Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia 2017

TAARIFA MPYA

Madhara ya Chai na Kahawa Kiafya

Picha
CAFFEINA/KAFEINA. Kafeina ni nini?: 1. Kafeina ni madawa ya kulevya kundi la ‘Stimulants drugs’. Utashangaa. Habari ndiyo hiyo. Hii ndiyo sababu kwa mtu aliyezoea kunywa chai hii kila siku au kahawa, siku asipokunywa kichwa humuuma, ni kwa sababu amekuwa mtegemezi au teja wa kafeina. Kafeina ni kiungo mhimu karibu katika soda zote zenye rangi nyeusi; Coca-cola, Pepsi, Sayona nyeusi, Azam cola na kadharika. Kafeina huongezwa pia katika Red bull, Malta na katika baadhi ya dawa za kupunguza maumivu mwilini. Kwahiyo Kafeina ambayo hupatikana katika chai na kahawa ni aina mojawapo ya madawa ya kulevya. 2. Kafeina ni kikojoshi (diuretics). Kafeina ni dawa ya kukufanya ukojowe. Ukinywa kikombe kimoja cha kinywaji chenye kafeina yaani chai au kahawa, basi muda si mrefu utaenda kukojoa vikombe viwili. Kwa sababu kafeina ni taka isiyotakiwa mwilini, mwili utafanya kila uwezalo ikibidi ujikamuwe wenyewe kupata maji ya ziada kuweza kuitoa kafeina hii uliyoinywa kwa kisingizio ch...

VIGOGO WAPONZWA NA CHAPA

Picha
o VIGOGO kadhaa wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi wameponzwa na zoezi la upigaji chapa mifugo nchi nzima, baada ya kuvuliwa nyadhifa zao. Uamuzi wa kuwawajibisha vigogo hao umefanywa na waziri wa wizara hiyo, Luhaga Mpina, huku akiongeza muda wa mwezi mmoja zoezi la upigaji chapa mifugo kitaifa. Waliovuliwa nyadhifa ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Ugani wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dk. Erastus Mosha na Kaimu Mkurugenzi wa Ugani na Usajili, Bezia Rwengozibwa kwa kushindwa kusimamia kikamilifu zoezi hilo kwa mujibu wa Sheria ya Utambuzi, Usajili na Ufuatiliaji wa Mifugo na 12 ya mwaka 2010 na Kanuni zake za Mwaka 2011 GN 362. Mbali na wakurugenzi hao, pia maofisa wawili wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Luzangi Deogratius na Felista Kimario ambao wamepewa onyo kali kwa kushindwa kusimamia zoezi hilo huku waliovuliwa madaraka akiagiza wachukuliwe hatua kali za kinidhamu. Akizungumza jana katika zoezi la kuhitimisha upigaji chapa kitaifa katika Kata ya Migato Wilaya ya Itil...

HAJI APATA MKATABA KENYA

Picha
Beki wa kushoto wa Yanga, Mwinyi Haji. IMEBAINIKA kwamba uongozi wa timu ya AFC Leopards ya Kenya umemalizana na beki wa kushoto wa Yanga, Mwinyi Haji na umempa mkataba wa miaka miwili huku kinachosubiriwa kwa sasa ni beki huyo kupewa ruhusa na timu yake kabla ya kujiunga na timu hiyo ambayo inashiriki ligi ya Kenya. AFC Leopards inayonolewa na Mtanzania, Dennis Kitambi, imefikia uamuzi huo wa kumpa mkataba beki huyo baada ya kukoshwa na uwezo wake aliouonyesha wakati akiwa na timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes wakati ilipokuwa inashiriki michuano ya Chalenji iliyofikia tamati hivi karibuni. Chanzo cha karibu na beki huyo kimeliambia Championi Jumatatu kuwa Wakenya hao walishamalizana na Mwinyi ambapo kwa sasa kinachosubiriwa ni Yanga kumpa ruhusa beki huyo baada ya hivi karibuni kuandika barua ya kutaka kuondoka kutokana na kukosa namba ndani ya kikosi cha kwanza. “AFC Leopards wamefanya kweli baada ya kuonesha nia ya dhati tangu walipovutiwa na Mwinyi wakati akiwa ...

KOCHA WA YANGA Akubali Mbao FC iliwazidi Uwezo

Picha
go Kocha msaidizi wa Yanga Shadrack Nsajigwa amekubali kuwa timu yake ilizidiwa na Mbao na kujikuta ikiruhusu magoli mawili ndani ya kipindi cha pili , mlinzi huyo wa zamani wa kulia wa Yanga na Taifa Stars amesema kipindi cha pili Mbao walibadilika na kutumia nafasi walizozitengeneza kupata magoli . Nsajigwa amekubali kuwa Mbao walistahili kushinda mchezo huo baada ya kufanya kazi yao vizuri uwanjani . “ Hali ya mchezo kwa ujumla ilikuwa nzuri kiasi chake , kipindi cha kwanza mechi ilikuwa nusu kwa nusu lakini kipindi cha pili kilibadilika , Mbao walibadilika wakaja juu badae wakapata nafasi wakazitumia . Mpira ni mchezo wa matokeo , usipobadili nafasi ulizopata kuwa magoli basi huezi kufunga ”- Shadrack Nsanjgwa . “ Tumepoteza mchezo tunawapa hongera Mbao wamefanya kazi yao vizuri wamepata ushindi .” Nsajigwa akishirikiana na benchi la ufundi la Yanga ...

