Machapisho

TAARIFA MPYA

Madhara ya Chai na Kahawa Kiafya

Picha
CAFFEINA/KAFEINA. Kafeina ni nini?: 1. Kafeina ni madawa ya kulevya kundi la ‘Stimulants drugs’. Utashangaa. Habari ndiyo hiyo. Hii ndiyo sababu kwa mtu aliyezoea kunywa chai hii kila siku au kahawa, siku asipokunywa kichwa humuuma, ni kwa sababu amekuwa mtegemezi au teja wa kafeina. Kafeina ni kiungo mhimu karibu katika soda zote zenye rangi nyeusi; Coca-cola, Pepsi, Sayona nyeusi, Azam cola na kadharika. Kafeina huongezwa pia katika Red bull, Malta na katika baadhi ya dawa za kupunguza maumivu mwilini. Kwahiyo Kafeina ambayo hupatikana katika chai na kahawa ni aina mojawapo ya madawa ya kulevya. 2. Kafeina ni kikojoshi (diuretics). Kafeina ni dawa ya kukufanya ukojowe. Ukinywa kikombe kimoja cha kinywaji chenye kafeina yaani chai au kahawa, basi muda si mrefu utaenda kukojoa vikombe viwili. Kwa sababu kafeina ni taka isiyotakiwa mwilini, mwili utafanya kila uwezalo ikibidi ujikamuwe wenyewe kupata maji ya ziada kuweza kuitoa kafeina hii uliyoinywa kwa kisingizio ch...

Guardiola aongeza rekodi nyingine EPL

Picha
Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola ameweka rekodi ya kuwa kocha wa kwanza kutwaa tuzo ya kocha bora wa mwezi mara nne mfululizo kwenye ligi kuu soka nchini England EPL. Kocha huyo raia wa Hispania ametwaa tuzo hiyo katika miezi ya Septemba , Oktoba , Novemba na Disemba hivyo kuweka rekodi hiyo ya pekee . Guardiola amefanikiwa kuweka rekodi hiyo akiwa ameiongoza City katika michezo 60 ya ligi kuu soka nchini England katika msimu mmoja na nusu tangu awe kocha wa timu hiyo . Katika mechi hizo ametwaa tuzo hiyo mara tano . Katika mwezi Disemba Man City imecheza mechi nane na kushinda mechi saba huku ikitoka sare mchezo mmoja dhidi ya Crystal Palace na kufunga mabao 19 katika mechi hizo . Guardiola sasa amemuacha mpinzani wake Jose Mourinho ambaye tangu aanze kufundisha timu za EPL amefundisha mechi 272 na kutwaa tuzo hiyo mara tatu pekee .

Takukuru kufatiria Matumizi , fedha za Umma

Picha
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ( Takukuru ), mkoani Kilimanjaro imesema mkakati wao mwaka huu ni kufuatilia matumizi ya fedha za umma zinazotolewa na serikali , ili zitumike kama zilivyokusudiwa . Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa Takukuru , Mkoa wa Kilimanjaro, Holle Makungu , alipokuwa akizungumza na wanahabari kuwa serikali inatoa fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo, lakini wapo baadhi ya watumishi wa umma ambao sio waadilifu na kuzifuja. Alisema, ili kuhakikisha lengo la serikali linakusudiwa, mkakati mkubwa watakaoutekeleza katika mwaka huu ni kufuatilia fedha hizo na utaanza zitakapotolewa na wizara kuhakikisha zinafika zote kwa mtumiaji, upatikanaji wa makandarasi, ulipwaji wa kandarasi na ukaguzi wa miradi. “Mpango huu utatoa uhakika kuwa fedha za umma zinatumika ipasavyo kwa ubora uliokusudiwa tofauti na ilivyokuwa awali, fedha nyingi zilichepushwa na kufanyiwa ubadhirifu, ndio maana tumekuwa tukiibua ub...

Ajibu Aipigia Magoti Yanga

Picha
Mshambuliaji wa Yanga , Ibrahim Ajibu . BAADA ya kipigo cha penalti 5-4 dhidi ya URA , juzi mshambuliaji wa Yanga , Ibrahim Ajibu Migomba ameom­ba radhi kwa mashabiki wa timu hiyo kuto­kana na ma­tokeo ma­baya . Yanga ilion­dolewa kwenye michuano ya Kombe la Map­induzi katika hatua ya nusu fainali na URA ya Uganda kutinga fainali dhidi ya Azam FC . Msham­buliaji huyo alisema hawakupenda kupata matokeo ya aina ile lakini ilitokea vile kwa sababu mpira una matokeo matatu. “Naomba mashabiki wetu wa Yanga wa­tusamehe kwa matokeo mabaya hakuna timu ambayo inapenda kupoteza zaidi mtupe sapoti ,”al­isema Ajibu. Hata hivyo katika mchezo huo wachezaji ambao wali­piga penalti ni Papy Tshishim­bi, Hassan Kessy, Gadiel Michael, Daud Raphael na Obrey Chirwa ambaye alikosa.

