TAARIFA MPYA

Madhara ya Chai na Kahawa Kiafya

Picha
CAFFEINA/KAFEINA. Kafeina ni nini?: 1. Kafeina ni madawa ya kulevya kundi la ‘Stimulants drugs’. Utashangaa. Habari ndiyo hiyo. Hii ndiyo sababu kwa mtu aliyezoea kunywa chai hii kila siku au kahawa, siku asipokunywa kichwa humuuma, ni kwa sababu amekuwa mtegemezi au teja wa kafeina. Kafeina ni kiungo mhimu karibu katika soda zote zenye rangi nyeusi; Coca-cola, Pepsi, Sayona nyeusi, Azam cola na kadharika. Kafeina huongezwa pia katika Red bull, Malta na katika baadhi ya dawa za kupunguza maumivu mwilini. Kwahiyo Kafeina ambayo hupatikana katika chai na kahawa ni aina mojawapo ya madawa ya kulevya. 2. Kafeina ni kikojoshi (diuretics). Kafeina ni dawa ya kukufanya ukojowe. Ukinywa kikombe kimoja cha kinywaji chenye kafeina yaani chai au kahawa, basi muda si mrefu utaenda kukojoa vikombe viwili. Kwa sababu kafeina ni taka isiyotakiwa mwilini, mwili utafanya kila uwezalo ikibidi ujikamuwe wenyewe kupata maji ya ziada kuweza kuitoa kafeina hii uliyoinywa kwa kisingizio ch...

Mahakama yazidi kumuweka pabaya Rais Zuma


Mahakama ya Katiba imepigilia msumari wa mwisho kuhusu kashfa  inayomkabili Rais wa nchi hiyo, Jacob Zuma, ya kutumia fedha za umma kukarabati makazi yake kwa kulitaka bunge kumuwajibisha.

Mahakama ya Katiba ya Afrika Kusini, imetoa uamuzi  huo leo na kusema  kuwa bunge lilishindwa kumwajibisha Rais Jacob Zuma kutokana na kashfa ya kutumia fedha za umma, kukarabati makazi yake binafsi, ya Nkandla. Hivyo mahakama imetaka bunge kuanza mchakato wa kumtoa madarakani kiongozi huyo.

 Uamuzi huo ni pigo la mwisho  la kimahakama, katika kashfa  inayomkabili Zuma, ambaye pia anakabiliwa na shinikizo kubwa kutoka kwa umma akitakiwa kujiuzuliu wadhifa wake katika nchi hiyo iliyo na neema ya uchumi wa viwanda, kabla ya uchaguzi wa 2019.  Hata hivyo haikuwekwa wazi mara moja ni hatua gani bunge litachukua.

Akitoa uamuzi huo leo, Jaji Chris Jafta alisema wamejiridhisha kuwa bunge halikutimiza wajibu wake. Uamuzi huo uliungwa mkono na wengi mahakamani hapo na ulionyeshwa mubashara katika luninga.

"Kwa  mtazamo wetu, mchakato wa suala hilo haukuendana na kifungu cha 89. Bunge lilijadili  na kuchagua kupiga kura ya kutokuwa na imani.-halikujiridhisha kuwa uvunjwaji wa katiba, katika suala hilo, ulikuwa umejikita katika kutafakari   kifungu hicho. Hivyo basi, tunahitimisha kuwa bunge halikuweza kumwajibisha rais kutokana na makosa yake kama inavyotakiwa katika kifungu cha 89,``alisema

Jafta alisema imeelezwa vyema, katika kifungu cha 89 kinachodokeza wajibu wa bunge kutunga sheria hasa zile za kumuondoa rais madarakani.  Akaongeza kuwa kwa kushindwa kujumuisha sheria hizo,  bunge limeshindwa kutimiza wajibu wake.

Chama cha mrengo wa kushoto cha Economic Freedom Fighter, na vyama vidogo vya upinzani, ndivyo vilivyopeleka suala hilo katika mahakama ya katiba.

Zuma, yupo katika nafasi  mbaya kwa sasa, baada ya makamu wa rais  Cyril Ramaphosa, kupata ushindi mwembamba na kupata  nafasi ya kukiongoza chama tawala cha Zuma, ANC wiki iliyopita. Hata hivyo  bado Zuma ana nafasi muhimu katika chama hicho na tayari alishapenya katika kura za kutokuwa na imani naye.

 Wakati huo huo, ANC imetoa taarifa na kusema kuwa kitapitia uamuzi huo na kujadili  madhara yake katika kikao cha Kamati kuu ya chama hicho,   kitakachofanyika, Januari 10, 2018.

Tangu Ramaphosa achaguliwe, randi ya Afrika  Kusini imekuwa dhabiti  katika siku za mwisho za mwaka. Imepanda kwa zaidi ya asilimia 10 dhidi ya dola.

Maoni

ZILIZO SOMWA MARA NYINGI

ULAJI WA MARA KWA MARA WA MBEGU ZA MABOGA HUKUKINGA NA KUKUEPUSHA NA MAGONJWA 1O MWILINI MWAKO...

Dalili 6 zitakazokuonyesha kuwa mwenzi wako ana mtu mwingine katika mahusiano

FAIDA YA JUICE YA KAROTI KATIKA MWILI WA BINADAM

DAWA BORA YA NGUVU ZA KIUME NA MAUMBILE MADOGO

AINA ZA MBOLEA & MATUMIZI YAKE KITAALAM

Madhara ya Chai na Kahawa Kiafya

Fahamu Aina 7 Za Juisi Zenye Kuondoa Sumu Mwilini

Ugonjwa wa Chango La Uzazi

Madhara Ya Kuangalia Video za Porno {Ngono} na Namna ya Kujizuia

Athari za kiafya za vyakula vyenye Wanga