KIBONYEZO: Cha mabom ya Nyuklia Kipo Kwenye Meza Yangu

Picha
o Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong- un amesema kuwa na kibonyezo cha silaha za nyuklia kwenye meza yake wakati wote na hivyo Marekani isithubutu kuanza vita. Katika hotuba ya mwaka mpya iliyopeperushwa kwa njia ya runinga , alisema kuwa Marekani inaweza kufikiwa na silaha za nyuklia za Korea Kaskania akiongeza kuwa huo ni kweli na wala sio vitisho . Lakini pia alitoa wito kwa Korea Kusini kuja kwenye mazungumzo . Korea Kaskazini pia itatuma kikosi katika mashindano ya olimpiki ya msikmu wa baridi nchini Korea Kusini , Kim alisema . Wakati aliulizwa na waandishi wa habari kuhusu vitisho vya Kim, Rais wa Marekani alisema , " tutaona , tutaona ". Alikuwa akizungumza kando mwa sherehe za kuukaribisha mwaka mpya katika eneo lake ya kifahari la Mar-a- Lago huko Florida. Korea Kaskazini imewekewa vikwazo zaidi mwaka uliopita kwa kutokana na mipango yake ya silaha za nyuklia ...

WENGER AVUNJA RECORD YA FERGUSON

Picha
KOCHA Mfaransa wa Arsenal, Arsene Wenger jana amevunja rekodi ya Mscotland, Alex Ferguson katika Ligi Kuu ya England.  Hiyo ni baada ya Arsene Wenger jana kuiongoza Arsenal katika mechi ya 811 ya Ligi Kuu ikilazimishwa sare ya 1-1 na wenyeji, West Bromwich Albion Uwanja wa The Hawthorns. Katika mchezo huo, Arsenal ilitangulia kupata bao dakika ya 83 baada ya shuti la mpira wa adhabu la Alexis Sanchez lilipombabatiza James McClean akajifunga. Lakini West Bromwich Albion wakasawazisha bao hilo kupitia kwa Jay Rodriguez aliyefunga kwa penalti dakika ya 89 baada ya  Calum Chambers kuunawa mpira. Wenger alijiunga na Arsenal Septemba 22, mwaka 1996, akichukua nafasi ya Bruce Rioch aliyefukuzwa mwezi Agosti mwaka 1996. Arsene Wenger jana amevunja rekodi ya Mscotland, Alex Ferguson katika Ligi Kuu ya England  Katika kipindi chote hicho, Wenger ameshinda mataji 17 Arsenal, matatu ya Ligi Kuu ya England misimu ya 1997–1998, 2001–2002 na 2003...

DAWA BORA YA NGUVU ZA KIUME NA MAUMBILE MADOGO

Picha
TATIZO hili limekuwa likiwaathiri watu wengi sana kisaikolojia, hasa baada ya kujiona wapo tofauti sana na wengine. Kwa kawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia nchi 6-8, ambapo upungufu wa vichocheo hivi huchochoe ukuaji wa uume change ambalo hushambulia  nerve ambayo uharibu kabisa ukuaji wa uume 3, ngiri punyeto , ambayo huathiri misuri ya uume nguri ambayo huleta maumivu ya tumbo kunguruma na kujaa gesi, korodani moja kuvimba, kutopata choo vizuri, sababu hizi na nyinginezo hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba na mara nyingi hata nguvu za kiume(hamu ya tendo) hupungua na kwisha kabisa. NHESHA ni dawa inayozalisha na kufanya uume kukua na kuongezeka . 3POWER ni dawa bora ya kurudisha nguvu za kiume, hukutia hamu ya kurudia tendo la ndoa zaidi pasipo kuchoka, pia itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa zaidi ya dakika 15 kwa mtumiaji.

Serikali Yatoa Maagizo Kwa Hospitali Zote Nchini

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amevitaka vituo vyote vya Afya Nchini pamoja na hospitali za Wilaya kutengeneza bustani za kupumzikia wagonjwa wanaosubiria matibabu.  “Hili agizo liende kwa Vituo vyote vya Afya Nchini pamoja na Hospital za Wilaya zilizoko chini ya TAMISEMI kuhakikisha wanatekeleza maelekezo haya katika maeneno yote, nataka hospitali iwe sehemu ya kutoa faraja kwa mgonjwa kwa kupata huduma nzuri lakini pia kusubiria huduma hiyo katika mazingira yanayovutia”, amesema Waziri Jafo. Waziri Jafo ameyasema hayo wakati akikagua Ujenzi wa miundombinu ya Afya katika Kituo cha Afya Makole kilichopo Manispaa ya Dodoma na kuutaka uongozi wa Kituo hicho kutenegenza bustani ya kisasa pamoja na kupanda miti ya kutosha ili kutunza mazingira. “Hivi ndio ninavyotaka wataalamu wangu kujiongeza katika baadhi ya maeneo mfano hapa mmejenga Maabara kubwa kulingana na wingi wa wagonjwa mnaowahudumia kwa siku, sio k...

Obama amgaragaza Trump kura za maoni

Picha
Tukiwa tunaelekea kumaliza mwaka 2017 tunayo stori kuhusiana raia wa Marekani kwa mara nyingine wamempigia kura Barack Obama na Hillary Clinton kama mwanaume na mwanamke wanaopendwa zaidi nchini humo katika utafiti wa Gallup 2017. Utafiti huo umefanywa kwa njia ya simu kuanzia Jumatatu December 4 hadi Jumatatu ya December 11, 2017 ambapo zilikuwa sampuli za watu wazima 1,049 waliopigiwa simu bila kufuata utaratibu wowote katika majimbo yote ya Marekani na Wilaya ya Columbia. Obama amepata asilimia 17% ya kura  wakati Trump akipata 14%, kwa upande wa wanawake Hillary Clinton amepata 9% kura huku mke wa Obama, Michelle akipata  7%. Bi Clinton ameshinda katika utafiti huo mara 22 na ndiye amewahi kushinda mara nyingi zaidi katika utafiti huo nchini Marekani. Obama alishinda hadhi hiyo miaka yote alipokuwa Rais na hata baada ya kuondoka madarakani. Baadhi ya marais waliopoteza hadhi hiyo ni Harry Truman in 1946-1947 na 1950-1952, Lyndon Johnson mwaka 1967-1968, Richard Nixon,...