Neymar Aja na Style mpya ya Ushangiliaji

Picha
Nyota Mbrazil , Neymar Junior akiweka kiatu chake kichwani kushangilia bao la kwanza aliloifungia Paris Saint-Germain dakika ya 53 kwa penalti katika ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji , Amiens SC kwenye mchezo wa hatua ya 16 Bora Kombe la Ligi Ufaransa usiku wa jana Uwanja wa Licorne , Amiens. Bao la pili la PSG lilifungwa na Adrien Rabiot dakika ya 78

Siri ya Yanga kutolewa Mapinduzi cup

Picha
UMAKINI wa safu ya kiungo na ulinzi ya timu ya URA uliiwia vigumu mabingwa wa soka nchini Yanga kuweza kupata ushindi kwenye dakika 90 za mchezo wa nusu fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi . Yanga inayodhaminiwa na kampuni ya Sportpesa jana ilitolewa kwenye michuano hiyo , baada kufungwa kwa penalti 5-4 na Waganda hao ambao sasa wametinga hatua ya fainali . Pamoja na kumiliki mpira kwa asilimia 56, Yanga walikosa mbinu ya kuipita ngome ya ulinzi ya URA licha ya mashambulizi waliyoyafanya katika kipindi cha kwanza. URA imeendelea kuwa mwiba kwa timu za Tanzania baada ya kuzifunga Azam FC na Simba kwenye hatua ya makundi kabla ya kuifunga Yanga jana . Wafungaji wa penalti kwa upande wa Yanga ambayo jana Kocha wake Mkuu , George Lwandamina aliishuhudia timu yake akiwa jukwaani ,  walikuwa ni Papy Tshishimbi ,  Hassan Kessy ,  Raphael Daudi na Gabriel Michael, hu...

Rais Magufuli afanya uteuzi mwingine

Picha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Alphayo Kidata kuwa Balozi. Soma taarifa kamili:

Usajili wa Coutinho waiumiza United kwa Dyabala

Ni mwendo wa pesa tu barani Ulaya, na kwa sasa kila mchezaji maarufu ukimgusa lazima uwe na kuanzia £70m na ndio maana haikushangaza sana kwa Philippe Coutinho kwenda Barcelona kwa dau la £145m. Lakini usajili huu umeanza kuongeza thamani ya wachezaji wengine na vilabu vingine vimeamua kuongeza dau kwa wachezaji wao baada ya kuonekana kwamba lolote linawezekana katika biashara ya sasa ya soka. Moja kati ya vilabu ambavyo inatajwa kuongeza bei ya mchezaji wake ni klabu ya Juventus, ripoti kutoka nchini Italia zinasema kwa sasa Juventus wameamua kwamba kwa timu yoyote inayomtaka Paulo Dyabala lazima ije na £150m. Pamoja na taarifa kutoka kwa mkurugenzi wa Juventus Giussepe Marotta kwamba Juventus haiwezi kumuuza Dyabala kwa kiasi chochote kile cha pesa lakini jarida moja la michezo nchini Italia limefahamu kuhusu mauzo ya Dyabala. Manchester United wanaonekana mstari wa mbele kumnunua Dyabala ambapo hapo mwanzo alitajwa kuwa na thamani ya £80m lakini sasa itawalaz...

U.R.A YAITUPA NJE YANGA MAPINDUZI CUP

Picha
YANGA SC itapanda boti kurejea mjini Dar es Salaam kesho baada ya kutolewa kwenye michuano ya Kombe la Mapunduzi kwa penalti 5-4 na URA ya Uganda kufuatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 jioni ya leo Uwanja wa Amaan , Zanzibar. Yanga SC imeendeleza utamaduni wake wa kufanya vibaya kwenye hatua ya matuta baada ya mshambuliaji wake Mzambia , Obrey Chirwa kumdakisha mpira kipa wa URA, Alionzi Nafian. Chirwa alikosa penalti ya mwisho ya Yanga baada ya wenzake wote wanne, Mkongo Papy Kabamba Tshishimbi na wazalendo Hassan Ramadhani Kessy, Raphael Daudi Lothi na Gardiel Michael Mbaga kufunga. Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Issa Hajji, aliyesaidiwa na Shehe Suleiman na Mwanahija Makame, penalti za URA zilifungwa na Patrick Mbowa, Enock Kigumba, Shafiq Kagimu, Jimmy Kulaba na Brian Majwega. Katika dakika 90 za mchezo timu zote zilishambuliana kwa zamu, ingawa URA ndiyo walioonekana kulitia misukosuko zaidi lango la Yanga. Tofauti na ilivyot...

NI YANGA NA URA, AZAM FC NA SINGIDA UNITED NUSU FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI JUMATANO ZANZIBAR

Picha
YANGA SC itakutana na URA ya Uganda katika Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi Jumatano Uwanja wa Amaan, Zanzibar wakati Singida United itacheza na Azam FC. Hiyo ni baada ya Yanga kutoka sare ya 1-1 na Singida United katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi usiku huu Uwanja wa Amaan. Nusu Fainali ya kwanza itakuwa kati ya Yanga na URA Saa 10:30 jioni na saa 2:15 usiku Singida United na Azam zitachukua nafasi kwa mujibu wa ratiba kama hakutakuwa na mabadiliko. Upo uwezekano mkubwa, mchezo kati ya Azam FC na Singida ukatangulia jioni na Yanga na URA wakahamishiwa usiku. Katika mchezo usiku wa leo wa Kundi B, baada ya dakika 45 ngumu za kipindi cha kwanza, Singida United walitangulia kwa bao la mshambuliaji Daniel Lyanga dakika ya 72 aliyefunga kwa kichwa akimalizia mpira wa adhabu wa kiungo Kiggi Makassy kutoka nje kidogo ya boksi upande wa kushoto. Yanga wakasawazisha katika mazingira yale yale, mpira wa adhabu wa kiungo mshambuliaji Ibrahim Ajib kutoka upande wa kulia ulipounga...

