TAARIFA MPYA
Simba ' Yanga Yapangua Mapinduzi Cup
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Simba, Yanga, Azam na Singida United zimeipangua ratiba ya Mapinduzi Cup inayotarajia kuanza December 29, 2017 kutokana na ratiba ya ligi kuu Tanzania bara ambayo itakuwa ikiendelea wakati mechi za kwanza za hatua ya makundi ya kombe hilo zitakapokuwa zikianza huku visiwani Zanzibar.
Ijumaa ya December 29, Azam watakuwa na mechi dhidi ya Stand United kwenye uwanja wa Azam Complex, Jumamosi kutakuwa na mechi tatu za VPL (Lipuli vs Tanzania Prisons, Mtibwa Sugar vs Majimaji, Ndanda vs Simba) wakati Jumapili Yanga watakuwa ugenini kucheza dhidi ya Mbao huku Singida United wao pia wakitarajia kucheza dhidi ya Njombe Mji.
“Ratiba kidogo iliingia utata kwa sababu Simba, Yanga, Azam na Singida United walipangiwa ratiba ya kucheza wakati kombe la Mapinduzi litakapokuwa limeanza lakini mechi zao tumezisogeza mbele.”
“Yanga wanaweza kuja tarehe 31 mwezi huu au tarehe 1 mwezi ujao, Azam watakuja mapema kwa sababu ratiba yao haiwakabi sana, Singida United na Simba nao watawahi kufika kati ya tarehe 1 au 2 mwezi ujao watakuwa tayari kuanza haya mashindano.”
“Kwa hiyo tuwaombe radhi wapenzi wa mpira Zanzibar kwamba, mechi za kombe la Mapinduzi zitaanza December 29, kwa kushirikisha timu za Zanzibar pekeake (Jamhuri, Mwenge, JKU, Zimamoto, Mlandege na Taifa Jang’ombe) halafu baadaye wataungana na timu za kutoka Tanzania bara. URA wanafika Dar December 29 kawawatafika mapema siku hiyohiyo wataunganisha Zanzibar au watafika kesho yake.”
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni
TAFADHARI !!
- Tumia Lugha Nzuri Kutoa Maoni
Usitumie kauli za Karaha AU Zenye Kukela :
C.E.O
Gneous OG