Mahakama yazidi kumuweka pabaya Rais Zuma

Picha
Mahakama ya Katiba imepigilia msumari wa mwisho kuhusu kashfa  inayomkabili Rais wa nchi hiyo, Jacob Zuma, ya kutumia fedha za umma kukarabati makazi yake kwa kulitaka bunge kumuwajibisha. Mahakama ya Katiba ya Afrika Kusini, imetoa uamuzi  huo leo na kusema  kuwa bunge lilishindwa kumwajibisha Rais Jacob Zuma kutokana na kashfa ya kutumia fedha za umma, kukarabati makazi yake binafsi, ya Nkandla. Hivyo mahakama imetaka bunge kuanza mchakato wa kumtoa madarakani kiongozi huyo.  Uamuzi huo ni pigo la mwisho  la kimahakama, katika kashfa  inayomkabili Zuma, ambaye pia anakabiliwa na shinikizo kubwa kutoka kwa umma akitakiwa kujiuzuliu wadhifa wake katika nchi hiyo iliyo na neema ya uchumi wa viwanda, kabla ya uchaguzi wa 2019.  Hata hivyo haikuwekwa wazi mara moja ni hatua gani bunge litachukua. Akitoa uamuzi huo leo, Jaji Chris Jafta alisema wamejiridhisha kuwa bunge halikutimiza wajibu wake. Uamuzi huo uliungwa mkono na wengi mahakamani hapo na uli...

Wenger; Mourinho acha kulilia kuhusu gharama za usajili

Picha
Jose Mourinho wa Man­chester United. KOCHA wa Arsenal, Ar­sene Wenger amesema Jose Mourinho wa Man­chester United anatakiwa kupambana na hali yake na kuacha kulialia kuhusu ghar­ama za usajili uliofanywa na Manchester City. Mara baada ya sare ya ma­bao 2-2 dhidi ya Burnley, Mourinho alisema kiasi cha pauni milioni 300 alichotumia kusajili tangu msimu uliopita hakitoshi kupambana na Man City kwa kuwa wao wametu­mia zaidi ya pauni milioni 360 kusajili. Akizungumzia sual hilo, Wenger ambaye mara kad­haa amewahi kukwaruzana na Mourinho, amesema kupambana na timu zinazotumia gharama kubwa kusajili ni jambo la kawaida kwake na hata Mourinho anatakiwa kuzoea. Ar­sene Wenger KOCHA wa Arsenal, Ar­sene Wenger amesema Jose Mourinho wa Man­chester United anatakiwa kupambana na hali yake na kuacha kulialia kuhusu ghar­ama za usajili uliofanywa na Manchester City. Mara baada ya sare ya ma­bao 2-2 dhidi ya Burnley, Mourinho alisema kia...

UKWELI Kuhusu kukamatwa ASKOFU KAKOBE

Picha
Ukweli kunaswa Askofu Kakobe LICHA ya kutokiri moja kwa moja juu ya taarifa zinazosambaa mitandaoni kuhusu kumkamata Askofu Zakaria Kakobe wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship ( FGFC ) lililoko Mwenge jijini Dar es Salaam, Jeshi la Polisi limesema ni lazima litamhoji kiongozi huyo wa kiroho . Kuhojiwa huko kumetokana na kauli yake dhidi ya serikali aliyoitoa wakati wa ibada ya Krismasi. Jana, kulienea taarifa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kueleza kwamba askofu huyo alitiwa mbaroni jana asubuhi na askari wa Jeshi la Polisi huku sababu za kukamatwa zikielezwa kuwa ni ujumbe alioutoa wakati wa mahubiri yake ya ibada ya Krismasi. Akizungumza na Nipashe jana kuhusiana na ukweli wa taarifa za kutiwa mbaroni kwa Askofu Kakobe, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, alisema kuwa ni kweli walishakuwa katika harakati za kumkamata. "Ametoa maneno ya kashfa katika mahubiri yake, lakini sina taarifa kama a...

Atoa Ujumbe kwa Vijana na Watanzania MO DEWJI

Picha
Bilionea anayemiliki kampuni kubwa ya Mohammed Enterprises nchini (MeTL), Mohammed Dewji `Mo' amefunguka na kutoa ujumbe wake kwa vijana kuelekea mwaka 2018 na kuwataka vijana na Watanzania kiujumla kuacha kulalamika mwaka 2018. Dewji katika ujumbe wake huo alioutoa kupitia mitandao yake ya kijamii amewashi Watanzania kama wanaona hawapendezwi na kitu fulani njia nzuri ni kukibadili kitu hicho na kuacha kulalamika kwani hakutaweza kubadili jambo lolote lile. "Kama hupendi kitu fulani, (jaribu) kibadilishe! Unataka kupunguza uzito? Badilisha milo yako, fanya mazoezi. Unataka kukutana na watu wapya? Toka nje, tembea na jichanganye na watu wengine! Kumbuka kulalamika hakubadilishi jambo usilolipenda!" alisisitiza Dewji