Hali mbaya Sudan wananchi waandamana kisa mkate

Picha
Sudan imekumbwa na maandamano katika miji mbalimbali kutokana na ongezeko la bei ya mkate. Habari zinasema gharama zimeongezeka mara mbili na sababu kubwa ni hatua ya serikali kuondoa ruzuku ya vyakula uamuzi ambao umesababisha bei ya mkate kuwa mara dufu. Maandamano yaliyofanyika magharibi mwa Darfur yamesababisha mwanafunzi mmoja kuuawa na wengine sita kujeruhiwa baada ya kuzuka fujo. Vyombo vya habari vimeripoti kwamba polisi walitumia mabomu ya machozi kutawanya watu ambao walikuwa wamefunga barabara na kuchoma matairi katika barabara za mji mkuu wa Khartoum. Lakini naibu waziri wa mambo ya ndani alisema maandamano hayo hayakutokana na ongezeko la bei na akaahidi kuwashughulikia wote waliofanya maandamano yenye fujo. Pia, Serikali imezuia kuuzwa mitaani magazeti yote yaliyokosoa ongezeko la bei. Vyanzo vya uhakika vimezema uamuzi wa kuongeza bei ya mkate umefikiwa na serikali ikiwa ni utekelezaji wa matakwa ya kufufua uchumi yaliyotolewa na IMF.

Dalili 6 zitakazokuonyesha kuwa mwenzi wako ana mtu mwingine katika mahusiano

Picha
Mahusiano yoyote yale huhitaji mtu mwenye uvumilivu, imara, mkweli na muwazi lakini hivi vyote vikishindikana basi, mahusiano hayo huingia doa. Watu kuwa na wapenzi wawili wawili huenda ikawa sijambo geni, lakini ni jambo geni pale mwezi wako akilifanya. Matatizo haya yamekuwepo kwa miaka mingi, lakini sidhani kama yatakuja kuzoeleka, maana kila mmoja hapa anahitaji upendo wa dhati na wakwake tuu, usio na kugawana na mtu mwingine. Vitabu vya dini vinasisitiza upendo ulio mmoja katika mahusiano yaliyohalalishwa na Mwenyezi Mungu mwenyewe, 'tuliheshimu hili'. Katika makala hii inayolenga kukuonyesha dalili za mwenzi wako kutoka nje ya mahusiano, kwa kiasi kikubwa itakusaidia wewe kuwa sehemu sahihi. Dalili 6 zitakazokuonyesha kuwa mpenzi wako anamahusiano nje ya ndoa au urafiki wenu. 1.  Mmekuwa wawazi kwa muda sasa, yani mwenzi wako amekuwa akishea na wewe mambo mbalimbali ya siku nzima, ghafla anaanza kuchelewa kurudi kutoka kazini, na akirudi hakuambii alikuwa wapi. 2....

Moto wazuka jumba la Trump New York

Picha
Maafisa wa kuzima moto wameitwa katika jumba la Trump Tower katika kisiwa cha Manhattan jijini New York kuzima moto uliokuwa umezuka kwenye ghorofa ya juu ya jengo hilo. Idara ya kuzima moto ya New York imesema moto huo ulidhibitiwa na kwamba hakukuwa na majeruhi. Shirika la habari la CBS News limesema moto huo ulizuka mwendo wa saa moja asubuhi saa za huko (saa sita mchana GMT) karibu na paa la jumba hilo la ghorofa 68. Jumba hilo lilikuwa makazi rasmi ya Bw Trump kabla ya kuapishwa kwake karibu mwaka mmoja uliopita. CBS News wamepakia picha za wazima moto wakiwa kwenye paa la jumba hilo huku moshi ukifuka kutoka kwa sehemu moja ya jumba hilo.

Simba Yatolewa Mapinduzi Cup na U.R.A

Picha
Rasmi Simba wameng’olewa katika michuano ya Mapinduzi kwa kuchapwa bao 1-0 na URA ya  Uganda. Kipigo hicho leo kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar kimekuwa cha pili mfululizo kwa Simba . Mechi iliyopita , Simba ilikutana na kipigo kama hicho kutoka kwa Azam FC na matumaini yao kuendelea ilikuwa leo dhidi ya URA . Bao la URA lilipatikana dakika za nyongeza za kipindi cha kwanza na kipindi chote cha pili, Simba ilishindwa kupata angalau bao moja.

Mbona wanawake wengi hufa kutokana na mshtuko wa moyo kuliko wanaume?

Picha
Ni wamawake wachache ambao hupatwa na matatizo ya mshtuko wa moyo wanaoweza kufa ikiwa watapata matibabu sawa na yale wanayopewa wanaume, uchunguzi umeonyesha. Utafiti huo uliangazia matokeo ya wagonjwa 180,368 nchini Sweden ambao walikumbwa na mshtuko wa moyo katika kipindi cha miaka 10. Waligundua kuwa wanawake wako mara tatu zaidi ya kufa kutokana na mshtuko wa moyo kuliko wanaume wanapopatwa na hali hiyo. Wakfu wa British Heart Foundation, ulisema kuwa mshtuko wa moto mara nyingi huonekana kama tatizo la wanaume lakini wanawake zaidi hufa kutokana na magonjwa ya moyo hata kuliko saratani. Watafiti katika chuo cha Leeds na taasisi ya Karolinska nchini Sweden walikusanya takwimu kutoka na sajili ya ugonjwa wa moyo ya mtandaoni ya sweden. Waligundua kuwa wanawake walikuwa na uwezekano mdogo wa kupata matibabu yanayostahili baada ya kupatwa na mshtuko wa moyo. Prof Chris Gale, wa chuo cha Leeds, ambaye aliandika utafiti huo alisema hii ni kutokana na sababu ya fikra za umma na h...

