TAARIFA MPYA
Uganda na Tanzania zatiliana Saini
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Tanzania kupitia kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo anayeshughulikia sekta ya Mifugo, Dkt. Mary Mashingo na Uganda kupitia kwa Balozi wake nchini Richard Tumusiime Kabonero leo zimesaini makubaliano ya kuboresha sekta ya mifugo.
Makubaliano hayo yamesainiwa mjini Bukoba na baada ya kutia saini Dkt. Mary Mashingo amesisitiza kwamba ushirikiano wa kitaalam katika kuratibu, kufuatilia hali ya mifugo na kufanya tathmini ya kila wakati utaleta mafanikio makubwa baina ya nchi ya Tanzania na Uganda.
“Magonjwa ya mlipuko kwa wanyama ni suala mtambuka duniani kote, hivyo ni muhimu kulishughulikia kwa pamoja ili kuwa na tija, pia tumeamua kwa pamoja kuanzia sasa kudhibiti tatizo la utoroshaji wa mifugo kwenye mipaka ya nchi zetu na hatua kali zitachukuliwa ili kutoa fundisho kwa yeyote atakayefanya makosa”, amesema Dkt. Mashingo.
Naye Balozi Kabonero amesema magonjwa ya mlipuko kwa wanyama hayana mipaka hivyo makubaliano yaliyofanyika yatasaidia kudhibiti magonjwa ya wanyama hatimaye kuboresha mifugo.
Kwa upande mwingine Dkt. Mashingo amezitaja baadhi ya sheria ambazo ni kipaumbele kwa wafugaji kuzingatia kwa sasa kuwa ni pamoja na Sheria ya Magonjwa ya Mifugo namba 17 ya mwaka 2003 na Sheria za Nyanda za Malisho na Vyakula vya Mifugo namba 13 ya mwaka 2010.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni
TAFADHARI !!
- Tumia Lugha Nzuri Kutoa Maoni
Usitumie kauli za Karaha AU Zenye Kukela :
C.E.O
Gneous OG