Waziri Wa Ardhi Atoa Onyo Kali kwa Vishoka wa Ardhi

Picha
Serikali imekemea baadhi ya wawekezaji wanaotumia vibaya jina la Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kuwatoa wananchi katika maeneo yao kwa kisingizio cha kupewa kibali na wizara hiyo wakati sio kweli. Kauli hiyo imetolewa na Waziri mwenye dhamana ya Wizara ya Ardhi William Lukuvi ambapo amewaonya baadhi ya wawekezaji ambao wameonekana kushirikiana na baadhi ya watumishi wa serikali katika kunyang'anya haki za wananchi kitendo ambacho amesema kwa utawala wa serikali hii ya awamu ya tano hakina nafasi. Ameongeza kwamba, kwa sasa serikali inaendelea na zoezi la kurudisha ardhi ya wananchi mikononi mwao bila ya gharama yeyote na kwa yale maeneo ambayo yatabainika kuwa na ukiukwaji wa umiliki watayarudisha kwa wenyewe ili kuendelezwa. Mh. Lukuvi amesema zoezi la utambuzi wa umiliki wa maeneo na urasimishaji ni endelevu kwa mikoa yote nchini lengo ni kujua maeneo yanayomilikiwa kihalali na kumaliza migogoro ya ardhi ambayo imeonekana bado ni changamoto kwa maeneo mengi...

Waziri Wa Ardhi Atoa Onyo Kali kwa Vishoka wa Ardhi

Picha
Serikali imekemea baadhi ya wawekezaji wanaotumia vibaya jina la Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kuwatoa wananchi katika maeneo yao kwa kisingizio cha kupewa kibali na wizara hiyo wakati sio kweli. Kauli hiyo imetolewa na Waziri mwenye dhamana ya Wizara ya Ardhi William Lukuvi ambapo amewaonya baadhi ya wawekezaji ambao wameonekana kushirikiana na baadhi ya watumishi wa serikali katika kunyang'anya haki za wananchi kitendo ambacho amesema kwa utawala wa serikali hii ya awamu ya tano hakina nafasi. Ameongeza kwamba, kwa sasa serikali inaendelea na zoezi la kurudisha ardhi ya wananchi mikononi mwao bila ya gharama yeyote na kwa yale maeneo ambayo yatabainika kuwa na ukiukwaji wa umiliki watayarudisha kwa wenyewe ili kuendelezwa. Mh. Lukuvi amesema zoezi la utambuzi wa umiliki wa maeneo na urasimishaji ni endelevu kwa mikoa yote nchini lengo ni kujua maeneo yanayomilikiwa kihalali na kumaliza migogoro ya ardhi ambayo imeonekana bado ni changamoto kwa maeneo mengi...

TFF yakanusha Kuzuia Mashindano

Picha
Shirikisho la soka nchini TFF limekanusha taarfia zinazosambaa zikipotosha kauli ya Rais Wallace Karia kuhusu kuzuia mashindano ya soka yasiyo rasmi. Taarifa ya TFF imeeleza kuwa watu wanamnukuu vibaya Rais Karia kwani hakusema shirikisho hilo linafuta mashindano bali zinaandaliwa kanuni ambazo zitatakiwa kufuatwa na waandaaji wa mashindano hayo. “TFF inaandaa kanuni ili mashindano yote ya aina hiyo yakidhi vigezo katika utaratibu mzuri na watapata vibali kupitia FA Wilaya na Mikoa baada ya kutimiza vigezo vitakavyowekwa”, imeeleza sehemu ya taarifa ya TFF. Mapema jana Karia mbele ya wahariri wa habari za michezo, alieleza dhamira hiyo ya TFF katika kuweka utaratibu utakaoboresha mashindano hayo.

Askari Jeshi la Police Amuua Mpenzi Wake

Picha
ASKARI wa kike wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ ) Kikosi cha 514 KJ Makambako mkoani Njombe , ameuawa kwa kupigwa risasi na mchumba wake ambaye ni askari wa Jeshi la Polisi , Inadaiwa kuwa tukio hilo , lilitokana na kuibuka ugomvi kati yao . Inadaiwa askari huyo namba H 2299 Zakaria Dotto , alimpiga risasi mbili mchumba wake, Neema Masanja (25) mkazi wa Mtaa wa Jeshini Kata ya Maguvani Halmashauri ya Mji wa Makambako mkoani Njombe, baada ya kuibuka ugomvi kati yao saa 12 jana alfajiri. Wakizungumza katika eneo la tukio, majirani wa marehemu walisema majira ya alfajiri walisikia risasi zikirindima katika chumba cha marehemu na walipoangalia nje ya nyumba hiyo walimuona mdogo wake akimkimbiza mtu ambaye hawakumuona sura. Mmiliki wa nyumba hiyo ambayo marehemu alikuwa amepanga, Asty Lusambo, alisema alisikia kishindo cha risasi na alipofungua dirisha akiwa na mkewe, walimuona mdogo wa marehemu akimkimbiza mtu. Mke wa Lusambo, Sophia Manyi...

LIVERPOOL YAMSAJILI VAN DIJIK KWA DAU LA REKODI YA DUNIA

Picha
KLABU ya Liverpool imevunja rekodi ya dunia kwa dau la usajili wa beki, Virgil van Dijk Pauni Milioni 75. Na mchezaji huyo atatambulishwa rasmi kuwa mali ya Liverpool Jumatatu dirisha la usajili la Januari litakapofunguliwa. Van Dijk alifanyiwa vipimo vya afya pwani ya kusini Jumatano na Southampton wakishirikishwa baada ya makubaliano ada ya uhamisho. Amesaini mkataba wa mshahara wa zaidi ya Pauni 180,000 kwa wiki ambao utamalizika Juni 2023. Liverpool imesajili mchezaji ambaye itaruhusiwa kumtumia kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa katika sehemu ya pili ya msimu - na anaweza kuanza kucheza hata dhidi ya Everton kwenye Kombe la FA Raundi ya Tatu Ijumaa ijayo.  Virgil van Dijk atatambulishwa rasmi Jumatatu kuwa mali ya Liverpool baada ya kukamilisha uhamisho wa Pauni Milioni 75 PICHA ZAIDI GONGA HAPA   Van Dijk aliyekabidhiwa jezi namba nne, mustakabali wake ulikuwa haueleweki baada ya Mholanzi huyo kuachwa katika kikosi cha Southampt...