Ndugai Ampa Pongezi Magufuli

Picha
Spika wa Bunge Mhe . Job Ndugai amempa pongezi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt . John Pombe Magufuli kwa kuweza kusikiliza maoni ya Bunge na wabunge kwa kutekeleza moja ya maombi yao kuigawa Wizara ya Nishati na Madini . Ndugai ametoa pongezi hizo leo Januari 8, 2018 akiwa Ikulu jijini Dar es Salaam katika hafla ya kuapishwa kwa Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Doto Mashaka Biteko na kusema kwa miaka mingi walikuwa wakitaka Wizara hizo kugawanywa lakini ilikuwa inashindikana ila katika awamu ya tano Rais Magufuli ndiyo ameweza kufanya hivyo. "Sisi Bunge tulikuwa tukishauri toka miaka ya nyuma kwa Serikali kwamba Wizara iliyokuwa inaitwa Wizara ya Nishati na Madini ilikuwa ni nzito mno, ilikuwa imejaza mambo mengi sana kwa wakati mmoja ushauri wetu ulikuwa ni vizuri kuzitenganisha na kuzisimika kila moja kivyake. Jambo hili Mhe. Rais umelitekeleza kabisaa kwenye awamu ya tano umeunda wizara mbili na hata tendo la leo linadhirish...

ARSENAL WATEMESHWA UBINGWA WA FA NA 'TIMU YA MCHANGANI'

Picha
Wachezaji wa Arsenal wakierejea katikati kinyonge kuanzisha mpira baada ya kufungwa bao la tatu katika kipigo cha 4-2 mbele ya wenyeji, Nottingham Forest katika mchezo wa Raundi ya Tatu ya Kombe la FA leo Uwanja wa The City Ground mjini Nottingham, Nottinghamshire. Arsenal waliokuwa mabingwa watetezi wanavuliwa ubingwa na kutolewa na timu hiyo ya Daraja la Kwanza, Championship. Mabao ya Nottingham yamefungwa na Eric Lichaj mawili dakika ya 20 na 44, Ben Brereton kwa penalti dakika ya 64 na Kieran Dowell kwa penalti pia dakika ya 85, wakati ya Arsenal yamefungwa na Per Mertesacker dakika ya 23 na Danny Welbeck dakika ya 79 

MESSI, SUAREZ WOTE WAFUNGA BARCA YAUA 3-0 LA LIGA

Nyota wa Barcelona, Luis Suarez, Lionel Messi na Paulinho baada ya wote kufunga katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Levante kwenye mchezo wa La Liga leo Uwanja wa Camo Nou. Messi alifunga dakika ya 12, Suarez dakika ya 38 na Paulinho dakika ya 90 na ushei 

AJIBU nenda Ulaya, usiridhike na Chipsi Mayai

Picha
Priva ABIUD Nmeona umri wa Ibrahim kwenye mitandao. Inasemekana ana Miaka 21. Sawa haina tatizo. Ni umri sahihi kwa mwanasoka mwenye ndoto za kucheza ligi kubwa ulaya. Sijui chochote kuhusu Ajib. Nimemuona mara kadhaa akicheza. Sio kwamba anajua sana. Ila ni mtu ambaye nina iman akipata nafasi hafanyi makosa. Ana mguu wenye ladha ya soka. Mguu wake una maelewano mazuri na mpira. Kimsingi niseme kibongo bongo basi nae anajua jua ila mimi naona bado sana. Siwezi kumfananisha na mshambuliaji yoyote ulaya. Maana hafanani nao kabisa. Bado naona soka lake ni la kitanzania. Lakini umri wake na uwezo wake unafaa kwenda ulaya. Unamruhusu kujifunza lugha ya mpira  wa ulaya nae akawa kama wa ulaya. Nataka nimwambie Ajibu kucheza Yanga na Simba si kitu. Utaishia kututishia kula chipsi mayai na kuendesha Passo lakini kisoka tunakuona mwenzetu tu. Ajib nataka nimwambie sisi tumewazidi Indonesia Viwango vya FIFA. Indonesia wapo nafasi ya 162 huko sisi tupo ya 147. Tena wao walishawahi kushuka ...

Ugonjwa wa Chango La Uzazi

Picha
Tunapozungumzia mgonjwa wa chango tuna maana kuwa ni matatizo yaliyopo katika viungo vya uzazi kwa mke au mume . Huu ni ugonjwa ambao humpata mtu katika umri mdogo utotoni . Kwa mfano :- mume , hupata maumivu ya tumbo mara kueneza anapokuwa mdogo . Kwa upande wa mwanamke hupata maumivu ya tumbo anapoanza kuvunja ungo . Maumivu hayo hupelekea mtu ( mume / mwanamke ) kupata madhara katika viungo vyake vya uzazi. DALILI ZAKE Kwa mwanaume atakuwa akishiriki tendo la ndoa, anawahi sana kufika kileleni na kurudia mara nyingine ni vigumu sana. Pia mwanaume hatakuwa na uwezo wa kusimamisha. Ni vigumu kumpa mimba mwanamke. Mwanamke mwenye chango la uzazi ana dalili zifuatazo:- Kupata maumivu makali wakati anapokaribia kuingia katika siku zake za hedhi Kuhisi maumivu makali wakati wa kushiriki tendo la ndoa Siku zake za hedhi hazitakuwa na ratiba, zitakuwa zinabadilika badilika Hujisikia homa kali anapokaribia siku zake za dhedhi Kupatwa has...

