TAARIFA MPYA
Obama amgaragaza Trump kura za maoni
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Tukiwa tunaelekea kumaliza mwaka 2017 tunayo stori kuhusiana raia wa Marekani kwa mara nyingine wamempigia kura Barack Obama na Hillary Clinton kama mwanaume na mwanamke wanaopendwa zaidi nchini humo katika utafiti wa Gallup 2017.
Utafiti huo umefanywa kwa njia ya simu kuanzia Jumatatu December 4 hadi Jumatatu ya December 11, 2017 ambapo zilikuwa sampuli za watu wazima 1,049 waliopigiwa simu bila kufuata utaratibu wowote katika majimbo yote ya Marekani na Wilaya ya Columbia.
Obama amepata asilimia 17% ya kura wakati Trump akipata 14%, kwa upande wa wanawake Hillary Clinton amepata 9% kura huku mke wa Obama, Michelle akipata 7%.
Bi Clinton ameshinda katika utafiti huo mara 22 na ndiye amewahi kushinda mara nyingi zaidi katika utafiti huo nchini Marekani.
Obama alishinda hadhi hiyo miaka yote alipokuwa Rais na hata baada ya kuondoka madarakani. Baadhi ya marais waliopoteza hadhi hiyo ni Harry Truman in 1946-1947 na 1950-1952, Lyndon Johnson mwaka 1967-1968, Richard Nixon, 1973, Gerald Ford mwaka wa 1974-1975, Jimmy Carter, 1980, na George W. Bush, 2008.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni
TAFADHARI !!
- Tumia Lugha Nzuri Kutoa Maoni
Usitumie kauli za Karaha AU Zenye Kukela :
C.E.O
Gneous OG