Simba ' Yanga Yapangua Mapinduzi Cup

Simba, Yanga, Azam na Singida United zimeipangua ratiba ya Mapinduzi Cup inayotarajia kuanza December 29, 2017 kutokana na ratiba ya ligi kuu Tanzania bara ambayo itakuwa ikiendelea wakati mechi za kwanza za hatua ya makundi ya kombe hilo zitakapokuwa zikianza huku visiwani Zanzibar. Ijumaa ya December 29, Azam watakuwa na mechi dhidi ya Stand United kwenye uwanja wa Azam Complex, Jumamosi kutakuwa na mechi tatu za VPL (Lipuli vs Tanzania Prisons, Mtibwa Sugar vs Majimaji, Ndanda vs Simba) wakati Jumapili Yanga watakuwa ugenini kucheza dhidi ya Mbao huku Singida United wao pia wakitarajia kucheza dhidi ya Njombe Mji. “Ratiba kidogo iliingia utata kwa sababu Simba, Yanga, Azam na Singida United walipangiwa ratiba ya kucheza wakati kombe la Mapinduzi litakapokuwa limeanza lakini mechi zao tumezisogeza mbele.” “Yanga wanaweza kuja tarehe 31 mwezi huu au tarehe 1 mwezi ujao, Azam watakuja mapema kwa sababu ratiba yao haiwakabi sana, Singida United na Simba nao watawahi...

PICHA HIZI HAPA NAMNA MAN CITY ILIVYOITWANGA NEWCASTLE NA KUZIDI KUCHANJA MBUGA EPL

Picha
NEWCASTLE: (5-4-1) Elliott 7.5; Yedlin 6.5, Mbemba 6.5 (Merino 77mins), Lascelles 7, Dummett 6.5, Manquilo 6; Aarons 6 (Atsu 70mins 6) Diame 6, Shelvey 6, Murphy 6; Joselu 5.5 (Gayle 61mins 6) Subs not used: Clark, Ritchie, Perez, Darlow. BOOKED: Gayle RAFA BENITEZ: 5 MANCHESTER CITY: (4-1-4-1) Ederson 6.5; Walker 6.5, Kompany 6 (Jesus 10mins 7), Otamendi 7, Danilo 6.5; Fernandinho 7.5; B Silva 7.5 (Sane 85mins), De Bruyne 8, Gundogan 7, Sterling 7.5; Aguero 7.5 (Mangala 76mins 6) Subs not used: Bravo, Adarabioyo, Toure, Diaz. GOALS: Sterling 30  PEP GUARDIOLA: 7.5 REFEREE: Andre Marriner 7 MAN OF THE MATCH: Kevin De Bruyne

YANGA Yaifuata Mbao FC kwa Tahadhari kubwa

Picha
Kikosi cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara , Yanga kinatarajia kuondoka leo jijini Dar es Salaam kwenda Mwanza tayari kuwavaa Mbao FC wikiendi hii . Yanga wanasema wako kamili kwa ajili ya mechi hiyo lakini wamesisitiza hawatakuwa na dharau wala kuigopa Mbao FC . Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga , Salum Nyika amesema wanaujua ubora wa Mbao kwa kuwa ni moja ya timu bora nchini . “ Kitu cha kwanza ujue ni timu ya ligi kuu , tunaiheshimu kama Mbao . Lakini si kwamba tunaigopa kwa kuwa tumejianda ana tuko tayari kwa mechi hiyo ,” alisema . Yanga imekuwa ikijifua bila ya Kocha wake, George Lwandamina ambaye alipata msiba wa kufiwa na mwanaye kwao Zambia.

TFF yawapiga Stop Wabunge

Picha
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania ( TFF ), Wallace Karia amefuta mashindano yoyote ya soka yaliyo nje ya mfumo wa shirikisho hilo isipokuwa tu kwa kibali maalum . Karia ameyasema hayo leo katika Mkutano wake na Wahariri wa vyombo vya Habari nchini uliofanyika kwenye hoteli ya Sea Scape, Kunduchi mjini Dar es Salaam leo . Karia amesema kwamba mashindano ya soka yasiyo rasmi kama ambayo huandaliwa na wanasiasa majimboni na hata na baadhi ya taasisi na wadau, yamekuwa yakipewa umuhimu mkubwa kuliko mashindano rasmi ya TFF zikiwemo ligi. Karia amesema wakati umefika sasa Wabunge na wanasiasa kwa ujumla watoe fedha kuzidhamini timu za majimboni mwao badala ya kuanzisha mashindano ya ng’ombe na mbuzi. Mapema kabla ya kuanza kutoa hotuba yake hiyo, Rais Karia alisaini mkataba wa udhamini wa jezi na kampuni ya Macron.  Mkataba huo utakaohusisha timu zote za taifa zikiwemo za vijana na wakubwa kwa wanawake na wanaume utakuwa na thamani...