CHELSEA YAKWAA KISIKI KOMBE LA FA, SARE 0-0 NA NORWICH

Picha
Kiungo Mbrazil wa Chelsea, Willian akimtoka beki wa Norwich City, Timm Klose katika mchezo wa Raundi ya Tatu Kombe la FA England jana Uwanja wa Carrow Road mjini Norwich, Norfolk timu hizo zikitoka sare ya 0-0 na sasa zitarudiana kutafuta timu ya kwenda Raundi ya Nne ya michuano hiyo PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

KOCHA MROMANIA WA AZAM AMEKUBALI KWA YULE MGHANA.

Picha
Bosi wa benchi la ufundi la Azam FC, Aristica Cioaba, raia wa Romania na wasaidizi wake, wanakoshwa na soka la mshambuliaji wao mpya, Bernard Arthur raia wa Ghana ambaye amekuwa msaada mkubwa katika ushambuliaji.  Arthur amejiunga na Azam akitokea Liberty Professional ya kwao Ghana, Jumatano wiki hii aliiongoza timu hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Jamhuri kwenye Kombe la Mapinduzi. Katika ushindi huo, Arthur alifunga bao moja kati ya matatu waliyopata na kuiwezesha Azam kufikisha pointi sita kabla ya mchezo wa jana dhidi ya URA na leo dhidi ya Simba.  Cioaba alisema Arthur amekuwa msaada katika safu yao ya ushambuliaji ambayo ilikuwa inafunga mabao machache. “Amekuja vizuri kwa kuingia ndani ya timu na kutupa matokeo yale ambayo tulikuwa tunayataka sisi, utaona kwamba ana muendelezo mzuri wa kufunga tangu alipoanza kutufungia dhidi ya Stand United katika ligi kuu. “Naamini kwa uwezo wake kuna kitu kikubwa ambacho atakifanya kwenye mechi zinazoku...

Serikali yamjibu Lissu

Picha
Saa chache tu baada ya Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu kufanya mkutano na waandishi wa habari katika Hospitali ya Nairobi Kenya ambapo alikuwa akipatiwa matibabu na katika mazungumzo yake kuihusisha serikali na tukio la yeye kushambuliwa Mjini Dodoma September 7, 2017, Msemaji Mkuu wa Serikali Dr Hassan Abbas amezungumza. Kupitia ukurasa wake wa Twitter Dr. Abbas ameandika ujumbe unaosema “Mhe Lissu bado ni mgonjwa na yuko wodini hivyo Serikali haioni busara kulumbana naye kwa sasa, Tunaendelea kumuombea apone haraka.”

Dodoma, Alliance, zaponza waamuzi daraja la kwanza

Kamati ya uendeshaji na usimamizi ya Bodi ya Ligi imewachukulia hatua waamuzi wote waliochezesha mchezo wa ligi daraja la kwanza kati ya Dodoma FC dhidi ya Alliance uliopigwa mjini Dodoma Jumamosi iliyopita ambapo mwamuzi wa kati alikuwa ni Andrew Shamba ambaye alionekana kuboronga zaidi katika mchezo huo na kuchezesha chini ya kiwango. Kitu ambacho kilistua wengi ni mwamuzi huyo kutoa kadi nne nyekundu kwa timu mmoja (Alliance) Afisa mtendaji mkuu wa Bodi ya Ligi Boniface Wambura amethibitisha: “Katika mechi hiyo, waamuzi wote wanne wamefungiwa miaka mitatu kila mmoja na sababu ya kuwafungia ni kwamba walichezesha mechi chini ya kiwango.” “Ripoti ya kamishna imeonesha hivyo na adhabu yao imezingatia kanuni ya ligi daraja la kwanza inayohusu udhibiti wa waamuzi na ikumbukwe kati ya waamuzi hao wawili ni waamuzi wa ligi kuu Tanzania bara kwa hiyo kamati imeona kwamba kama mwamuzi wa ligi kuu anakwenda kuchezesha mechi ya daraja la kwanza chini ya kiwango kamati ilia...

Arsene Wanger Afungiwa

Picha
Kocha Arsene Wenger atatumikia adhab ya kukosa mechi tatu England KOCHA wa  Arsenal,  Arsene Wenger  amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya Pauni 40,000 kwa kumtolea maneno makali refa kwenye chumba cha kubadilishia nguo baada ya mchezo dhidi ya West Bromwich  Jumapili iliyopita.Wenger alikasirika baada ya refa Mike Dean kuwazawadia The Baggies penalti ya dakika ya mwisho baada ya mpira uliopigwa na Kieran Gibbs kumfikia mkononi Calum Chambers. Alimfuata Dean baada ya mechi na kuanza kumtolea maneno ya kulaumu uamuzi wake baada ya Jay Rodriguez kufunga penalti hiyo kuipatia timu yake sare ya 1-1. Wenger alifunguliwa mashitaka na Chama cha Soka England mapema wiki hii na sasa atakosekana kwenye mechi ya Raundi ya Tatu Kombe la dhidi ya Nottingham Forest Jumapili na mechi ya kwanza ya Nusu Fainali ya Kombe la Ligi , maarufu kama Carabao  dhidi ya Chelsea.

