TAARIFA MPYA
Mwakyembe Amlilia Mayage
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amesema amepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha mwanahabari nguli Mayage S. Mayage.
Mayage alifariki dunia jana Jumatatu Desemba 25,2017 asubuhi katika Hospitali ya Mbweni Misheni jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.
Kaimu mkuu wa kitengo cha mawasiliano serikalini katika wizara hiyo, Octavian Kimario katika taarifa leo Jumanne Desemba 26,2017 amesema Dk Mwakyembe ameeleza kuwa tasnia ya habari imepoteza mmoja wa wanahabari wazuri wenye uelewa mkubwa katika uchambuzi wa masuala ya kisiasa na kijamii nchini.
Waziri Mwakyembe ametoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na wanahabari wote nchini. Pia, amewaombea Mungu awape faraja katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao.
Mayage aliwahi kuwa mhariri wa siasa katika kampuni ya Raia Mwema Ltd na kaimu mhariri katika kampuni ya Habari Corporation Ltd.
Hadi kifo chake Mayage alikuwa mwandishi mwandamizi katika kampuni ya Tazama Newspapers Ltd.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni
TAFADHARI !!
- Tumia Lugha Nzuri Kutoa Maoni
Usitumie kauli za Karaha AU Zenye Kukela :
C.E.O
Gneous OG