TAARIFA MPYA
SIMBA YA KILI JUMHITAJI ASANTE KWASI ' YA TUMA BARUA LIPULI
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Baada ya kimya cha muda mrefu hatimaye klabu ya Simba imenyoosha maelezo na kukiri kuwa inamuhitaji beki raia wa Ghana anayekipiga katika klabu ya Lipuli FC, Asante Kwasi.
Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba Zakaria Hanspoppe amesema klabu hiyo tayari imeandika barua kwenda kwa klabu ya Lipuli ya kumuhitaji beki huyo, huku akiwahakikishia wadau wa soka nchini kuwa Simba haina mpango wa kumsajili mchezaji huyo kwa njia isiyo halali.
"Ni kweli tunamuhitaji Asante Kwasi, na sasa tumepeleka barua rasmi Lipuli FC baada ya TFF kuongeza muda wa usajili. Nawahakikishia wadau wote wa soka kwamba Kwasi akija Simba atakuwa amekuja kihalali, hawezi kuja kwa njia isiyo halali," amesema Hanspoppe.
Uongozi wa klabu ya Lipuli FC imekiri kupokea barua hiyo na kuwakaribisha Simba kwa ajili ya mazungumzo
Hanspoppe pia amezungumzia wachezaji walioachwa Simba akithibitisha kumuacha mchezaji mmoja pekee na kwamba hakuna mchezaji mwingine mpya aliyesajiliwa klabuni hapo wakati wa dirisha dogo la usajili linalotarajiwa kufungwa Desemba 23 mwaka huu.
"Mchezaji aliyeachwa Simba ni Mwanjali peke yake, hakuna mchezaji mwingine aliyeachwa au aliyeongezwa Simba zaidi ya Kwasi," amesisitiza Hanspoppe
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni
TAFADHARI !!
- Tumia Lugha Nzuri Kutoa Maoni
Usitumie kauli za Karaha AU Zenye Kukela :
C.E.O
Gneous OG