Fahamu Aina 7 Za Juisi Zenye Kuondoa Sumu Mwilini

Picha
Sumu mwilini hutokana na vile vitu au vyakula ambavyo binadamu hutumia huenda kwa kujua au kutokujua. Sumu hizo pia huweza kuchangiwa na matumizi ya yasiyosahihi ya dawa mbalimbali. Miongoni mwa mbinu bora na nzuri ya kuondoasumu hizo ndani ya mwili ni pamoja na kutumia vyakula halisi mara kwa mara. Hapa nanayo orodha ya vinywaji ambavyo huweza kuondoa sumu ndani ya mwili:- 1. Juisi ya mchanaganyiko wa tango na spinachi. 2.Jusi ya mchanganyiko wa tangawizi na spinachi. 3. Juisi ya mchanganyiko wa chungwa na tango. 4. Juisi ya komamanga pamoja na mapera 5. Juisi ya changanyiko wa passion na tango 6. Juisi ya mchanganyiko wa apple na parachichi 7. Juisi ya mchanganyiko wa mbegu za maboga na strawberry

Cervical Cancer Saratani Ya Mlango Wa Kizazi

Picha
Saratani ya mlango wa kizazi  Hii ni njia ya kizazi kati ya uke na mji wa mamba.Ugonjwa huu ukijulikana mapema unweza kutibiwa, wakati wa kufanyiwa uchunguzi wa ubwabwa na fupa nyongo. Nani yumo hatarini Wanawake wengine wamo hatarini mwa kupata saratani ya mlango wa kizazi: Wanawake wasioenda kwa uchunguzi wa kila mwaka wa fupa nyongo na ubwabwa Wanawake walio na “human papillomavirus” HPV au genital warts Kuvuta sigara, kuwa na ukimwi,na kutokula vyakula bora huweza kusababisha saratani ya mlango wa kizazi. Dalili ya saratani ya mlango wa kizazi Hamna dalili zozote mpaka unaposambaa nje ya mlango wa kizazi. Hali hii ikitokea waweza kuwa: Kuvuja damu katikati ya siku za hedhi, unaposhiriki ngono au baada ya hedhi kukatika Kuvuja damu nyingi zaidi ya kawaida. Ukiona dalili hizi pata ushauri wa daktari. Saratani ya Utumbo Mpana na Sehemu za Siri za Nyuma  Saratani ya sehemu za siri za nyuma zipo. Huambukiza sehemu za mmeng’enyo (digestive system...

Wivu wa mapenzi wapelekea kuua familia yake

Picha
Mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina la Ammy Lucas Lukule ambaye ni Mhasibu wa Hospitali ya Rufaa Mbeya, amechukua uamuzi wa kuua familia yake kutokana na wivu wa mapenzi. Akizungumza na mwandishi wa www.eatv.tv Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Benedict Kitalika amethibitisha kutokea kwa tukio hilo la mauaji, na kusema kuwa muuaji alifanya tukio hilo usiku wa jana huko nyumbani kwao Kimara jijini Dar es salaam, na kisha kutokomea kusikojulikana. “Ni kweli mwanaume mmoja ambaye anafanya kazi ya uhasibu katika hospitali ya rufaa ya Mbeya, aliyejulikana kwa jina la Ammy Lucas Lukule, ameua mke, mtoto na shemeji yake, inasemekana kulikuwa na ugomvi ambapo mwanaume alikuwa akimtuhumu mkewe kuwa huyu mtoto mdogo sio wake na anajihusisha na mapenzi na wanaume wengine, hivyo aliamua kuwaua kwa jembe na kukimbia”, amesema Kamanda Kitalika. Kamanda Kitalika ameendelea kwa kueleza kuwa baada ya kufanya tukio hilo marehemu aliacha ujumbe kuwa polisi wasihangaike kwani yeye ndiy...

Mark Zuckerberg ameahidi kufanya marekebisho Facebook

Picha
Mark Zuckerberg ameahidi katika mwaka huu wa 2018 kufanya marekebisho kutokana na makosa mengi yaliyojitokeza katika kutekeleza sheria na kuzuia utumiaji mbaya wa mtandao wa Facebook. Mkurugenzi huyo wa Facebook amekuwa na mpangilio wa kujiwekea malengo binafsi kila mwaka tangu 2009. Zuckerberg amesema hayo kupitia ujumbe aliouandika katika akaunti yake ya mtandao huo. Mtandao wa Facebook umekuwa ukikosolewa vikali kwa kuruhusu matangazo yenye uhusiano na nchi ya Russia wakati wa kinyang’anyiro cha uchaguzi wa Urais Marekani mwaka 2016. Hii ni taarifa yake. Every year I take on a personal challenge to learn something new. I’ve visited every US state, run 365 miles, built an AI for my home, read 25 books, and learned Mandarin. I started doing these challenges in 2009. That first year the economy was in a deep recession and Facebook was not yet profitable. We needed to get serious about making sure Facebook had a sustainable business model. It was a serious year, and I w...

Mohamed Salah ashinda Tuzo ya Mchezaji bora wa Afrika

Picha
Mohamed Salah amempiku mchezaji mwenzake wa Liverpool, Sadio Mane na mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang kutwaa Tuzo ya Mchezaji wa Afrika wa Mwaka 2017. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Misri aliibuka mshindi katika kinyang’anyiro hicho dhidi ya wachezaji wenzake katika mkutano wa Tuzo za Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika mjini Accra. Salah, ambaye ataikosa mechi ya Kombe la FA raundi ya tatu dhidi ya Everton, Ijumaa usiku, amefurahia mwaka wa mafanikio kwa klabu na kwa taifa lake pia. Baada ya kufunga mara 10 akiwa Roma kati ya Januari na Mei, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 aijiunga na Liverpool kwa uhamisho wa rekodi kwa klabu hiyo na kwa haraka ameshafanikiwa kuweka kimiani magoli 24 katika michuano yote. Akiongea kuelekea hafla hiyo, Salah aliwaambia waandishi: “Nadhani tuna timu bora ya taifa na tumefanya vizuri kwenye Kombe la Afrika na kufuzu Kombe la Dunia.” Salah pia alizifumania nyavu mara mbili katika ushindi wa Misri wa...

