TAARIFA MPYA
LIVERPOOL YAMSAJILI VAN DIJIK KWA DAU LA REKODI YA DUNIA
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
KLABU ya Liverpool imevunja rekodi ya dunia kwa dau la usajili wa beki, Virgil van Dijk Pauni Milioni 75.
Na mchezaji huyo atatambulishwa rasmi kuwa mali ya Liverpool Jumatatu dirisha la usajili la Januari litakapofunguliwa.
Van Dijk alifanyiwa vipimo vya afya pwani ya kusini Jumatano na Southampton wakishirikishwa baada ya makubaliano ada ya uhamisho.
Amesaini mkataba wa mshahara wa zaidi ya Pauni 180,000 kwa wiki ambao utamalizika Juni 2023.
Liverpool imesajili mchezaji ambaye itaruhusiwa kumtumia kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa katika sehemu ya pili ya msimu - na anaweza kuanza kucheza hata dhidi ya Everton kwenye Kombe la FA Raundi ya Tatu Ijumaa ijayo.
Virgil van Dijk atatambulishwa rasmi Jumatatu kuwa mali ya Liverpool baada ya kukamilisha uhamisho wa Pauni Milioni 75 PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Van Dijk aliyekabidhiwa jezi namba nne, mustakabali wake ulikuwa haueleweki baada ya Mholanzi huyo kuachwa katika kikosi cha Southampton cha mechi za hivi karibuni dhidi ya Tottenham na Huddersfield.
Amekuwa akitakiwa na klabu zote kubwa katika Ligi, wakiwemo vinara wa sasa, Manchester City ambao kocha wao, Pep Guardiola alikuwa anataka sana kumuongeza kwenye kikosi chake na tayari walikuwa kwenye mazungumzo na Southampton.
Klabu hizo mbili zimekuwa katika biashara nzuri tangu mwaka 2014 na Van Dijk anakuwa mchezaji wa sita kuondoka St Mary kuhamia Anfield akiwafuatia Rickie Lambert, Adam Lallana, Dejan Lovren, Nathaniel Clyne na Sadio Mane. Uhamisho wa wachezaji wote ni Pauni Milioni 168.5.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni
TAFADHARI !!
- Tumia Lugha Nzuri Kutoa Maoni
Usitumie kauli za Karaha AU Zenye Kukela :
C.E.O
Gneous OG