Watumishi Kuorodhesha Mali Zao

Picha
Kamishna wa Maadili Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu, Harold Nsekela, amesema sheria ya maadili ya viongozi wa umma kupitia kifungu cha 9 (1) (b) inamtaka kiongozi wa ummma kila ifikapo mwisho wa mwaka kupeleka kwa kamishna wa maadili tamko la maandishi katika hati rasmi inayoorodhesha mali au rasilimali zake na za mwenza wake, watoto wake wenye umri usiozidi miaka 18 na ambao hawajaoa au kuolewa. Akizungumza jijini Dar es Salaam, Nsekela ameeleza kwamba mwisho wa kupokea fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni mwisho wa kupokelewa ni Desemba 31, 2017 na kwa mtu ambaye bado hajapata fomu hizo anaweza kuingia tovuti ya sekretarieti hiyo ya www.ethicsssecretariat.go.tz. “Kwa kuzingatia kifungu cha 9(1) (a) na (c) cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, viongozi wapya wanaochaguliwa au kuteuliwa wanatakiwa kujaza fomu hizo na kuzirejesha kwa kamishna wa maadili ndani ya siku thelathini baada ya kupewa wadhifa. Kiongozi anapofika mwisho wa kutumikia wadhifa...

Trump Atuma Ujumbe Zimbabwe

Picha
Rais wa Marekani , Donald Trump amesema utawala wake uko tayari kufanya kazi na Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe lakini amesisitiza kuwa hilo litawezekana iwapo taifa hilo litaacha kuendelea kutumia Dola ya Marekani . Amelitaka kutotumia dola hiyo na badala yake lianzishe mfumo utakaohakikisha linatumia sarafu yake ya Zimbabwe. Kwa miaka mingi Zimbabwe ilikoma kutumia sarafu yake na kutumia ile ya Marekani hali ambayo ilikosolewa vikali na wanauchumi. Duru za habari zimenukuu Waziri anayeshughulikia masuala ya Afrika, Don Yamamoto akisema Zimbabwe anapaswa kudhibiti uchumi wake na siyo kuendelea kutegemea sarafu ya nje. “ Hivi leo hali ya uchumi wa Zimbabwe ni mbaya. Taifa hili linaagiza chakula kutoka nje, taasisi zake za kiuchumi hazipo katika hali nzuri. Wamelazimika kutumia Dola ya Marekani. Hawapaswi kutegemea sarafu ya Marekani au taifa lingine lolote la kigeni. Haya ndiyo mageuzi tunayopenda kuona yakifanyika sasa,” amenu...

NAFASI YA MBOWE YAZUNGUMZIWA

Picha
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM ), Humphrey Polepole amefunguka na kusema wao CCM hawajawahi kuzungumzia juu ya Mwenyekiti wa CHADEMA , Freeman Mbowe kushikilia nafasi hiyo kwa muda mrefu bila kufanya mabadiliko . Polepole amesema hayo wakati akimjibu moja ya mwananchi ambaye alitaka kufahamu kuwa ni kwanini Wanachama wa CCM wao ndiyo wamekuwa wakipiga sana kelele juu ya nafasi ya Mwenyekiti wa CHADEMA, ndipo hapo alipofunguka na kusema hawajawahi kuzungumzia hilo na kwa kuwa hakuna mwengine ambaye wanaona anafaa basi aendelee Mbowe kwa miaka 100. "Msemaji wa CCM ni mimi na hatujawahi kutoa kauli hiyo, huyo Mwenyekiti maadamu hakuna mwingine anayefaa kuliko yeye aendelee tu miaka 100" aliandika Polepole Mbali na hilo Polepole ameulalamikia upinzani wa Tanzania kwa sasa na kusema umekuwa wa kupinga kila kitu hata kwa mambo mazuri wenyewe umekuwa ukipinga tu hivyo amefananisha kuwa huenda hiyo ni siasa...

Mwakyembe Amlilia Mayage

Picha
Waziri wa Habari , Utamaduni , Sanaa na Michezo , Dk Harrison Mwakyembe amesema amepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha mwanahabari nguli Mayage S. Mayage . Mayage alifariki dunia jana Jumatatu Desemba 25,2017 asubuhi katika Hospitali ya Mbweni Misheni jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu . Kaimu mkuu wa kitengo cha mawasiliano serikalini katika wizara hiyo, Octavian Kimario katika taarifa leo Jumanne Desemba 26,2017 amesema Dk Mwakyembe ameeleza kuwa tasnia ya habari imepoteza mmoja wa wanahabari wazuri wenye uelewa mkubwa katika uchambuzi wa masuala ya kisiasa na kijamii nchini. Waziri Mwakyembe ametoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na wanahabari wote nchini. Pia, amewaombea Mungu awape faraja katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao. Mayage aliwahi kuwa mhariri wa siasa katika kampuni ya Raia Mwema Ltd na kaimu mhariri katika kampuni ya Habari Corporation Ltd. Hadi kifo chake Mayage alikuwa mwandishi mwandamiz...

Yanga yaifunga Mdomo Simba

Picha
Ushindi wa Yanga wa mabao mawili 2-0 dhidi ya Reha FC imedhihirisha kuwa timu hiyo iliingia uwanjani ikiwa na ari ya kupata ushindi . Timu hiyo ya Jangwani ilifanya mashambulizi kadhaa ambayo wapinzani wao walijitahidi kufanya hivyo pia, lakini umakini wa makipa wa pande zote uliwafanya kuingia kipindi cha pili kwa kila timu bila kuona lango la mwenzake . Mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru umedhihirisha kuwa timu za Ligi Daraja la Pili siyo za kubeza kutokana na kuonyesha soka la kuvutia. Wiki hii Simba ambao walikuwa mabingwa mtetezi, walifungwa na Green Warriors timu ya Ligi Daraja la Pili mchezo ulioisha kwa kupigiana mikwaju ya penalti 4-3. Yanga imefanikiwa kuvuka hatua raundi ya tatu ya michuano hiyo ya Kombe la FA kwa mabao yaliyowekwa wavuni na Amissi Tambwe na Pius Buswita.

