TAARIFA MPYA
Mwanamke anaswa na mzigo wa Bangi
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Tofauti na ilivyoanza kuzoweleka hivi sasa kukamatwa wasafirishaji wa bangi wanaotoka Tarime mkoani Mara kwenda Mwanza, safari hii mwanamke anashikiliwa na polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kukutwa na bangi.
Hata hivyo kinachoshangaza ni namna mwanamke huyo alivyokamatwa akiwa na bangi hiyo inayokadiriwa kuwa na uzito wa kati ya kilo 30 na 50 wilayani Ukerewe. Mara nyingi polisi imekuwa ikiwakamata watu wanaojihusisha na biashara hiyo kwenye magari yanayofanya safari zake kati ya Sirari wilayani Tarime na Mwanza.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema mwanamke huyo alikamatwa Desemba 19 katika Kisiwa cha Lyegoba kilichopo Kata ya Irugwa, saa moja jioni.
Msangi alisema bangi hiyo ilikuwa kwenye gunia moja, maboksi matatu na misokoto 371 kwa pamoja ikikadiriwa kuwa na kilo kati ya 30 hadi 50.
Alisema polisi wanaendelea na upelelezi ikiwamo kumhoji mtuhumiwa na endapo uchunguzi utakamilika watamfikisha mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabaili.
Baadhi ya wakazi wa Jiji la Mwanza akiwamo Beatrice Gerald walisema biashara ya bangi katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo inachangiwa na wananchi kutotoa taarifa na kikubwa ni polisi kuwa na ushirikiano mzuri na raia ili kuwabaini wahusika.
Mkazi wa Nyegezi, Stanslaus Wilbard alisema mbinu za kusaka dawa za kulevya kwa kutumia mbwa maalumu zikizingatiwa zitaleta ufanisi katika kupambana na vitendo hivyo.
Hivi karibuni polisi jijini Mwanza walizindua mbinu mpya ya kusaka dawa za kulevya kwa kutumia mbwa maalumu. Hatua hiyo ya polisi ilichochewa na wimbi la dawa la kulevya hususan bangi kunaswa katika vyombo vya usafiri vinavyotoka mkoani Mara.
Kamanda Msangi alisema watatumia mbinu hiyo ili kukomesha biashara ya dawa za kulevya na mkakati huo utakuwa shirikishi kati ya polisi na wananchi.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni
TAFADHARI !!
- Tumia Lugha Nzuri Kutoa Maoni
Usitumie kauli za Karaha AU Zenye Kukela :
C.E.O
Gneous OG