TAARIFA MPYA
Serikali Yatoa Maagizo Kwa Hospitali Zote Nchini
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amevitaka vituo vyote vya Afya Nchini pamoja na hospitali za Wilaya kutengeneza bustani za kupumzikia wagonjwa wanaosubiria matibabu.
“Hili agizo liende kwa Vituo vyote vya Afya Nchini pamoja na Hospital za Wilaya zilizoko chini ya TAMISEMI kuhakikisha wanatekeleza maelekezo haya katika maeneno yote, nataka hospitali iwe sehemu ya kutoa faraja kwa mgonjwa kwa kupata huduma nzuri lakini pia kusubiria huduma hiyo katika mazingira yanayovutia”, amesema Waziri Jafo.
Waziri Jafo ameyasema hayo wakati akikagua Ujenzi wa miundombinu ya Afya katika Kituo cha Afya Makole kilichopo Manispaa ya Dodoma na kuutaka uongozi wa Kituo hicho kutenegenza bustani ya kisasa pamoja na kupanda miti ya kutosha ili kutunza mazingira.
“Hivi ndio ninavyotaka wataalamu wangu kujiongeza katika baadhi ya maeneo mfano hapa mmejenga Maabara kubwa kulingana na wingi wa wagonjwa mnaowahudumia kwa siku, sio kwa sababu ramani imeonyesha maabara ndogo basi mnafuata hivyo hivyo", ameongeza Jafo.
Kituo cha Afya Makole ni miongoni mwa vituo 211 Nchini vilivyopokea/vitakavyopokea fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya Afya kwa lengo la kuboresha miundombinu ya Afya.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni
TAFADHARI !!
- Tumia Lugha Nzuri Kutoa Maoni
Usitumie kauli za Karaha AU Zenye Kukela :
C.E.O
Gneous OG