Agizo la Raisi Laanza Kutekelezwa

Picha
Waziri wa Habari, Utamaduni, sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe amesema wizara imeanza kutekeleza agizo la Rais Magufuli juu ya baadhi ya wasanii ambao wanadaiwa kuwa chanzo cha kuporomoka kwa maadili ya kitanzania. Waziri Mwakyembe amesema kwamba kitendo cha Rais Magufuli kusema suala hilo, kimewapa nguvu ya kuzidi kupambana na wasanii, ambapo hapo awali walikuwa wakiwagusa huwajia juu na kulalamika. "Pale tunapoona kuna ukwiukwaji, tufumbe macho tusijali malalamiko yanavyokuja kutolewa, maana ukiwagusa wasanii walikuwa wanakuja juu sana, lakini tunashukuru mkuu wa nchi kulisemea hilo, basi na sisi tumeongezewa nguvu basi hatutaachia suala hilo kuendelea kuharibu vizazi vyetu", amesema Waziri Mwakyembe. Hivi karibuni Rais Magufuli alizitaka mamlaka husika kuwachukulia hatua wasanii wanaovaa nusu utupu kwenye kazi zao za sanaa ambazo zingine huonyeshwa kwenye television, ambazo amedai hazina maadili na zinadhalilisha utamaduni wetu na kuharibu kizazi kijacho.

Magonjwa ya kuku Wetu

1. Ugonjwa wa Mdondo: Ugonjwa huu huathiri kuku katika umri wowote na unapoingia kwenye kundi huweza kuua idadi kubwa ya kuku hao hadi kufikia asilimia tisini. Ndege wakubwa hustahimili kidogo kuliko wale wadogo kwasababu ya usugu mwilini (body immunity) uliojengeka kwa muda mrefu zaidi. Ugonjwa huu husababishwa na kimelea cha kirusi kiitwacho Paramyxo viridae na huenezwa kwa njia ya hewa na kugusana. Dalili zake: Kukohoa na kuhema kwa shida Ute hutoka mdomoni na puani Kuku walioathirika hupata kizunguzungu. Kuharisha uharo wa kijani na njano Kuzubaa, kusinzia na mabawa kushuka Baada ya siku 2 kuku hupindisha shingo Kuvimba macho Kuzunguka Kuku hutaga mayai hafifu. 90% ya kuku huweza kufa Tiba: Ugonjwa huu hauna dawa. Kinga: Kuchanja; Chanja kuku wako kila baada ya miezi mitatu /na mara nne kwa mwaka. Kuna chanjo aina mbili za ugonjwa huu, nazo ni; 1. Lasota : Chanjo hii hutolewa katika dawa yenye umbile la kidonge kimoja kimoja ambacho kina dozi ya kuku 1000 na huw...

Faham Namna ya kuishi na Mpenzi anaekupendea Hela (Pesa)

Picha
HAPA   tunazungumza kuhusu mapenzi kama kawaida yetu . Leo nimekuja na mada ambayo naamini itawagusa wengi . Marafiki zangu , kusaidia katika mapenzi ni jambo zuri tena lenye mantiki sana. Suala la kusaidiana si la upande mmoja . Linaweza kuwa kwa wote , kwa mwanaume au mwanamke . Ni kati ya nguzo muhimu katika mapenzi , lakini kwa bahati mbaya kuna wale ambao   wamekuwa na tabia ya kupenda sana fedha! Unajua wenzi wanajuana kulingana na wanavyoishi, hivyo ni rahisi sana kumgundua mwenzako kama anapenda sana fedha au ni kweli ana tatizo linalohitaji msaada wako. Hii ni kasoro, lakini haimaanishi kwamba ndiyo sababu ya kuachana. Katika mada hii ipo dawa ya namna ya kudumu katika mapenzi motomoto na mwenzi wa aina hii. Imekuwa ni kawaida kumsikia msichana akitamba mbele ya wasichana wenzake kwa kusema: “Mimi nina kibuzi changu bwana kila ninachotaka kinanipa, kinajua kisiponipa nakitosa tu, yaani nakichuna kama sina akili nzuri....

AZAM YAZIDI KUSONGA MBELE

TIMU ya Azam FC , imeanza vema michuano ya Azam Sports Federation Cup ( ASFC ) baada kuipiga Area C United mabao 4-0, mchezo uliomalizika usiku huu kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi , Dar es Salaam. Azam FC ilionyesha kuwa imedhamiria kuibuka na ushindi katika mchezo huo baada ya kufanya shambulizi kali dakika ya pili tu kufuatia Enock Atta kuwazidi ujanja mabeki wa Area C na kupiga mpira mzuri wa faulo uliomkuta Paul Peter, aliyepiga kichwa kilichogonga mwamba wa pembeni kabla ya mabeki kuokoa hatari hiyo. Azam FC kwa ushindi huo mnono, ni kama imetoa zawadi ya Sikukuu ya Krismasi kwa mashabiki wake kutokana na mchezo huo kuwa wa mwisho kwa timu hiyo kabla ya maadhimisho ya sikukuu hiyo kufanyika keshokutwa Jumatatu na Jumanne. Alikuwa ni kiungo Salmin Hoza, aliyeanza kufungua mlango wa mabao kwa Azam FC dakika ya 17 baada ya kupiga shuti kali nje kidogo ya eneo la 18 akimalizia mpira wa faulo aliotengewa na winga Enock Atta Agyei, ambay...