Mvua yazua taharuki Dodoma

Picha
Watu saba wanahofiwa kufa maji kufuatia mvua kubwa zilizonyesha jana Alhamisi mkoani Dodoma. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge amesema watu hao wamekufa baada ya kuzama katika mashimo ya machimbo, makaro ya vyoo na wengine wawili hawajulikani waliko baada ya kusombwa na maji wakiwa kwenye gari eneo la Kikomho Manispaa ya Dodoma. "Taarifa zote kamanda wetu wa polisi atawaambia lakini ni kweli Kongwa kuna watu wawili wamekufa baada ya kutumbukia kwenye shimo la choo wakiwa msibani ambapo mvua zilinyesha na kulivunja shimo hilo wakatumbukia watu sita wawili walikufa," amesema Mahenge. Wengine ni Ramadhani Haruni mtu mzima aliyekufa ndani ya shimo la machimbo ya dhahabu Nzuguni na Daudi Luwinga (16) mkazi wa Nzuguni pia ambaye alitumbukia kwenye shimo la kujenga choo wakati akitoka kwenye mchezo wa mpira. Katika kijiji cha Kikombo gari Toyota Mitsubishi lilisombwa na maji usiku wa kuamkia leo Ijumaa ambapo lilikuwa na dereva na abiria mmoja na wote hawajapatikana. ...

Ronaldo De Lima awafungukia Cristiano na Messi

Picha
Nyota wa zamani wa Real Madrid, Barcelona na timu ya taifa ya Brazil Ronaldo Luís Nazário de Lima amesema Cristiano Ronaldo na Lionel Messi wamefanikiwa kutwaa tuzo za mchezaji bora mara nyingi kutokana na kukosa ushindani. Ronaldo ambaye ni mshindi mara tatu wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa FIFA, amesema anaheshimu mafanikio ya nyota hao wawili lakini ukweli ni kwamba wameyapata kwasababu hakuna watu wengine wa kushindana nao tofauti na zamani ambapo vipaji vilikuwa vingi. ''Cristiano na Messi wamefanya vizuri kwa muda mrefu lakini suala la kuwa wachezaji bora katika kizazi chao limekuwa rahisi aidi kutokana na kukosekana kwa watu wa kushindana nao tofuati na zamani ambapo vipaji vilikuwa vingi'', amesema Ronaldo de Lima. Ronaldo ameengeza kuwa wakati yeye anakuwa mchezaji bora kulikuwa na ushindani mkubwa kuliko sasa. ''Wakati mimi natwa tuzo ya mchezaji bora mara tatu kulikuwa na vipaji vikubwa kama Zinedine Zidane, Rivaldo, Lus Figo pamoja na Ronaldi...

Hali ya Kingunge Yaimalika

Picha
 Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imesema hali ya mwanasiasa mkongwe nchini Kingunge Ngombale Mwiru, inaendelea kuimarika baada ya kuanza kupata matibabu. Akizungumza na Mwananchi leo Ijumaa hospitalini hapo, Ofisa Uhusiano wa MNH, Neema Ngomuo amesema kwa sasa afya yake imeimarika. "Anaendelea vizuri na afya yake imetengamaa, bado yupo chini ya uangalizi wa karibu wa madaktari, baada ya upasuaji aliofanyiwa," amesema Ngomuo. Taarifa za awali zimeeleza kuwa Rais mstaafu, Jakaya Kikwete jana Alhamisi jioni alifika hospitalini hapo kwa ajili ya kumjulia hali mwanasiasa huyo. Kingunge aliyelazwa katika wodi ya Mwaisela, alifiwa na mke wake Pares Mwiru jana Alhamisi saa nane mchana katika wodi ya Sewahaji alikokuwa amelazwa. Neema amesema mke wa mwanasiasa huyo alifikishwa Muhimbili tangu Oktoba 3, mwaka jana. Wakati Peras akifariki,  mumewe Kingunge anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali hiyo. Awali mtoto wa Kingunge, Kinje Mwiru alisema kifo cha mama yake kimeto...

Dr SHEIN Ataka Muungano Ufanyike Z'nzibar pia

Picha
Zanzibar. Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein ametaka jambo linalohusu Muungano linalofanyika Tanzania Bara , lifanyike pia na visiwani humo bila ubaguzi wowote . Dk Shein ametoa kauli hiyo jana katika ufunguzi wa jengo jipya la Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ( SMZ ) liliopo Mazizini nje kidogo ya mji wa Zanzibar. Huku akitolea mfano jengo hilo alisema , “ Kukamilika kwa jengo hili ambalo linafanana na lile la Dodoma ni ishara mojawapo ya kuwa ipo haja kwa kila jambo la muungano linalofanyika Tanzania Bara na Zanzibar linapaswa kufanyika pia ili kutoufanya upande mmoja kujiona kama umetengwa . Si busara kwa mambo ya muungano kufanywa upande mmoja tu au upande mmoja kuonekana unajivutia wenyewe kila kitu , hali hiyo inaweza kuleta madhara makubwa katika utendaji wa masuala ya muungano .” Alisema watendaji wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,...

