TAARIFA MPYA
KIJANA mmoja Akatwa SIKIO baada ya kumlawiti Mtoto
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
KIJANA Msigala Salum (24), mkazi wa Kata ya Ndala mjini Shinyanga, amenusurika kifo kutokana na kufumwa akimlawiti mtoto wa miaka mitatu, baada ya baba mzazi wa mtoto huyo kuchukua kisu na kumkata masikio yote kisha kukimbia kusikojulikana.
Tukio hilo limetokea juzi majira ya saa 3:00 asubuhi katika maeneo ya Majengo Mapya Kata ya Lubaga mjini Shinyanga, wakati kijana huyo akiwa katika shughuli zake za kuosha magari, ndipo alipodaiwa kumrubuni mtoto huyo akiwa na wenzake akicheza na kwenda kumfanyia ukatili huo.
Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga, Simon Haule, alisema baada ya kijana huyo kutenda unyama huo na kukatwa maskio, jeshi lilipewa taarifa na kufika eneo la tukio na kufanikiwa kumtia nguvuni.
Alisema baada ya kumkuta mtuhumiwa akiwa katika hali mbaya, walimpeleka kwenye Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kupatiwa matibabu. Kamanda Haule alisema upelelezi juu ya suala hilo unaendelea na kwamba utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.
Aidha, alisema Jeshi pia linamtafuta baba mzazi wa mtoto huyo kwa kosa la kujichukulia sheria mkononi kwa kuwa baada ya kumkata masikio yote mawili, alikimbia kusiko julikana.
Haule alisema mtoto aliyefanyiwa unyama huo alipelekwa kuchukuliwa vipimo na kupatiwa tiba kwenye hospitali ya mkoa.
Katika tukio lingine, jeshi hilo liliua Bahati Peter (28) mkazi wa Kata ya Oldshinyanga, anayetuhumiwa kuwa jambazi wakati akiwatoroka askari polisi waliomtia kizuizini kwenda kuwaonyesha wezake walipo.
Alisema askari walimpiga risasi na kufariki dunia wakati akijaribu kukimbia.
Kamanda Haule alisema tukio hilo liltokea Desemba 19, mwaka huu, majira ya saa 4:30 usiku katika eneo la Kata ya Ndala mjini Shinyanga, mahali alipokuwa ameficha silaha aina ya Shotgun yenye namba 006096210 TZ CAR 98454 ikiwa na risasi nne na alipoamriwa akaonyeshe wenzake ndipo akaanza kukimbia na kupigwa risasi.
Alisema kabla ya kuuawa, mtu huyo alipekuliwa nyumbani kwake na kukutwa na mali za wizi ikiwamo Laptop HP, simu aina ya Samsung na alikili kuiba mali hizo zikiwa kwenye gari eneo la Club ya Level Four, jengo la NSSF mjini Shinyanga.
Haule alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Shinyanga, huku juhudi za kuwakamata majambazi wenzake zikiendelea kwa kuhusisha taarifa za kiitelenjensia.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni
TAFADHARI !!
- Tumia Lugha Nzuri Kutoa Maoni
Usitumie kauli za Karaha AU Zenye Kukela :
C.E.O
Gneous OG