michezo 23 iliyofuata na kumaliza mchezo bila kufunga goli.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni
TAFADHARI !!
- Tumia Lugha Nzuri Kutoa Maoni
Usitumie kauli za Karaha AU Zenye Kukela :
C.E.O
Gneous OG