TAARIFA MPYA
Club ya Ajax Yatimua Benchi Lote la Ufundi
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Klabu ya soka ya Ajax Amsterdam ya Uholanzi imelitimua benchi lake lote la ufundi likiongozwa na kocha mkuu Marcel Keizer baada ya kufanya vibaya kwenye ligi ya nyumbani na ligi ya Mabingwa Ulaya.
Ukiacha kocha mkuu Marcel Keizer, wengine waliofutwa kazi ni wasaidizi wake Dennis Bergkamp pamoja na Hennie Spijkerman.
Meneja mkuu wa timu hiyo ambaye ni golikipa wa zamani wa Manchester United Edwin Van De Sar amefutwa kazi pia, huku mkurugenzi wa ufundi Marc Overmars naye akitupiwa vilago.
Ajax inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 38 nyuma ya PSV yenye alama 43. Mlinzi wa zamani wa kimataifa wa uholanzi Michael Reiziger, na Winston Bogarde wamekabidhiwa timu kwa muda.
Makocha wanaotajwa kuchukua nafasi katika timu hiyo ni Ronald Koeman na Frank De Boer ambao wanatajwa huenda wakapewa timu kwa mkataba mrefu.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni
TAFADHARI !!
- Tumia Lugha Nzuri Kutoa Maoni
Usitumie kauli za Karaha AU Zenye Kukela :
C.E.O
Gneous OG