Sahau kuhusu matokeo lakini haya unapaswa kuyajua baada ya El Clasico ya leo

Picha
Lioneil Mesai alifunga bao lililomfanya kufikisha mabao 25 katika El Clasico na hilo likiwa bao lake la 50 mwaka huu, Messi anakuwa amefunga mabao 50 kwa miaka 6 kuanzia 2010 akiwa ameacha 2013 tu. Mchezo huu uliisha kwa sare ya bila kufungana katika kipindi cha kwanza na hii ikiwa mara ya kwanza kwa Barca kushindwa kufunga bao la katika kipindi cha kwanza Santiago Bernabeu tangu April 2011 katika La Liga. Goli la kwanza la Barcelona lilifungwa na Luis Suarez likiwa ni bao lake la 5 katika El Clasico 7 alizocheza na huku Real Madrid wakishindwa kuweka clean sheet katika michezo ya El Clasico 7 iliyopita. Lioneil Messi alimpoteza Cristiano Ronaldo hii leo kwani ukiachana na bao alilofunga lakini alikamilisha pasi 50/57,akitengeneza chance 9 na mashuti 3 on target, huku CR7 akikamilisha pasi 22/27,akitengeneza chance 1 na shuti 1 on target. Bao la 3 la Barcelona lilifungwa na Alex Vidal dakika ya mwisho na kuifanya Barcelona kwa mara ya kwanza katika historia kushinda michezo 3 mful...

Waziri wa Ulinzi Awatembelea Wanajeshi DRC CONGO

Picha
Ikiwa zimepita siku 16 tangu kuuawa kwa askari 14 wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) waliokuwa kwenye  oparesheni ya ulinzi wa amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Waziri wa Ulinzi wa Tanzania Husssein Mwinyi  amewatembelea wanajeshi wa Tanzania waliopo nchini humo. Mwinyi alifika nchini humo December 22, 2017 ambapo  alipowatembelea Wanajeshi wa Tanzania wanaoshiriki katika kikosi cha kimataifa cha kulinda amani mashariki ya Congo, na kuwatembelea wanajeshi waliojeruhiwa wakati wa shambulizi la December  7, 2017. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Beni, Mwinyi ametoa wito wa kudumisha ushirikiano kati ya pande zote zinazoshiriki katika kuleta amani Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). Wanajeshi 14 wa Tanzania wa kikosi maalum cha nchi za Kusini mwa Afrika SADC waliuawa na wengine 44 kujeruhiwa wakati wa majibizano ya risasi na waasi wasiojulikana katika kambi yao huko Semulik, karibu na mji wa Beni.

Acacia yaendelea kuitesa Serikali

Picha
Wakati Serikali ikipambana kuhakikisha Wananchi wake wanapata ajira, Kampuni ya Uchimbaji Madini ya ACACIA imetangaza kupunguza wafanyakazi wake zaidi ya 3,000. Hatua hiyo imesababishwa na gharama za uendeshaji kuwa kubwa kutokana na hali ya ukata kuikumba kampuni hiyo. Aidha hatua hiyo imepelekea kupungua kwa shughuli za uzalishaji katika migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi iliyopo wilayani Kahama, Mkoani Shinyanga. Tanzania na Barrick Gold Corporation inayomiliki migodi hiyo kwa ubia na ACACIA zilifikia makubaliano tarehe 19 Oktoba, 2017 na kutiliana saini mkataba wa kutekeleza mwelekeo mpya wa namna kampuni hiyo itakavyoendesha biashara ya madini ya dhahabu yanayochimbwa katika migodi yake hapa nchini.

Lwandamila Aendelea kubaki Zambia

Picha
Kocha mkuu wa mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania bara klabu yaYanga , Mzambia George Lwandamina amepata msiba baada ya kufiwa na mtoto wake wa kiume . Taarifa ya Yanga imeeleza kuwa mtoto huyo aitwaye Mofya Lwandamina amefariki jana jioni huko nyumbani kwao Zambia. “ Kwa wana Yanga na wadau wote wa soka , kocha wetu George Lwandamina amepata msiba , amefiwa na mtoto wake wa kiume jana huko Zambia”, imeeleza taarifa ya klabu . Kocha George Lwandamina ataendelea kuwa kwao Lusaka kwa muda mrefu , ikumbukwe aliondoka Dar es Salaam wiki iliyopita kwenda nyumbani kwa ajili ya kuhudhuria mahafali ya mwanawe wa kike , Nasanta Lwandamina aliyehitimu Stashahada ya Afya ya Jamii katika Chuo Kikuu cha NRDC . Yanga SC kesho watakuwa kwenye Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam kumenyana na   Reha FC katika hatua ya 64 Bora ya kombe la shirikisho ( ASFC ).

Huyu Ndie Mwanamke Tajiri Zaidi Duniani

Picha
Baada ya Mfaransa Liliane Bettencourt , 94, kufariki mwezi uliopita , ambaye alikuwa mmiliki wa maduka ya bidhaa za urembo L’Oreal , ambaye ndiye aliyekuwa mwanamke tajiri zaidi duniani akiwa na utajiri wa Dola za Marekani bilioni 39.5, sawa na takriban Tshs trilioni 94, mikoba yake imepata mrithi . Mikoba hiyo imechukuliwa na Alice Walton, ambaye ana mali ya jumla ya Dola za Marekani bilioni 33.8. Kwa jumla, alishikilia nambari 17 katika orodha ya mabilionea wa Forbes waliotangazwa mapema mwaka huu. Hadi kufikia mwezi November mwaka huu Alice Walton ametajwa kuwa na utajiri wa Dola bilioni 45.9 sawa na Tsh za Tanzania trilioni 108. Watson ambaye ni binti pekee wa mwanzilishi wa maduka ya Wal-Mart Sam Walton, ndiye mwanamke tajiri zaidi Marekani na utajiri wake unatokana na hisa zake katika Wal-Mart pamoja na malipo ya mgawo wa faida.