Wezi Wa Pesa Za Escrow Watajwa na Rugemarila

Picha
Leo January 5, 2017 Mfanyabiashara James Rugemarila anayekabiliwa na kesi ya utakatishaji fedha amewataja wezi wa fedha za Escrow katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kama alivyodai awali kuwa atawataja . Wezi hao amewataja mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu , Thomas Simba baada ya Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Leornad Swai kueleza upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, hivyo anaomba iahirishwe hadi tarehe nyingine. “Mwizi ni Standard Chartered Tanzania Ltd na Standard Chartered Hong Kong ambao wameisababishia serikali hasara ya Trilioni 37, pia nimewapelekea TAKUKURU washiriki wengine wa fedha hizo, hivyo ninaomba niendelee kuwa hai ili nije kuwa shahidi mzuri wa upande wa mashtaka kuhusu wezi hao.” – James Rugemarila Pia Rugemarila amedai kuwa wezi hao ndio wamemuibia hata kwenye kampuni anayoisimamia ya VIP ambayo inawadai Trillion 16. Wakili Swai alidai kuwa ni kweli Rugemarila aliwasilisha taarifa ofisini kwao na wanazifanyia kaz...

Madiwani Wengine Waikimbia Chadema

Picha
Madiwani wawili kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zakayo Chacha Wangwe wa kata ya Turwa wilaya Tarime, na mwenzake wa Kata ya Mwangata Manispaa ya Iringa Mjini, Angelusi Mbogo wametangaza kujivua uanachama wa Chama hicho kwa kile kilichoelezwa kuwa kimepoteza imani yao kwa wananchi huku pia kikiendeshwa kibabe hivyo wameamua kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) ili kuunga mkono juhudi za Rais John Magufuli katika kuleta maendeleo na vita dhidi ya ufisadi.

Hofu ya Kenya ' Sport Pesa , Yawapa Hofu SIMBA ' YANGA YATOA AHADI

Picha
Hofu ya Simba na Yanga kwamba wanaweza kumkosa mdhamini sasa imetoewa . Maan Kampuni ya kubashiri michezo ya kubahatisha ya SportPesa Tanzania imezitoa hofu klabu za Simba , Yanga na Singida United ya kuendelea kuzidhamini kama kawaida . Hiyo , ikiwa ni moja tangu kampuni hiyo kusitisha udhamini wake kutokana na uamuzi wa serikali ya Kenya kuongeza ushuru . Klabu ambazo SportPesa inazidhamini za kutoka Kenya ni Gor Mahia , AFC Leopards na Nakuru All Stars pamoja na Ligi ya Super 8. Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa , Abbas Tarimba alisema kilichokea Kenya cha kusitisha mkataba wa kuendelea kuzidhamini klabu , hausiki kwa Simba , Yanga na Singida United. Tarimba alisema, wao SportPesa wamepanga kuendelea na udhamini wa klabu hizo za hapa nchini tena kwa kuzidi kuziboresha zaidi siku za baadaye ili kuhakikisha klabu hizo zinapata mafanikio. Aliongeza kuwa, tofauti na udhamini wa klabu hizo, pia wamepan...

Arsenal Wakata Tamaa

Picha
Usiku wa jana kwa mara nyingine tena mzimu wa penati unaendelea kumtesa golikipa wa Arsenal Petre Cech , wengi walitarajia Hazard angefunga tuta lile labda kama angepiga nje ya lango la Arsenal. Ni penati ya 15 kwa Cech tangu ajiunge na klabu ya Arsenal akitokea Chelsea, lakini huwezi amini kwamba pamoja na ubora wake wote alionao mlinda lango huyo lakimi hajawahi kuokoa penati hata moja akiwa na Arsenal. Mbaya zaidi ni kwamba kati ya mikwaju ya penati 15 iliyopigwa kuelekea lango lake, mikwaju 3 tu ndio aliweza kuifuata huku mikwaju 12 ya penati aliruka upande ambao mpira haukwenda. Tayari hoja kuhusu uwezo wa golikipa huyo kwenye suala la penati imekuwa kubwa kiasi cha kumfanya mlinda lango wa zamani wa Arsenal David Seaman kuwaomba mashabiki wa Gunnerz kuwa watulivu. Seaman ametoa ushauri kwa Cech kwamba kama anataka ushauri kutoka kwake baasi anaweza kumpigia simu wakati wowote na anaweza kumpa ushauri kuhusu mbinu za kuokoa penati....

Nini Tutarajie Tuzo Mchezaji Bora

Mohamed Salah , Pierre Aubameyang na Sadio Mane wanatoana jasho kuwania tuzo ya mchezaji bora wa bara la Afrika ambapo tuzo hizo hutolewa kila mwaka na mwaka huu zinatolewa mjini Accra. Salah aanapewa nafasi kubwa sana kutwaa tuzo ya mchezaji bora Afrika mwaka huu , hii iko wazi kutokana na kiwango kikubwa sana anachokionesha msimu huu na Liverpool ambapo ndio anaongoza kwa ufungaji EPL. Salah anaonekana kuibeba Liverpool mabegani mwake sawa na alivyowabeba Wamisri na kuwapeleka fainali za kombe la dunia mwakani na ni wazi kwamba sio Mane wala Aubameyang anayekaribia mafanikio yake msimu huu . Dua za raia wa Senegal zitakuwa mbaya kwa Salaah kwani wana kiu sana ya kutwaa tuzo hiyo ambayo tangu  El Hadji Diouf atwae tuzo hiyo mwaka 2002 haijawahi kufika tena Senegal na Mane ndio anategemewa kuipeleka Senegal. Tayari Piere Aubameyang ameshatwaa tuzo hiyo mwaka juzi lakin...